Monday, January 16, 2017

HII NI WOTE WANAO JUWA NA SIO JUWA NINI MASHEIKH WANAFANYIWA KATIKA GEREZA LA SEGEREA KISHA JIULIZE HUU NDIO UBINADAMU JE NCHI HII INA SHERIA JE NCHI HII INA VIONGOZI JE INA VIONGOZI WA DINI NCHI HII.....????

Afbeeldingsresultaat voor kisa za uamsho
MASHEIKH, MAMUFTI WAKUU, MAMAULAMA, MARAISI, MAMAKAMO WA RAISI, WAZIRI MKUU, MAJESHI, POLISI, MAJESHI NA KILA ALIYEKUWA NI BINADAMU ANAE FURAHIYA MASHEIKH HAWA KUWA JELA UKAE UKIJUWA DHULMA DHULMA DHULMA MNAYOWAFANYIA MASHEIKH KATIKA JELA ZENU MJITAYARISHE VYA KUMJIBU M.MUNGU HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA PIA

BARUA YA WAZI TOKA KWA MAHABUSU WA UTUHUMIWA WA UGAIDI GEREZA LA SEGEREA
Kumb:DA.13/PI:29,2014/2016
Mahabusu PI/29/2014
Gereza la Mahabusu
Segerea, Dar es Salaam
28/12/2016
Dar es Salaam

MH. JAJI MKUU MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DAR ES SALAAM-TANZANIA.


YAH: UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Tafadhali husika na mada iliyotajwa hapo juu.
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
tunaelezea uvunjwaji wa haki za Binadamu katika maeneo mawili makubwa, kwa upande wa Mahakama na pili ni kwa upande wa Jeshi la Magereza, hasa kwa Gereza la Mahabusu Segerea Dar es Salaam.
Tukianza kwa upande wa Mahakama kwa kupitia Mahakama ya rufaa (TCA), kwa muda wa miaka mitatu sasa kuanzia tarehe 24/12/2014 mpaka leo hii tarehe 28/12/2016, imeshindwa kupanga tarehe ya kusikiliza rufani ya upande ya mashitaka inayopinga maamuzi ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam yaliyotolewa na Mhe. Jaji Dr Fauzi Twaibu ya kuiambia Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu inao uwezo wa kutoa maamuzi kwenye hatua za mchakato wa ufunguaji wa shauri.Gerelateerde afbeeldingSambamba na hilo Mahakama ya Kisutu pamoja na kuelezwa na Mhe. Jaji Dr. Fauzi kuwa inao uwezo wa kutoa maamuzi imeshindwa kutoa maamuzi kwa madai kuwa upande wa mashtaka umekata rufaa.Gerelateerde afbeeldingVile vile upande wa mashitaka umekuwa ukitumia mgongo wa kutokamilika kwa upelelezi ili wazidi kutuweka jela kwa lengo la kutukomoa na huku wakiidanganya mahakama kuwa upelelezi utakamilika ”Very soon” na huku ikichukua zaidi ya miezi tisa.Afbeeldingsresultaat voor Mufti Mkuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi,Pia Hakimu kuegemea upande mmoja wa wanaoshtakia (Upande wa DPP), mfano Mhe. Hakimu Mwijage akiwa katika kiti cha uhakimu alitoa maelezo kuwa ”Anaongea kama afisa wa Magereza” wakati magereza ndio wanaolalamikiwa na yeye akajisahau kuwa ni Hakimu hapaswi kuegemea upande wowote. Hata hivyo tulimuandikia hakimu mfawidhi wa mahakama ya Kisutu kuhusu jambo hili yenye Kumbukumbu namba DA.10/PI.29.2014/2016.Afbeeldingsresultaat voor Mufti Mkuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi,Vile vile mnamo tarehe 15/12/2016, Mheshimiwa Hakimu Wilbrod Mashauri, tulipo mlalamikia juu ya vitendo vibaya tunavyofanyiwa na jeshi la magereza hapa Segerea kwa kupigwa mshtakiwa namba sita (6) Mohammed Ishaq Yusuph, PI:29/2014 na kupelekwa chumba cha adhabu kijulikanacho kwa ufupi PC kwa muda miezi mitatu (Siku tisini bila ya mapumziko) huku akikoseshwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na waliompiga ni maaskari aitwaye 2upaki na Bahati.Gerelateerde afbeeldingKufungiwa kwenye chumba cha adhabu ambacho ni choo kwa muda wa siku tisini bila ya mapumziko ambayo ni kinyume na wanavyo adhibiwa wengine (Kila wiki wanatolewa siku moja kama ni mapumziko na vile vile kuyasaidia macho kuona vitu vya mbali kutoka kutizama karibu).
Amezuiliwa kufanya ibada kutokana na kuwekwa ndani ya choo, alichukua mswala ili atandike kwa ajili ya kufanya ibada nao amenyang’anywa na afisa usalama anayeitwa Rashid, pia wamemnyang’anya vitabu alikuwa akivisoma.Gerelateerde afbeeldingMhe, Jaji Mkuu wamezuia wanafamilia yake kumtembelea na kumletea huduma yeyote kwa muda wa miezi mitatu akiwa ndani ya adhabu.

Hasa ukizingatia ni mgonjwa mwenye matatizo ya kuanguka na kuzimia ambayo ni matokeo ya mateso na vipigo akiwa mikononi mwa Polisi, aliandikiwa akafanyiwe kipimo cha CT-Scan katika Muhimbili Hosptali tokea 2015 mpaka sasa hajapelekwa Hospitali na tarehe 25/12/2016 ameanguka na kuzimia akiwa ndani ya chumba cha adhabu (pc) na hata alipopata fahamu alilejeshwa tena chumba cha adhabu (PC).
Afbeeldingsresultaat voor viongozi wakuu bakwataSiku tisini za adhabu alizopewa mahabusu Mohammed Ishaq Yussuf amaeanza kuitumikia kuanzia tarehe 05/12/2016 mpaka tarehe 06/03/2017 ambacho atakuwa akipewa robo ya resheni ya chakula cha mchana na maji ya chumvi lita nne (4lita) kwa siku.
Maji hayo atakunywa, atatumia kwa choo (kwenda haja) atakogea, lita nne hizi itakuwa ndio kipimo cha matumizi ya maji kwa muda wote wa adhabu wa siku tisini (90) Miezi mitatu.Gerelateerde afbeeldingMheshimiwa Jaji Mkuu, Malalamiko haya kuhusu mshtakiwa namba sita (Mohammed Ishaq Yusssuf,) tulipomueleza Mheshimiwa hakimu Wilbrod Mashauri ametutaka malalamiko yetu tuyalete mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, lililotushangaza hakuwauliza magereza chochote kuhusu tulichokilalamikia, isipokuwa alisema mahakama yake imefungwa mdomo na mikono.
Mheshimiwa Jaji Mkuu kwa upande wa magereza kumekuwa na udhalilishaji uliopindukia mipaka, utu wa mtu umekuwa haujaliwi kwani mahabusu wote wanaonekana kuwa ni wahalifu wakati sheria iko wazi ambayo inaelekeza kuwa mahabusu hatakuwa ni mhalifu hadi pale mahakama itakapo mtia hatiani.
Mhe. Jaji Mkuu wakati tukiingia gerezani tarehe 17/07/2014 tulimuomba mkuu wa gereza Segerea muongozo wa gereza na kurudia kukumbushia kwa mkuu wa gereza mpya, lakusikitisha mpaka tunaandika maandiko haya hatujapatiwa bila ya sababu za msingi isipokuwa tunaambiwa tutii bila shuruti.Gerelateerde afbeeldingMahabusu kupigwa na kutukanwa matusi ya nguoni haya ni mambo ya kawaida hapa gerezani, huku wenyewe magereza wakiwa wanajisifu kwa kusema hizi rungu walizo nazo ZIMEPITISHWA NA BUNGE KWA AJILI YA KUWAPIGA MAHABUSU. Mfano Mhabusu Hassan Khamis namba PI:41/2014, siku ya tarehe 21/12/2016 wa mahakama ya Kisutu amepigwa marungu kadhaa kwa kukutwa na mchuzi. Askari aliyempiga anaitwa 2paki huku akijisifu kupandishwa vyeo kwa kufanya kazi nzuri.
Mahabusu Kassim Mkadam Khamis alipigwa kwa kukutwa na peni ya high lighter, pia mahabusu Rajabu ambaye ni mgonjwa wa ngiri ambae anakaa cell namba tatu (3) ambayo ni sehemu yanayokaa wagonjwa kesi namba PI:14/2015 tarehe 24/12/2016 pamoja na mahabusu wengine wakati wa zoezi lao magereza la kusachi mahabusu wote alipigwa sana na kila alipojaribu kusema mimi naumwa alijibiwa hivi ”Wagonjwa wako Muhimbili”.Afbeeldingsresultaat voor viongozi wakuu bakwataMahabusu Salim Ali Salim namba PI:41/2014 ambaye amelazwa katika Hospitali ya gereza ijulikanayo Cell namba samba (7) alilazimishwa kutoka ndani huku wakijua hawezi hata pale afisa wa zamu aliposema muacheni amri hiyo haikuheshimiwa inavyostahiki. Je Mhe. Jaji Mkuu, hivi ndivyo sheria inavyosema pamoja na haki za Kibinadamu, mahabusu na wafungwa wa kisiasa?
Mhe. Jaji Mkuu, adhabu zinazotolewa hapa gerezani nyingi haziendani na kosa husika na hazitolewi kwa mujibu wa sheria bali ni kwa utashi tu wa watu.

