Friday, April 29, 2011

RAZA ASEMA ASIYETAKA MUUNGANO SIO MWANA HALALI WA ZANZIBAR







                                 Aliyekuwa Mshauri wa Rais Zanzibar, Mohammed Raza

Aliyekuwa Mshauri wa Rais Zanzibar, Mohammed Raza, amesema asiyetaka Muungano sio mwana halali wa Zanzibar, kwa vile umesaidia kujenga umoja wa kitaifa na udugu kati ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, mjini Zanzibar jana. “Asiyetaka Muungano sio mwana halali. Na bahati mbaya wanaokataa Muungano hawafahamu faida ya kuwa na umoja,” alisema Raza.
Hata hivyo, alisema Zanzibar kama mdau mkuu wa Muungano, ni vizuri muswada wa kuweka utaratibu wa marekebisho ya Katiba ukapitishwa na wabunge kwa kuzingatia theluthi mbili ya wabunge kutoka kila upande wa Muungano.
Aliwataka wabunge wa Zanzibar kutokubali muswada huo kupitishwa kwa wingi wa kura za wabunge, kwa vile wabunge wa Zanzibar ni wachache ukilinganisha na wa Tanzania Bara.
Aidha, aliwataka Wazanzibari kujenga hoja wakati wa mjadala wa Katiba mpya utakapofika na kuondoa woga na kuwa wakweli katika kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano.  “Wakati wa kuzungumza maslahi ya nchi mbili tuzungumze hoja na tuondoe woga na tuwe wakweli.
Zanzibar tunapenda Muungano. Tusitukane. Tuondoe jazba,” alisema.
Aliwataka viongozi wa dini kufanya kazi ya kuwaombea dua watendaji ili watayarishe muswada mzuri, utakaoleta maslahi ya pande zote mbili za Muungano.
Hata hivyo, alisema matatizo yaliyofikia Zanzibar katika Muungano, yamesababishwa na unafiki wa watendaji ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba (SMZ).
“Matatizo yaliyotufika Zanzibar yanatokana na unafiki wa sisi Wazanzibari. Tusiwabebeshe mzigo wa lawama wenzetu wa Tanzania Bara na kukwepa udhaifu wetu,” alisema Raza.


HILI NDIO JIBU LAKO RAZA NA WENGINE WATA SEMA ZAIDI

WEWE RAZA RAZA TIKE TIKE DENGU CHEEE leo unajuwa kusema sio na ww ushakisoma kiswahili sasa unakizungumza vizuri ndio unatukana watu namnuku alivyosema.asiyetaka Muungano sio mwana halali wa Zanzibar. je nakuliza wewe unamjuwa mwana wa halali wa zanzibar??????? sawa wazanzibar hawataki muungano na wanaukata na wewe unasema hawajuwi faida za muungano. sasa wewe kichwa kimoja ndiye unayejuwa faida ya muungano ila hivyo vichwa vingine vyote havijuwi wala haviona faida ya muungano. sema kweli raza unautaka muungano maana una mabala yako unayoyafanya ambayo yamejificha kwa sababu ya muungano. unajuwa wazi kuwa muungano ukifa hutaweza tena kufanya mabala yako ndio unaupingiya debe sio?unawambiya viongozi wa zanzibar ni wanafiki ww pia ulikuwa kiongozi wakati wa salmin amour na ulibana kimya wewe ndiye mnafiki wa kwanza unawambiya viongozi wa zanzibar waoga wewe tike tike ukisikiya mliyo wa risasi tu ushafika INDIA zamani unatuleteya hapa za kuleta. kaa kimya fanya biashara zako wachiye wazanzibar wajikombowe kama unaona woga wa mali zako nenda huko bara unako wasifu ukaishi huko na mali zako wameja tike tike kama wewe kariako na kongo nenda ukaishi bara hujazuiliwa ila hapa usitulete uchorokochoroko ukatutiribuwa au ndio utakuwa kama mituni na aksheyi utatupinga sote mara moja sio hahahaha