Mhe. Jaji Mkuu, Mshtakiwa namba sita Mohammed Is’haq Yussuf wa PI:29/2014 adhabu hii aliyopewa kuishi ndani ya chumba cha adhabu kwa muda wa miezi mitatu, siku tisini (90) bila kutolewa na kupewa mlo mdogo usiozidi gramu 80 (80grams) na huku mahabusu huyu akiwa amesharipoti juu ya suala la afya yake na huku magereza wakiwa na taarifa zake kamili, hapa ni wazi jeshi la magereza linaendeleza maelekezo walioyaanza Jeshi la polisi kuhakikisha japo mtu mmoja lazima afariki dunia ndani ya mikono yao.
Gerelateerde afbeeldingKwani adhabu hii hailingani na kosa analodaiwa kulitenda bali inaonekana wazi kuwa ni chuki ndizo zinashawishi utoaji wa adhabu hiyo ambayo tokea tumefika hapa gerezani Segerea tarehe 17/07/2014 haijawahi kutolewa kwa mahabusu yeyote yule wala mfungwa.
Mh. (jaji Mkuu), mshtakiwa kwa kuliona hilo ameamua kugoma kutokula hicho chakula kidogo na leo hii tarehe 28/12/2016 ni siku ya nne.
Mh. Jaji Mkuu, hata unapodai kumuona mkuu wa greza sisi tunaoitwa ”wapemba” PI.29/2014 nayo ni shida kumuona kwa ajili ya kutoa malalamiko.
Gerelateerde afbeeldingMhe. Jaji Mkuu, kumekuwa na kauli mbali mbali za chuki na za ubaguzi dhidi yetu sisi tunaoitwa ”Wapemba”. Kwa mfano siku ya tarehe 05/12/2016 askari anaehusika na kitengo cha upekuzi alimueleza mahabusu Mohammed Is’haq Yussuf wa PI.29/2014 ambaye ni mshitakiwa namba sita kuwa sasa ataruka na wapemba na hata pale Mohammed alipomueleza kuwa atawaambia wenyewe alijibu ninakutuma ukawaambie ”wapemba wenzio”.
Siku ya tarehe 15/12/2016 sehemu hiyo hiyo ya upekuzi wakati tukirudi mahakamani alimuambia mahabusu Hussen Mohamme Ali kuwa ni mchawi na tarehe 21/12/2016 alimwita Hassan Khamis wa PI.41/2014 kuwa ni Mshenzi. Kauli kama hizi tuliziripoti kwa mkuu wa gereza aliepita ACP Abdallah Kiangi na zilikoma kwa muda na sasa baada ya utawata huu mpya zimerudi tena kwa kasi kubwa.
Mhe. Jaji mkuu hapa tunajiridhisha kuwa yale maneno tuliyoambiwa na ”Task force” ya kuwa tumeletwa Tanzania bara kuja kukomolewa ni ya kweli na huenda hizi chuki na ubaguzi ni sehemu ya maagizo waliopewa jeshi la magereza watufanyie.
Mhe.Jaji mkuu, ubaguzi tunayofanyiwa na askari magereza hapa gerezani Segerea haiendani na sera ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli aliyoitangaza siku ya uhuru wa Tanganyika tarehe 09/12/2016 ya kuwa Tanzania ni moja.
Mhe. Jaji mkuu, udhalilishaji huu unaofanywa na jeshi la magereza kupitia gereza la mahabusu segerea ni kinyume cha katiba ya nchi, kinyume cha mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, mahabusu na wafungwa wa kisiasa na ni kinyume cha utawala bora wa sheria.Afbeeldingsresultaat voor viongozi wakuu bakwataMhe. Jaji mkuu, tunakuomba kwa vile wewe ni ndiyo mkuu wa watoa haki katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine husika kwa mujibu wa sheria za nchi hapa Tanzania muunde ”TUME HURU” ili ichunguze usahihi wa tunayoyaeleza ili zichukuliwe taratibu za kisheria kwa kasoro hizi zilizojitokeza ili zisiendelee kuvunjwa haki za binadamu, mahabusu na wafungwa wa kisiasa.
Mhe. Jaji Mkuu kwa sasa tunaishi katika hofu kubwa na hali ya wasiwasi na kuona kuwa usalama wetu uko hatarini kwa namna tunavyotendewa hapa gerezani Segerea.
Uongozi wa magereza unapaswa kuwajibishwa kwa madhara yoyote yanayoweza kutupata mbeleni. Magereza kushindwa kutoa muongozo wa maisha ya gerezani ni kubariki kutokujua haki zetu za gerezani na hivyo kila tunachofanyiwa tuone ni sheria kwetu.
Baada ya miaka mitatu kupita wamejaribu kuweka karatasi mbili zinazoonyesha sehemu ya makosa pasi na kuonesha ni nani anapaswa kusimamia mchakato mzima wa kesi kuwa ni magereza au Hakimu, karatasi hizo mbili hazionyeshi haki wala wajibu wa mahabusu akiwa gerezani.
Tunakutakia kila la kheri na utendaji mwema katika kutekeleza majukumu yako kwa uadilifu.
Kwa niaba ya Washtakiwa wote PI:29/2014 Mahakama ya Kisutu.
Mahabusu Farid Hadi Ahmed Gereza la mahabusu Segerea Dar es Salaam.
NAKALA
1. Makamu wa Rais Jamhuri ya muungano Tanzania.
2. Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Tanzania.
3. Waziri wa Katiba na sheria Tanzania.
4. Mufti wa Tanzania (BAKWATA).
5. Kamishna Generali wa Magereza Tanzania.
6. Tanganyika law society(TLS) Tanzania.
7. Zanzibar law society (ZLS) Zanzibar.

Thursday, January 12, 2017

NCHINI ZANZIBAR MWAKA 1964 DAMU YA WAZANZIBARI ULIMWANGWA BILA YA KOSA LOLOTE KISHA IKAPEWA JINA LA MAPINDUZI DAIMA

Image may contain: plant, outdoor and nature
Afbeeldingsresultaat voor MZEE KARUME,OKELLO,BABU
WAUWAJI WALIO UWA WAZANZIBARI NDIO HAWA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KUFURAHIKIA MAUWAJI WALIO YAFANYA USIKU KAMA WA JANA KUAMKIA LEO.
Image may contain: outdoor
Afbeeldingsresultaat voor MZEE KARUME,OKELLO,BABU
HAWAFIDHINA WA WAKATI HUO WAKILA RAHA ZAO ZA DUNIA LEO HII WAKO WAPI WOTE TAKRIBANI WAKO MAKABURINI HUKO WANAJIBU WALIO YAFANYA
Afbeeldingsresultaat voor MZEE KARUME,OKELLO,BABU
KATIKA KATIKA OKELLO MUUWAJI KUSHOTO MZEE KARUME MUHAFIDHINA WA SIKU HIZO NA KULIA BABU NA PIA MUHAFIDHINA WA SIKU HIZO WALIO KUWA WAKIJALI ZAIDI MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO KULIKO MAUWAJI YALIO TENDEKA KWA KULIWA WATU WASIO NA HATIA WAO HAWAKUJALI WALIJALI UONGOZI TU.
Image may contain: outdoor
Afbeeldingsresultaat voor MZEE KARUME,OKELLO,BABU
HAWAFIDHINA WA WAKATI HUO WAKILA RAHA ZAO ZA DUNIA LEO HII WAKO WAPI WOTE TAKRIBANI WAKO MAKABURINI HUKO WANAJIBU WALIO YAFANYA
Image may contain: bird and outdoor
HII ILIKUWA NI KAMA USIKU WA JANA KUAMKIA LEO WAZE WETU NDUGU ZETU JAMAA ZETU WALIVAMIWA HAPA NCHINI KWETU ZANZIBAR NA HAO LEO TUNAO WAITA ATI NDUGU ZETU WA DAMU NA KUUWA NDUGU ZETU BILA YA HURUMA NA KUPORA MALI ZETU NA MAJUMBA NA MASHAMBA NA KUNAJISI MAMA ZETU ,DADA ZETU ,ANTI ZETU ,HALATI ZETU ,BIBI ZETU WAKAWANAJISI WATAKAVYO KISHA WENGINE WAKAUWA NA WENGINE WAKAWALAZIMISHA ATI WAWE NI WAKE ZAO LEO HII YANAFURAHIKIWA MAMBO HAYA YA HARAMU NA KUPEWA JINA ATI MAPINDUZI MATUKUFU ASTAHAFIRUH ALLAH NYINYI MNAJUWA NINI UTUKUFU NYINYI...? ILA HAKUNA SHIDA DUNIA MAPITO TU WENGI WAO WALIO FANYA HAYO MAPINDUZI WAKO WAPI WENGI WAMENYAMAZA NDANI YA MATUMBO YA ARDHI NDANI YA MWANA NDANI WAO NA MUNGU WAO TU WALIDHANI WAKIFANYA UNYAMA HUU WATAISHI MILELE KUMBE WAPI DUNIA MAPITO TU.

Saturday, December 17, 2016

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ACHA KUITAWALA ZANZIBAR KWA MITUTU WALISHINDWA MAKABURU MTAWEZA NYINYI MAKABURU WEUSI CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA CCM CHA CHANGANYA DINI NA SIASA KISIWANI PEMBA NCHINI ZANZIBAR

Afbeeldingsresultaat voor mabomu na risasi pemba
Afbeeldingsresultaat voor mabomu na risasi pemba
Afbeeldingsresultaat voor mabomu na risasi pemba
Risasi na mabomu yaridima nchini zanzibar kisiwani pemba.

Ugomvi mkubwa umezuka kutokana na kutajwa Shein Kitumwa cha Mkoloni Mweusi Tanganyika katika khutba ya ijuma. Imamu wa Msikiti ambae ni CCM alifanya hivyo mbona CCM mnachanganya Dini na Siasa......? na wananchi wa pemba hawakukubali kitendo hicho kifanyike. Msikiti ulichomwa moto na watu wanaosadikiwa kuwa ni Usalama wa Taifa kwa makusudi ili kuchochea zaidi na lengo lao ni kusingizia wananchi waishio pemba ambao karibia wote ni Wapenzi wa Chama Cha CUF ili waweze kupata sababu ya kuwapiga na kuwafunga jela dikteta shein anaonyesha wazi kuwa siasa imemshinda na sasa anatafuta kilasababu aichafuwe nchi iwe haikaliki akishirikiana na Mkoloni Mweusi Tanganyika.

Milio ya risasi na mabomu yamekuwa yakisikika huko Kangagani kisiwa Pemba nchini Zanzibar. Hali hii imewafanya wakazi wa Kangagani usiku wajana kuamkia leo kuyakimbia majumba yao na kukimbia misituni kupata manusura. Chanzo na Kisa cha kufanya Wananchi wote hawa wasiweze kulala katika majumba yao na kuishia kulala maporini na misituni ni kukata na kupinga jina la Dikteta Shein lisitanjwe kwenye Khutba ya Ijumaa tunawauliza tena CCM mbona mnachanganya Dini na Siasa...? 

Tokea mchana wakati wa Swala ya Ijumaa hali imekuwa tete kwa wakati wa Kangagani kisiwani Pemba nchini Zanzibar ambapo waliswali Ijumaa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika na Mitutu yao na Mabomu ya Machozi huku Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini na Mkuu wa Wilaya ya Wete walio wekwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika na sio kwa kura za Wananchi wote wakiwa wamehudhuria. Wiki iliyopita vijana 7 wamekamatwa na polisi hadi leo hii wako mahabusu.
Bado haijajulikana wa watu wangapi mpaka sasa wameumia kwenye Mashambulizi haya ya jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika la kuwashambulia Wananchi wa Nchi ya Zanzibar hapa Kangagani kisiwani Pemba, lakini inasemekana majeruhi ni wengi.Pia haijajulikana mpaka sasa ni watu wangapi wamekamatwa.