5 comments:

  1. asanteni sana kwa comment zenu ila nawaomba mujiunge hapa na muwache comment zenu hapa maana mulizo wacha zimekuja kwenye email yangu hii ndio blog http://free-zanzibar.blogspot.com

    Author: zengazenga
    Comment:
    huyo jina lake maraza siyo raza kwani yeye nani hana cheo chochote kwenye ccm wanamuona kama kinyago cha mpapure hao ccm siku moja aliambiwa na baba yake usijishirikishe na siasa itakueka pabaya hakusikia sasa anaona hata ccm hawamjali muongo mnafik


    Author: maguvu
    Comment:
    Raza bora kama hujuwi kusema basi bora kaa kimya na tafadhali usitutukane wazanzibar yani unathubutu kuwaita viongazi wetu wanafik na wazanzibari na masheikh kuwa ni wanaharamu? kumbe kweli wewe ni hasidi wa zanzibar umeweka mbele maslahi yako kuliko ya wazanzibar?
    sasa tunakwambia sisi hatutotishwa na binadamu kwa kudai haki yetu na Inshaallah ALLAH yupo pamoja na sisi wewe endelea na kutukashif lakini ipo siku tutafanikiwa na wewe tutakushuhulikia.
    maasalam.


    Author: Mchwaka
    Comment:
    Assallam Allaykum ?
    ALLAH U AKBAR !!
    (Raza Aliyekuwa Mshauri wa Rais Zanzibar, Mohammed Raza, amesema asiyetaka Muungano sio mwana halali wa Zanzibar, kwa vile umesaidia kujenga umoja wa kitaifa na udugu kati ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.sema.)

    Sasa na sisi wazanzibar tunakuambia ww kibaraka wa kihindi RAZA ANAETAKA MUUNGANO NI MWANAHARAMU WA KITANGANYIKA KAMA WW.

    NA UKOME KUJIFANYA KUUTETEA HUO MUUNGANO WW NI MWIZI WA PESA NA MALI ZETU UNACHOTAKA NI SIFA TU HUNA LOLOTE BARADHULI MKUBWA !!!!

    KAMA WW NDIO UNAJUA FAIDA YA MUUNGANO HUU WA KINAFIKI BASI HAYA KWENDA TANGANYIKA, MSHENZI WA TWABIA MWIVI MKUBWA

    ReplyDelete
  2. asanteni sana kwa comment zenu ila nawaomba mujiunge hapa na muwache comment zenu hapa maana mulizo wacha zimekuja kwenye email yangu hii ndio blog http://free-zanzibar.blogspot.com



    Author: nas
    Comment:
    nyie munamsikiliza huyu kumbaro.huyu nimfanyabiashara hajali yeye siasa yenyewe haijui .simunamkumbuka wakati wa salimini amur.


    Author: sundaz
    Comment:
    huyu jamaa alitowa mkanda wa vidio ambao ulikuwa akikemee juu ya muungano haya ndio mambo yanotuponza wazanzibariiiii


    Author: kassem
    Comment:
    Raza ni mtu mwenye kutaka sifa tu na kutaka naye awe midomoni mwa watu. Na hawa waandishi wa habari hawana kazi. Raza ni nani kwa Zanzibar juu masuala mazito kama haya?

    Raza amechukuwa misimamo ya watu walio changia na kutaka kujifanya kama ni ushauri wake. Hilo la thuluthi mbili ndilo lililo pendekezwa na wanasheria wetu na baadhi ya wana zanzibar, pindi ikija hoja ya kujadiliwa bungeni. Nilicho ona mimi hapa jipya kutoka kwa raza hili la kuwaita watu si wana halali, na kama angekuwa nchi kama UK na kutowa kauli kama hii, basi siku ya pili yake angeona cha mtema kuni.