Sunday, December 11, 2016

ABDULLA KASSIM HANGA MWANA MAPINDUZI ALIYE LIWAA NA MAPINDUZI NA KABURI LAKE LISIJULIKANE LILIPO HADI LEO HII

Gerelateerde afbeeldingPili, nawaomba radhi kwamba siko nanyi tukaweza kumzungumza pamoja Al Marhum Sheikh Abdulla Kassim Hanga. Madhumuni ya mhadhara kama huu yawe si kusikiliza tu mtu kama Hanga amesoma wapi, amefanya nini au amekula mandazi kwa mbazi au kunde, lakini yaweze pia kutupa fursa ya kujifunza mawili matatu kutokana na maisha yake.
Yupo wa kumlaumu kwanini sipo hapa nanyi. Na si mwengine ila Muhammad Yusuf kwa ubakhili wake wa kutoniwezesha kufika.
Bado muswada huu ungali “work in progress” na kwa hivyo, kutadhihirika mapengo ya hapa na pale katika nitayoyasema leo. Ni matumaini yangu kwamba kutatokea hapa wataoweza kuyajaza mapengo hayo.Mwisho nataka kuwajulisha kwamba mengi nitayoyasema leo nimeyadokoa kutoka kwenye muswada wangu wa maneno yanayokaribia 20,000 (elfu ishirini), muswada ambao bado haujakamilika kuchapishwa na uitwao “The Killing of Hanga” (Mauaji ya Hanga).
Ama baad,
Wiki iliyopita nilihudhuria hafla moja jijini London ambapo mshairi mmoja binti wa Kipalestina, Jehan Bseiso, akisoma baadhi ya mashairi yake.
Kuna kipande cha mshororo wa shairi lake moja kilichonikaa moyoni tangu nikisikie. Chasema: “Hata waliokufa nao huzeeka…”
Lau angelikuwa hai, Abdulla Kassim Hanga leo angelikuwa “Mzee” wa miaka 84. Alipouliwa 1969 alikuwa kijana wa miaka 37 tu.
Sijui kuna siri gani lakini wanaharakati wengi walio vipenzi vya umma huiaga dunia wakiwa katika rika hilo. Frantz Fanon, aliyezaliwa kisiwani Martinique na aliyeyakumbatia Mapinduzi ya Algeria na akawa Mualgeria, alifariki akiwa na miaka 36; kadhalika, Patrice Lumumba wa Congo, naye alikuwa na umri huohuo wa miaka 36; Walter Rodney, mwanahistoria kutoka Guyana aliyewahi kusomesha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliuliwa akiwa na umri wa miaka 38. Malcolm X naye aliuliwa miezi mitatu kabla hajatimia miaka 40.
Hanga wa kihistoria hakuwa na bahati. Alionewa kwanza na wenzake alioshirikiana nao kuyaandaa na kuyaongoza mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Wao ndio waliomdhulumu roho yake. Akaonewa tena na historia iliyomnyanyua halafu ikamtupilia mbali, asisikike tena.
Hii leo Hanga, aliyekuwa akivuma zama za kupigania uhuru wa Zanzibar, amesahaulika.
Nimesema “amesahaulika” ingawa sidhani kama “amesahaulika” ni tamko sawa. Hanga hakusahaulika. Amesahauliwa kwa kusudi. Watawala hawataki akumbukwe. Nasema hivi kwa sababu kumkumbuka Hanga ni kuufichua uhaini aliofanyiwa na wapinduzi wenzake pamoja na Mwalimu Julius Nyerere, aliyemleta machinjoni Zanzibar ya siku zile.
Kwa kadhia hiyo tu Nyerere hawezi kusafishika. Na nathubtu kusema kwamba itamyima “utakatifu” (sainthood) ambao wapambe wake wanampigania apewe huko Vatikani, kwenye Makao ya Papa.
Angelikuwa Hanga ameishi nchi nyingine, hii leo tungeshuhudia mengi yakiitwa kwa jina lake: majengo, skuli, viwanja vya mpira, barabara au taasisi mbalimbali. Lakini bahati yake ilikuwa kuzaliwa nchi isiyowathamini watoto wake.
NIMKUMBUKAVYO HANGA UTOTONI MWANGU
Ingawa siasa zikimwenda katika damu yake tangu alipokuwa mwanafunzi Hanga aliangukia kwanza kuwa mwalimu kabla hajawa rasmi mwanasiasa. Alikuwa mwalimu aliyekuwa akipendwa na wanafunzi wake wa kila kabila lakini umaarufu wake aliupata katika medani ya kisiasa, hasa katika siasa za usoshalisti wa kimataifa na katika mapinduzi ya Zanzibar.
Mimi binafsi nilianza kumjua alipokuwa mwalimu na nilipokuwa nasoma skuli ya “primary” ya Darajani katika miaka ya kati ya 1950. Wakati huo Hanga alikuwa anamaliza masomo yake ya ualimu katika Seyyid Khalifa Teachers’ Training College, Beit-el-Ras.
Aliletwa Darajani kufanya mazoezi ya kusomesha (teaching practice). Kwa muda mfupi alinisomesha somo la Kiingereza. Alipohitimu masomo yake ya ualimu, akarudishwa skuli ya Darajani ambako pamoja na kusomesha alikuwa pia akisimamia mambo ya riyadha na kuogolea. Alikuwa “sports Master”.
Miaka hiyo ya 1950 mara kwa mara nikikumbana naye jioni nilipokuwa nikitoka kwetu Vuga kwenda Baraste Kipande kumzuru bibi yangu. Nyumba ya bibi yangu ilikuwa karibu sana na nyumba ya dada yake Hanga. Saa hizo za jioni Hanga akipendelea kwenda Jogoo Club kucheza bao au dhumna.
Jogoo Club ilikuwa kama barza ya Mahizbu, wafuasi wa chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Hanga alikuwa Afro, mfuasi wa Afro-Shirazi Party (ASP), chama kilichokuwa kikipingana vikali na kile cha Hizbu. Jogoo ndiyo iliyokuwa nembo ya chama cha Hizbu. Juu ya yote hayo, Hanga hakuona taabu yoyote kwenda kupiga soga Jogoo Club.
Hanga wa siku hizo alikuwa mtu wa mbwembwe na mikogo. Alikuwa na mwendo wa kuyumbayumba, akipiga hatua huku akitikisa mabega yake. Mtu mwengine angelikuwa anakwenda kama yeye angeonekana kinyago cha kuchekwa. Lakini huo mwendo wa mbwembwe ulimsibu Hanga kwa urefu wake na umbo lake. Ilikuwa kama mwendo huo aliumbiwa nao.
Hanga alifanikiwa kuitia mikogo yake bila ya kuonesha kama akijidai. Na hakuwa mtu wa kujidai wala mwenye majivuno.
Wala Hanga hakuwa na watu waliokuwa wakimfuata na kumuigia lakini walikuwepo watu waliokuwa wakimhusudu kwa namna alivyokuwa akiipenda lugha ya Kiingereza. Walikuwepo wengine waliokuwa wakimdhihaki kwa alivyokuwa akiupenda uzungu; si bure kwamba kuna baadhi ya watu waliokuwa wakimwita “Ba Zungu”.
Alikumbwa na ule ugonjwa aliouelezea Frantz Fanon kwenye kitabu chakeBlack Skin, White Mask, ugonjwa uliokuwa ukiwafanya Waafrika wadanganyike kimawazo kwamba wakifikia kiwango fulani cha elimu watakubalika kwa watawala na watapewa dhamana katika dola.
Viongozi wengi wa Kiafrika waliokuwa na hamu ya kuwaiga wakoloni Wakizungu waliambukizwa ugonjwa huo, hata kiongozi mfano wa Kwame Nkrumah katika ujana wake. Na walikuwa nao ugonjwa huo mpaka walipotanabahi kwamba nawasome vipi lakini wakoloni Wakizungu hawatowakubali kuwa ni sawa nao. Daima wataendelea kuwa chini yao.
Hanga aliishi na ugonjwa huo mpaka alipoanza kuamka kisiasa. Mwamko wake, hata hivyo, haukuwa wa mara moja. Aliamka pole pole. Akaanza kufuata itikadi nyingine.
Alipoiangalia jamii ya Zanzibar aliiona jamii iliyogawanyika. Licha ya kuwa na dini moja na utamaduni unaoweza kusema kuwa ulikuwa mmoja kwa kiwango kikubwa, hata hivyo kila jamii (kabila) ilikuwa na ya kivyake. Nadhani hichi ndicho alichokiona mwandishi wetu adhimu wa riwaya, Abdulrazak Gurnah.
Katika riwaya yake inayosifika sana na iitwayo Admiring Silence, Gurnah ameandika kwamba miaka hiyo kila kabila la Zanzibar lilikuwa likiishi katika “historical ghettoes” zake. Kila kabila lilikuwa limefungika na ya kwake. Ndiyo tulikuwa na utamaduni mmoja lakini kila kabila lilikuwa na mkondo wake wa kitamaduni uliokuwa umefungika ndani ya kabila hilo.
Lililozidi kumshughulisha Hanga, aliyekua anaanza kuamka kisiasa, ni imani yake kwamba mfumo wa kikabila uliokuwepo ulilinufaisha tabaka fulani la wakaazi wa Zanzibar na kwamba mtu kama yeye, aliyejiona kuwa ni “Mwafrika halisi”, akiangaliwa vingine. Hanga wa ujanani na aliyeanza kuamka kisiasa hakuamini kwamba Wazanzibari walikuwa wakiishi katika jamii moja iliyojaa furaha tupu.
Wacha nisimumunye maneno, Hanga akiamini kwa dhati kwamba wale waitwao “Waarabu” hapa Zanzibar au wale wanaojinasibisha na “Uarabu” ndio waliokua na ulwa, ndio waliokuwa juu katika jamii na Waafrika ndio waliokuwa chini.
Najua kuna wengi wanaoipinga dhana hii na kuna hoja nyingi ambazo mtu anaweza kuzitoa kuonesha kwamba dhana hiyo ni potovu. Juu ya hayo, hatuwezi kuipuuza kwasababu hisia za waliokuwa wakiiamini dhana hiyo ndizo zilizochangia pakazuka mapinduzi na chuki zinazoenezwa na watawala ingawa si na wananchi.
Isitoshe, kwa sababu ya kuwepo kwa hisia hizo Sheikh Abeid Karume, kiongozi wa ASP, aliweza kuwashawishi zaidi ya nusu ya wakaazi wa Zanzibar kwamba “ukabila” na “upendeleo wa kikabila” yalikuwa mambo ya hakika. Walimuunga mkono kwa sababu walimuona kuwa yeye ndiye sura ya uananchi wa Kiafrika. Wapinzani wake, kwa upande mwingine, walikuwa na hakika kwamba alikuwa sura ya uovu.
Hivyo ndivyo jamii ya Zanzibar ilivyokuwa imegawika siku hizo. Kuiangalia Zanzibar hivyo ni kuitathmini kijuujuu kwa sababu si Waarabu wote waliokuwa katika tabaka la mabwanyenye (bourgeois class), wengi wakiishi maisha ya chini sawa na hao waliokuwa wakiitwa “Waafrika”. Lakini tusiyaingilie hayo kwa sasa asije Hanga akatupotea.
HANGA NA SIASA ZA KIKABILA
Hanga wa ujanani mwake alikuwa akizifuata siasa za kikabila zilizokuwa zikihubiriwa na chama chake cha ASP, kilichokuwa kikiupinga, kile chama hicho ilichokiita “ubwana wa Waarabu”. Hanga akavuka mpaka. Akaanza kuupinga na ufalme, usultani. Kulikuwa gazeti lililokuwa likiitwa MWIBA, ufupisho wa “More Work Illustrate Better Africa”, lililokuwa likimilikiwa na kuhaririwa na Marehemu Jamal Ramadhan Nasib.
Gazeti hilo liliporipoti matamshi ya Hanga ya kuupinga usultani, Jamal Nasib alilazimishwa kumuomba radhi sultani kupitia redio ya Sauti ya Unguja na pia kwenye gazeti la serikali lililokuwa likiitwa Maarifa.
Hanga aliupinga usultani licha ya kwamba dadake, yule aliyekuwa akiishi Baraste Kipande alikuwa mke wa pili wa jamaa wa aila ya Kifalme, Seyyid Farid. Huyu alikuwa mwana wa Sultan Seyyid Ali bin Hamoud, ambaye 1911 baada ya kwenda London kuhudhuria sherehe ya kutawazwa Mfalme George V (wa tano) alilazimishwa na Waingereza ajiuzulu. Ufalme akapewa shemeji yake Seyyid Khalifa bin Haroub, babu yake Sayyid Jamshid bin Abdulla, mfalme wa mwisho wa Zanzibar.
Mama yake Seyyid Ali alikuwa Mnyasa. Alipokuwa mdogo alipelekwa Uingereza kusoma katika skuli ya Harrow na alikuwa mfalme pekee wa Zanzibar ambaye baadhi ya nyakati akiacha kuvaa majokho na akipiga suti na tai. Baada ya kupokonywa ufalme aliishi Paris, Ufaransa, ambako alifariki Desemba 20, 1918.
Kama nilivyokwishasema mwanawe, Seyyid Farid, alikuwa shemeji yake Hanga. Alizaa watoto kadhaa na dadake Hanga.
Kwa vile akiupenda usomi na akizipenda siasa Hanga aliwavutia viongozi wa jumuiya ya African Association ambayo ilikuwa dhaifu. Jumuiya hiyo iliasisiwa 1934 na wafanyakazi Wakiafrika, wengi wao wakiwa wahamiaji Wakikristo kutoka Tanganyika na hadi Malawi.
Haikuchukua muda Hanga akawa kipenzi cha jumuiya hiyo kabla haijaungana na jumuiya ya Washirazi, Shirazi Association, kuunda chama cha siasa cha Afro-Shirazi Party (ASP). Jumuiya hiyo ilimpenda Hanga kwa sababu alikuwa na ujasiri wa kuyatamka yale ambayo yakiogopwa kutamkwa na viongozi wa Jumuiya hiyo waliokuwa wamesoma na waliokuwa wakiogopa wasivitie vitumbua vyao mchanga kwa vile walikuwa watumishi wa serikali ya kikoloni.
Miongoni mwa viongozi hao walikuwa Maalim Aboud Jumbe, aliyekuwa mwalimu wa skuli ya serikali ya sekondari , na Sheikh Ali Khamis, mtumishi wa serikali aliyesomea Uingereza. Watu kama hao waliliacha jukumu lao la kihistoria la kuwatetea Waafrika wenzao.
HANGA AELEKEA ULAYA
Nadhani ilikuwa 1957 baada ya kuasisiwa ASP Hanga alipoondoka Zanzibar kwenda London akifadhiliwa na chama hicho. Marafiki zake wanakumbuka kwamba alikodi chumba katika nyumba ya bibi mmoja wa Kizungu katika mtaa wa Clapham Common, kusini mwa London. Wanakumbuka pia kwamba chumba chake kilikuwa nadhifu sana.
Alipofika alikuwa akisomea masomo ya GCE “A” levels katika skuli ya Westminster College ili aweze kuingia chuo kikuu. Ilisadifu kwamba mwishoni mwishoni mwa 1964 nami nilijiunga na skuli hiyohiyo, iliyokuwa eneo la Westminster karibu na Victoria, kwa madhumuni hayo hayo.
Hanga alikuwa na hamu akimaliza ajiunge na London School of Economics And Political Science (LSE), ambayo ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London. Huko ndiko alikosoma Jomo Kenyatta, Rais wa mwanzo wa Kenya, na ndipo aliposoma Salim Rashid, katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
Bado sikujua kwa nini lakini mambo yalimwendea vingine Hanga. Alipewa msaada wa masomo (scholarship), na akaukubali, wa kwenda Moscow kusomea mambo ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Lumumba.
Kuna jambo jengine lililomtokea London na bado sikuupata undani wake wa namna lililovyoanza. Na jambo lenyewe ni usuhuba mkubwa aliokuwa nao na Oscar Kambona, mwanafunzi wa sheria aliyetokea Tanganyika. Kambona hakumaliza masomo yake kwa sababu Nyerere alimwita arudi Tanganyika kwenda kusaidia harakati za kupigania uhuru.
Hadithi ya Kambona ni ndefu na hapa sipo mahala pake. Naitoshe tu tukikumbusha kwamba Hanga alikuwa na usuhuba naye na kwamba usuhuba huo ulichangia baadaye kuyaponza maisha yake.