    ReplyDelete
  3. asanteni sana kwa comment zenu ila nawaomba mujiunge hapa na muwache comment zenu hapa maana mulizo wacha zimekuja kwenye email yangu hii ndio blog http://free-zanzibar.blogspot.com



    Author: ashakh
    Comment:
    Wazanzibar
    ipo haja kujenga mtandao imara utakao toa mafunzo kwa kauli zisimo kipimo kama hizi. Mara nyingi nimeeleza umuhimu wa kuchambua maneno yanayosemwa.

    Sisi wenyewe na viongozi wetu hatuna ustaaribu wa usanifu wa lugha. Kila mtu anasema kama vile aliyenyyweshwa maji ya choo.

    Kauli kama hizi ambazo hazina vipimo zinahitaji kukomeshwa. Njia moja ni kukosesha jukwaa la kuzitangazia. Kwani wako wanaotafuta umaarufu.


    Author: misali
    Comment:
    raza ni fisadi asibabaishe watu tena mlarushwa mkubwa anazambi nyingi kwakuwazulumu wazanzibar inatakiwa huyu asikuwepo uraiyani nilazima atumikiye chuo cha mazunzo


    Author: Pandu
    Comment:
    Ashakh.

    Umesema kweli lakini watu wengine wataona wewe pia una mawazo kana Raza unajua mimi kwaupande wangu naona watu wenye upeo na mawazo hawaandiki kitu humu katika mzalendo watu kidogo sana wenye ufahamu lakini wengi wao mazogo tu na matusi .Alichoonge Raza si maneno yakuleta matusi na ujinga lakini ukosefu wa kisomo mimi nimemaliza school 1990 na nikaondoka Zanzibar hadi leo nipo europ na najua au nafahamu elimu Zanzibar imepanda lakini nikisoma maoni ya Vijana naona bado kiwango ziro katika maoni hakuhitaji matusi unaandika point zako ambazo mtu akisoma atafahamu na atafurahi na mawazo yako sio kutukanana sio lengo la Mtandao .Raza katowa point zake na wewe mpinge kwa point zako. na sisi tunaosoma tutapima point gani? inaridhisha .


    Author: Hisba
    Comment:
    Kauli ya Raza “Asiyetaka Muungano sio mwana halali". Mimi naitafsiri kuwa ni matusi kwa sisi Wazanzibari tuliowengi tusiotaka Muungano. Hivyo, wito wangu kwa Raza, aombe samahani kwa kauli hiyo na akikataa basi tunamuomba sheikh Farid tum-jumuishe Raza katika kile kisomo cha waziri Samia. Na vile vile, ikiwa atakataa kutuomba samahani, tumgomee hata DENGU lake tusilinunue alipeleke Mrima akamuuzie Pinda.

    ReplyDelete
  4. asanteni sana kwa comment zenu ila nawaomba mujiunge hapa na muwache comment zenu hapa maana mulizo wacha zimekuja kwenye email yangu hii ndio blog http://free-zanzibar.blogspot.com


    Author: santorini
    Comment:
    Raza,
    Hata wewe raza leo unao mdomo mpana wa kusema asietaka muungano si mwana halali wa nchi hii?,hebu tupe tafsiri kamili ya maneno yako? ikiwa wewe ni mwana halali ,kutokana na usemi wako ,ungelitumia lugha hii ambayo si ya kistaarabu,ni kama kweli unaupenda muungano ungelimsafirisha mke wako kumpeleka canada kila wakati wa uchaguzi ukifika?
    tusiseme mengi tunataka utupe tafsiri ya kwa asie mwana halali wa zanzibar ikiwa si hivyo umejiumbua ,tunakupa wiki mbili.