HANGA AKIWA MOSCOW
Huko Moscow, Hanga alimuona, akampenda na hatimaye akamuoa mwanamke wa Kirussi, Lily Golden. Lily alikuwa Mrussi mweusi. Babake alikuwa Mmarekani mweusi, John Oliver Golden na mamake, Bertha Bialek, alikuwa Yahudi aliyezaliwa Poland.
Baba mkwe wa Hanga alikuwa mtaalamu wa kilimo na Mkomunisti maarufu kutoka Mississippi. Alikuwa rafiki wa wanaharakati wengine Wamarekani weusi waliokuwa pia maarufu. Miongoni mwao walikuwa mwimbaji Paul Robeson, mshairi wa Harlem na mwandishi Langston Hughes, mshairi mwengine na mwandishi wa riwaya Claude McKay na kiongozi wa wafanyakazi George Padmore.
Nina mengi kuhusu wakwe zake Hanga ambao wote wawili walikuwa Wakomunisti. Hapa nitayafupisha maelezo yao. Kwa ufupi, walihamia Urussi katika miaka ya 1930 ambako binti yao Lily alizaliwa.
Hanga hakumuona babamkwe wake kwa sababu alifariki 1940. Lakini alimuona mama mkwe wake aliyefariki 1985. Binti yao Lily alisomea historia katika Chuo Kikuu cha Moscow State University na baadaye akawa profesa katika Taasisi ya Mitaala ya Kiafrika, Moscow. Aliwahi pia kuuwakilisha Muungano wa Sovieti katika mashindano ya mchezo wa tenis. Alifariki Desemba 2010 akiwa na miaka 76.
Mara ya mwanzo Hanga kumuona Lily ilikuwa 1957 alipohudhuria Tamasha la Kimataifa la Vijana, jijini Moscow. Kuna Wazanzibari wenzake waliomuona mwanzo na wakamhadithia Hanga. Sikuwajua walikuwa akina nani ingawa nadhani Ali Sultan Issa alihudhuria tamasha hilo.
Siku moja saa za usiku 1958 Hanga alipiga hodi kwa Lily, akamlilia hali akitaka kumuoa. Alikuwa ameolewa kwa muda wa miezi michache tu na mpiga piano na mumewe akafa katika ajali ya gari. Huyo mumewe alikua mtoto wa watu, wa familia ya wasomi Wakirussi waliokuwa wakiheshimika.
Lily mwanzo akisitasita kumkubali Hanga lakini mamake akimshikilia amkubali. Ilipita miaka miwili kabla ya Lily kukubali kuolewa na Hanga na ndoa yao ilifungwa 1960. Walijaaliwa binti mmoja, Yelena Khanga.
Nilikutana na Yelena alipopita London akiwa njiani kuja Zanzibar kuwatafuta jamaa zake. Nililetewa na mjombake Hanga, Marehemu Mohamed Ibrahim aliyekuwa baharia aliyeishi London kwa maka mingi. Sadfa nyingine ni kwamba huyu bwana ndiye aliyenipokea London 1964 na akanikaribisha kukaa kwake. Alipomleta Yelena ofisini kwangu akitaka nikamjulishe na Abdulrahman Babu, ambaye siku hizo akiishi London. Ukimuangalia Yelena ni kama Hanga aliyejizaa, sema yeye ni mwanamke.
Yelena anatafahari kuwa yeye ni Mrusi mweusi na Mmarekani. Ni maarufu Urussi kwa vile alikuwa akiendesha vipindi vya televisheni vyenye kuvutia. Yeye na mama yake wote wameandika vitabu. Chake kinaitwa Soul to Soulna cha mama yake kinaitwa My Long Journey Home. Alikiandika baada ya kuhamia Marekani 1988. Mwaka 1993 akisomesha Chuo Kikuu cha Chicago State University.
Masomo ya Hanga Moscow yalikuwa ya muda wa miaka mitano lakini Lily ameandika kwamba alimaliza masomo hayo kwa muda wa mwaka tu. Vipi Hanga aliweza kufanya hivyo sijui.
Hata hivyo, baada ya kumaliza masomo alibaki kwa muda Moscow na akisafirisafiri kwenda Zanzibar na London ambako akishiriki katika mazungumzo kuhusu katiba mpya ya kuipatia uhuru Zanzibar.
Alipokuwa Moscow, Hanga alikuwa akidekezwa na kuengwaengwa na Warussi. Maisha yake na mkewe yalikuwa ya raha. Walipewa fleti nzuri iliyokuwa na vitu vya anasa. Ilikuwa fleti waliyowekewa waheshimiwa kutoka nchi za nje. Lily amesema kwamba alikuwa akipata mambo asiyowahi kuyapata kabla. Walikuwa na watumishi waliokuwa wakiwahudumia. Wakiletewa matunda na nyama. Na waliekewa sinema yao ya kuangalia michezo kwenye chumba chao cha kulala.
Kuna mambo aliyoyasema Lily ambayo yamenivunja moyo. Kwa mfano, ameeleza kuwa japokuwa Hanga alikuwa mfuasi wa Marx na hivyo mtu wa kimaendeleo, moyoni mwake khasa alikuwa mtu wa ujinsia, yaani akipendelea mfumodume. Akaongeza kuwa Hanga alikuwa kama mchukia wanawake (misogynist) kwa sababu alipozaliwa Yelena, alivunjika moyo kwamba hakujaaliwa mtoto wa kiume.
Si hayo tu lakini Lily pia alieleza kwamba Hanga alikuwa na wivu kupita kiasi. Alikuwa hamruhusu mkewe achanganyike na wanaume, hata wenzake kazini au marafiki zake yeye Hanga. Kila Lily alipotaka kutoka ilimbidi kwanza amuombe ruhusa Hanga. Wakiwakaribisha wageni wa kiume nyumbani, Hanga alimlazimisha mkewe akae kimya, asifungue mdomo. Pia alimzuia asende kazini alipokuwa Hanga yuko mjini Moscow.
Hanga alikuwa na wake wengine wawili: mmoja Mguinea na mwengine Mzanzibari, Marehemu Bimkubwa Said “Maghee” aliyekuwa mwalimu wa skuli na aliyefariki dunia Dar es Salaam miaka michache iliyopita.
HANGA NA BABU
Hatuwezi kumzungumza Hanga bila ya kumgusa Abdulrahman Mohamed Babu kwa sababu baada ya Mapinduzi ya 1964, nchi za Magharibi zikiwaona kuwa ndio wakorofi wa Zanzibar waliokuwa na nia ya kuueneza ukomunisti Afrika ya Mashariki nzima.
Babu na Hanga walikuwa waumini wa itikadi ya Kimarx. Lakini Zanzibar walikuwa wafuasi wa vyama tofauti. Babu alikuwa katibu mkuu wa zamani wa ZNP (Hizbu) na baadaye Mwenyekiti wa Umma Party. Hanga alikuwa mmoja wa vigogo vya ASP na aliporudi Zanzibar baada ya kumaliza masomo Moscow aliteuliwa msaidizi wa katibu mkuu.
Hata Ukomunisti wa kimataifa ulipogawika na kuwa na mapande mawili la Sovieti na la China, Babu na Hanga nao pia waligawika. Babu akiwaunga mkono Machina na Hanga Wasovieti. Mapambano ya pande hizo mbili yalikuwa makali.
Hanga na Babu wakitafautiana kwa mengine pia. Kwanza walipita njia tafauti kuufikia Umarx. Hanga aliufikia kwa kupitia tarika ya uananchi wa Kiafrika. Babu, ingawa alikuwa muumini wa umajumui Wakiafrika (pan-Africanism) aliufikia Umarx kwa mtazamo wa kimataifa (cosmopolitan outlook) ingawa siasa zake za awali zilikua zikielemea falsafa ya “anarchism”, ya mfumo wa utawala huria usio na serikali.
Ingawa wote walikuwa na haiba lakini khulka zao zikitafautiana. Hanga akionekana kama saa zote akisononeka, akiwa katika mafikra. Babu lilikuwa jitu la raha, akipenda kustarehe na alikuwa mcheshi na mtu wa mizaha.
Ntatoa mfano wa nämna walivyokua wakiangalia sinema. Wakati Babu akionekana kama mgaagaa na njia (Bohemian) akenda sinema ili kujifurahisha, Hanga, kwa mujibu wa mkewe Lily, alikuwa hendi sinema kwa kujipumbaza tu. Alikuwa akenda sinema alipokuwa akijua tu kwamba atajifunza kitu cha kisiasa, kitachoitanua elimu yake ya kisiasa.