    Author: uchungu
    Comment:
    wewe raza hujui chochote wewe mnafiki kusikia watu hawataki muungano roho imekuruka kuhusu biashara zako unazofanya tanganyika hakuna jengine mznzbari gani wewe usiewatakia wazanzibar wenzako uhuru hufai kabisa sera zako wewe sawa na huyo pinda wewe ulikuepo hapa serikalini ulikua kazi kujisifu tu na mikopo yako ya baskeli na majembe ukitoa msaada jembe moja tu unataka tvz wakurushe hewani


    Author: uchungu
    Comment:
    wewe raza juzi tu mwaka jana wakati uliposema kuwa bado kuna mpasuko wa ccm ndani ya znz na point yako kubwa ilikua kuwa wastaafu hawakupatiwa usafiri na wengineo kukatiwa umeme na siku ya pili yake MIZUNGUO WAKO PINDA akakujibu hujui kitu kuhusu siasa na wala huna ulazima kuwa ccm sasa leo hii hatukufahamu nini unachozungumza bora nyamazi hatujui tukuweke wapi india , tanganyika au znz

    ReplyDelete
  5. Author: masikini roho yangu
    Comment:
    RAZA ALIKUWA MSHAURI WA RAIS SALMIN WA MICHEZO.SALMIN JUU YA MATATIZO ALIYOKUWA NAYO ALIJUWA KUWA RAZA HAFAI KWA LOLOTE LA MAANA LABDA MICHEZO HUKO, NA AKAFANYE MCHEZO WOWOTE ANAOTAKA YEYE HAYAMUHUSU ILIBIDI AMPE USHAURI HUO KWA SABABU WALIKUWA WASHIRIKA KATIKA BIASHARA NA ALIMPA FURSA YA KUSAMBAZA CHOCHOTE SMZ WANACHOTAKA MAOFISINI HATA MAJUMBANI IKIWAMO FANICHA ZA IKULU SASA RAZA AKATAKA UHESHIMIWA ILI AWEZE KUPITA AIRPORT KIRAHISI PAMOJA NA MIZIGO YAKE MUHIMU PALE VIP HAPO NDIO AKASUKUMIWA HUO USHAURI WA MICHEZO.

    SASA HAPO NDIPO RAZA AKONA KWA NINI NA YEYE ASIWE JAPO WAZIRI AU RAIS SIKU MOJA NDIO AKAANZA KUFUMBUA MDOMO WAKE KIDOGO KIDOGO NA MWISHO AKAONA ACHUKUE FOMU ZA URAIS BAADA YA KUJA RAIS KARUME NA KUMUONDOLEA HIYO MIKATABA YAKE NA SALMIN NA KUMPIGA MARUFUKU KUINGIA IKULU KAMA ALIVYOZOEA,SASA KARUME HAYUPO ALIYEKUWA ANAMUOGOPA NDIO ANAANZA UTUMBO WAKE UPYA PIA ANAELEWA KUWA RAIS SHEIN YUKO KARIBU SANA NA SALMIN HIVYO ANATARAJIA CHOCHOTE TENA NDIO MAANA MNAMSIKIA UPYA, HUYU MTU DUNIA HILO MLIELEWE.

    SAFARI HII JAPO USHAURI WA MIKARAFUU AKIPEWA ATACHUKUA.




    MIMI WALA SIKOSI USINGIZI RAZA AKISEMA NENO HATA AKINAMBIA NYUMBA YANGU INAUNGUA BASI HATA SIWAITI WAZIMA MOTO KWA SABABU NAJUA ALIYENIPA ONYO NI RAZA NA RAZA HAAMINIKI HAFAI HATA KUTANGAZA MPIRA WACHILIA MBALI KUSHAURI UNACHEZWAJE.

    NINGEWAOMBA MUMSAMEHE HUYU BWANA NA KUMDHARAU KWA KUFANYA HIVYO ATAKASIRIKA ZAIDI HIYO KUMSOMEA KISOMO NDIO HAIFAI KABISA KWANI KISOMO ALICHONACHO CHA UJINGA KINAMTOSHA NDIO KINACHOMTIA MASHAKANI HADI LEO.


    NAWASALIMIA.

    ReplyDelete