Lily amesema kwamba baada ya kufunga ndoa, Hanga alimwambia amuandikie orodha ya filamu za Kisovieti zitazoweza kumuendeleza kisiasa. Akampa mifano ya filamu bubu Battleship Potemkin na October(maarufu kwa jina la Siku Kumi Zilizoutikisa Ulimwengu). Filamu zote mbili zilifanywa na mwananadharia wa filamu za kimapinduzi Sergei Eisenstein.
Hanga alikuwa kama mtu aliyepandwa na pepo wa kisiasa, aliyehitaji kupungwa. Alikua kama akichukua hatua zake zote kwa sababu za kisiasa, tena siasa kali.
HANGA NA MAPINDUZI
Sitozungumzia jinsi Hanga alivyoshiriki katika Mapinduzi. Dk. Harith Ghassany ameyaeleza mengi kwenye kitabu chakeKwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.
Labda niseme tu kwamba juu ya tafauti zao zote, Babu na Hanga walikuwa na lengo moja wakati wa mapinduzi ya Zanzibar. Hata kabla ya mapinduzi, Babu na wafuasi wake wa Umma Party wakishirikiana na viongozi wa mrengo wa kushoto wa ASP, wakiwemo Hanga, Hassan Nassor Moyo, Abdul Aziz Ali Twala na Saleh Saadalla.
Umma Party haikuyapanga mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 ingawa makada wake walishiriki baada ya serikali ya Shamte ilipokuwa imekwishaangushwa.
Mpangilio wa Serikali ya kwanza ya Mapinduzi ulimuorodhesha Sheikh Karume awe Rais, Hanga waziri mkuu na Babu, waziri wa mambo ya nje.
Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi ulikuwa na vituko vyake. Karume aliwashangaza wote waliohudhuria kwa namna alivyonuna na alivyoukataa urais. Hakutafuna maneno.
“Sitaki kuvishwa kilemba cha ukoka,” aliwafokea wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Hanga alishtuka. Akaanza kubabaika. Karume alisema aliyoyasema kwa sababu akijua kwamba madaraka halisi alikuwa nayo Hanga aliyekuwa waziri mkuu mwenye nguvu za utendaji (executive powers). Cheo cha urais alichopewa Karume kilikuwa kama cha kumfutia machozi.
Hanga alikuwa dhaifu mbele ya Karume na akasema hakuwa akiyataka madaraka aliyopewa. Babu alinieleza mara kadhaa kuhusu kisa hicho na kila mara akinambia kwamba akimvuta suruali yake Hanga chini ya meza ili asiyaachie madaraka lakini Hanga alikuwa amekwishamridhia Karume.
Kisa hiki niliwahi kuhadithiwa pia na Salim Rashid, aliyekuwa katibu wa Baraza hilo, pamoja na nikikumbuka na Khamis Abdalla Ameir, aliyekuwa mjumbe wa Baraza. Kama Sheikh Khamis yupo hapa leo labda atatueleza zaidi. Sisemi kama Hanga alikuwa hajui kuzicheza siasa sawasawa lakini labda ilikuwa moyo wake safi na utiifu wake kwa Karume uliomponza.
Hamna shaka yoyote kwamba lau Hanga asingetetereka basi Zanzibar ingeufuata mkondo mwingine. Kwa hivyo, kuanguka kisiasa kwa Hanga na hata kuuliwa kwake ni mambo aliyojichongea mwenyewe kwa kuridhia kuuacha uwaziri mkuu.
Wadhifa wa uwaziri mkuu ukafutwa na Hanga akateuliwa Makamu wa Rais.
Muungano ulipoundwa miezi mine baadaye Karume akaongezewa cheo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Hanga pamoja na Babu wakahamishiwa Dar es Salaam na wakateuliwa mawaziri.
Hanga alijichongea pia kwa kumshikilia Karume aukubali Muungano. Kwa mujibu wa Sheikh Aboud Jumbe katika kitabu chake The Partner-ship Nyerere alimpelekea Karume wajumbe wawili, Oscar Kambona na Bi Titi Mohamed, kumshawishi akubali kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika. Hakufanikiwa.
Afbeeldingsresultaat voor Abdullah Kassim Hanga
Nyerere alifanikiwa pale tu alipomtumia Hanga na Saleh Saadalla wamshawishi Karume. Ilikuwa kama Hanga alijichimbia kaburi mwenyewe, kwani usuhuba wake na Kambona baadaye ulimghadhibisha Nyerere na lazima ulichangia katika uamuzi wake wa kumpeleka Hanga Zanzibar alikotakiwa na Karume na alikouliwa.
Tangu mapinduzi nchi za Magharibi zilitishika na Zanzibar. Na zilizidi kutishika mwezi mmoja kabla ya Muungano kuundwa pale Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party, alipolisoma uwanja wa Mnazi Mmoja lile liitwalo “Tangazo la Machi 8”. Tangazo hilo liliainisha sera za Serikali ya Mapinduzi. Kwa hakika, tangazo zima lilikuwa ilani ya Umma Party. Ndipo nchi za Magharibi zilipoanza kuiita Zanzibar kuwa ni “Cuba ya Afrika”, hasa baada ya kuimarisha mahusiano yake na nchi za Ulaya ya Mashariki, zikiwa pamoja na Ujerumani ya Mashariki ya wakati huo.
Mwezi uliofuatia Julius Nyerere alimshawishi Sheikh Karume, kwa msaada wa Hanga, kwamba Tanganyika na Zanzibar ziungane. Nyaraka za siri za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) zinaonyesha kwamba Nyerere alichukua hatua hiyo kwa kuhimizwa na Marekani pamoja na Uingereza.
WASIA ALIONIPA HANGA
Mara yangu ya mwisho kukutana na Hanga ilikuwa London. Siku moja mtangazaji mwenzangu wa BBC, Emmanuel Vivian Kassembe, alininong’oneza kwamba Hanga akitaka kuniona pamoja na Wazanzibari wengine wawili: Salim Hamdan, ambaye siku hizi anaishi Maskati, Oman, na Khamis Nura, ambaye sasa ni marehemu.
Salim aliwahi kuwa mhandisi wa Sauti ya Unguja na alikuwa Uingereza akisomea teknolojia ya elektroni. Nura alikuwa mwanasheria wa kimataifa aliyesomea Moscow. Siku hizo akiogopa kurudi nyumbani na akifanya kazi ya ukarani serikalini London. Mimi nilikuwa kijana wa miaka 23 niliyekwishafanya kazi miaka mine BBC na nilikuwa karibu namaliza masomo yangu ya shahada ya falsafa katika Chuo Kikuu cha London.
Kati ya sisi watatu, Nura ndiye aliyekuwa karibu sana kisiasa na Hanga. Na ni Hanga aliyemkuta London akampatia msaada wa kwenda kusoma Moscow.
Lakini siku ya miadi yetu na Hanga ilipowadia, Nura hatukumuona. Kassembe akatuchukua miye na Salim kutupeleka alikokuwako Hanga. Ilikuwa nyumbani kwa Oscar Kambona karibu na stesheni ya treni ya Belsize Park, kaskazini mwa London.
Kambona alitufungulia mlango na kutukaribisha. Kulikuwa vyumba viwili chini ndani ya nyumba hiyo. Kambona alikuwa katika chumba cha mwanzo na mtu mwengine na baadaye Kassembe.
Kambona akatuonyesha mimi na Salim chumba cha pili akisema: “Maalim yuko humo”.
Mara tukamuona Hanga ametoka chumbani akitabasamu na akatukaribisha ndani.
Yeye na Salim wakikaa vitini na mimi nikajipachika kitandani.
“Nimekwiteni kukuhakikishieni kwamba mimi sina matatizo yoyote na Mzee (akiwa na maana ya Karume). Sina matatizo naye lakini anahisi mimi ni kitisho kwake, kwa jinsi ninavyopendwa na watu,” alisema.
Halafu Hanga akatueleza maisha yake alipokuwa waziri Zanzibar na Dar es Salaam. Alitueleza jinsi alivyokuwa akipenda kwenda kwa miguu badala ya kuendeshwa katika gari la waziri na pia kwamba alikuwa akimsikiliza kila mtu aliyetaka msaada wake.
Baada ya hapo akawa kama akitoa mawaidha marefu kupinga ukabila. Alianza kwa kutwambia kwamba alifanya makosa alipokuwa na siasa za kikabila na akatuasa “kama viongozi wa siku za mbele” tuepukane na siasa kama hizo.
Alisema aliwakasirisha baadhi ya viongozi wa ASP alipowasaidia waalimu Wakizanzibari wenye asili ya Kiarabu wapatiwe kazi Bara. Aliwataja baadhi ya waalimu aliosema aliwasaidia wakiwa pamoja na Maalim Salim Sanura na Maalim Shaaban Saleh Farsy. Waalimu wote hao wazuri waliokuwa na ujuzi walifukuzwa kazi na serikali ya Mapinduzi bila ya sababu yoyote ya maana na walikuwa wakizurura tu mjini Zanzibar.
“Nilipowasaidia waje kufanya kazi Bara sikuwaona kuwa wao ni Waarabu. Niliwaona kuwa ni Wazanzibari tu,” alisema Hanga.
Akaanza kunukuu aya za Qur’ani khasa mkasa wa Nabii Musa na Bahari ya Shamu kama ulivyoelezwa humo. Nikimsikiliza lakini nilikuwa na hamu ya kujua fikra zake juu ya Babu na Karume akimuonaje Babu.
“Akiwa Marxist mwenzangu namtakia kheri,” alisema na halafu akaongeza: “Yuko salama kwa sababu si kitisho kwa Karume kama nilivyo mimi.”
Alitwambia kwamba Karume akimuogopa yeye lakini khofu hiyo haikuwa na msingi kwa sababu hakuwa na nia mbaya dhidi ya Karume.
Nilipomuuliza kuhusu mipango yake na atafanya nini, alinijibu hivi:
“Kama ujuavyo nina mke Guinea na amejifungua mtoto wa kiume. Kwa hivyo ntakwenda huo nimpe jina mwanangu kabla sikurudi Zanzibar.”
Alipotutajia kwamba atarudi nyumbani, mimi niliruka nikionyesha wasiwasi wangu na nikamuuliza haogopi?
Hanga alikuwa mtulivu, alimgeukia Salim na akamwambia: “Mtizame kijana huyu. Kwa nini niogope? Sikufanya makosa yoyote. Sikuua wala sikuiba kitu.”
Alitushangaza alipotupa jicho na kukonyeza upande wa ukuta wa chumba alichokuwa Kambona akisema: “Angalau huyo [Kambona] ameiba pesa za TANU.”
Tulimuombea kheri tukaagana naye. Miaka kadhaa baadaye Kambona alinambia kwamba hata yeye alimsihi asirudi Tanzania lakini Hanga hakumsikiliza. Pia alinieleza kwamba Hanga alipofika Conakry alikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na Kwame Nkrumah, aliyekuwa akiishi huko uhamishoni. Nkrumah naye alimbembeleza asirudi, akimwambia kwamba hamuamini Nyerere.
Kambona pia alinambia kwamba hata kabla ya Hanga kwenda Conakry, Nkrumah alimwandikia barua alipokuwa London akimtaka asirudi Tanzania. Lakini Hanga alishikilia lazima arudi. Aliiamini ahadi aliyopewa Rais Ahmed Sekou Toure wa Guinea na Nyerere kwamba Hanga akirudi hatodhuriwa.
Baada ya kuwa na familia yake ya Guinea kwa muda Hanga akafunga safari ya kurudi Tanzania kwa kupitia Cairo. Huko alikaa kwa mwenziwe Ahmed Diria Hassan aliyekuwa balozi wa Tanzania. Sijui walizungumza nini Hanga alipokuwa kwa Diria. Lakini katika miaka ya 1980, balozi mmoja mstaafu wa Tanzania alinieleza kwamba aliambiwa na rafiki yake ya kuwa aliiona barua ambayo Diria alimwandikia Karume akimuelezea kuhusu kukaa kwake Hanga jijini Cairo.
Inasemekana kwamba barua hiyo ilieleza kwamba pale Diria alipomsindikiza Hanga uwanja wa ndege wa Cairo, alimuona Hanga akikumbana na Mohamed Fayek, ambaye wakati wa Rais Gamal Abdel Nasser alikuwa waziri wake wa mambo ya Afrika.
Kwa mujibu wa barua aliyopelekewa Karume, Hanga alikumbatiana na Fayek na halafu wakasimama wakizungumza kwa muda. Pakazuka dhana kwamba Hanga akitaka msaada wa Misri kumpindua Karume.
Nakumbuka 1984, Diria alipokuwa balozi Bonn, Ujerumani, alinialika kwake kwa chakula cha usiku. Nilimuuliza kuhusu hiyo barua anayosemekana kumuandikia Karume. Alikanusha.
Hanga alirudi Dar es Salaam na baadaye alikamatwa kwa amri ya Nyerere na kupelekwa Zanzibar alikotakiwa na Karume. Kabla ya hapo, Nyerere alimuadhir Hanga hadharani katika uwanja wa Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Mkutano ulifanywa karibu na Arnaoutoglou Hall. Nyerere alimwita Hanga “baradhuli”.
Afbeeldingsresultaat voor Abdullah Kassim Hanga
Hii ndio siku ya Nyerere alimuadhir Hanga hadharani katika uwanja wa Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Angalia picha vizuri utaona Hanga yuko katikati ya polisi wawili na Nyerere akimuadhiri mbele za watu.
“Huyu ni baradhuli,” alisema Nyerere. “Mnajua maana ya baradhuli nyinyi? Haijambo liji-Babu [yaani Abdulrahman Babu] linachapa kazi. Lakini huyu baradhuli.”
Gerelateerde afbeelding
Alipofika Unguja, Hanga aliuliwa kwa kupigwa risasi. Inasemekana maiti yake ilifunganishwa na mawe mazito halafu ikazamishwa baharini. Mkewe wa Kirussi, Lily, alijaribu kuulizia yaliyomfika mumewe. Alijaribu hata kumuomba Svetlana Yosefna, binti wa dikteta Josef Stalin, amsaidie.
Hakufanikiwa hadi ulipoporomoka Muungano wa Sovieti. Nyaraka za siri za Shirika la Ujasusi la Kisovieti (KGB) zimeeleza vingine kidogo. Nyaraka hizo zinasema kwamba baada ya Hanga kupigwa risasi maiti yake ilikatwa vipande vipande, ikatiwa kwenye gunia lililozamishwa baharini. Hakuna mwanadamu anayestahili kifo kama hicho.
Nina na “version” nyingine, maelezo mbadala, ya jinsi alivyouawa lakini bado ningali nikiyafanyia utafiti. Hanga, aliyekuwa mtiifu kwa Karume, hakustahiki kuuliwa. Si yeye, si Othman Sharif, si Saleh Saadalla, wala si Abdulaziz Ali Twala. Wote walionewa. Waliliwa na mapinduzi.
Hakuna serikalini aliyetwambia walikuwa na hatia gani au kulikuwa na ushahidi gani wa kuwaingiza hatiani au walihukumiwa na nani. Na huyo aliyewahukumu, au hao waliowahukumu, walikuwa na haki gani ya kuwahukumu? Ni sheria gani iliyowapa madaraka ya kuwa majaji?
Serikali ina dhima si kwa familia zao tu lakini kwa jamii nzima ya Wazanzibari itwambie kwanini viongozi hao waliuliwa na maiti zao ziko wapi.
Tumkumbuke Hanga kama mzalendo Wakizanzibari aliyekuwa mfano wa mwanasiasa aliyeteleza kwa kufuata siasa za kikabila lakini ambaye baadaye alitanabahi kuwa alikosea na akiwataka Wazanzibari waungane, wawe kitu kimoja.
Magharibi ya Aprili 7, 1972 ilipothibitika kwamba Sheikh Karume aliuawa, kuna bibi mmoja kizee aliyetoka nje ya nyumba bila ya kujistiri sawasawa. Alikuwa akirukaruka nje akishangilia mauaji ya Karume. Bibi huyo akiitwa Mashavu binti Hassan. Alikuwa mamake Hanga.