Tuesday, May 24, 2011

BILAL ASEMA WALIYO CHOMEWA VIBANDA VYEO WAMILIKISHWE ARDHI HAPA ZANZIBAR


huyu ndiye nyerere mpya aliyethamiriya kuwamaliza wazanzibar

bilal umeliona kaburi ndio nyumba zetu hizi sote na wewe unamjegea
mwenzako kesho nakeshokutwa tutakujengeya wewe tenda mema
au endeleya na thulma ya kuwathulumu wazanzibar kisha utakiona
ndani ya nyumba hiii nini faida na nini hasara mimi nakukumbusha tu

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zitaharakisha taratibu za umiliki wa ardhi, ili kuwawezesha wananchi waliochomewa moto vibanda vyao vya biashara katika maeneo ya Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kupata sehemu za kudumu za kufanyia biashara zao.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi hao aliposimama kwa muda katika kambi yao iliyoko mpakani mwa Pwani Mchangani na Kiwengwa.
Akiwa katika eneo hilo, Makamu wa rais ambaye yuko katika ziara yake ya kikazi kisiwani Unguja, aliwapa pole wananchi hao, kufuatia kuteketezwa kwa mali zao katika tukio hilo lililotokea hivi karibuni.
Dk Bilal alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaelewa matatizo hayo na kwamba itafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa wananchi hao wanapewa maeneo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kibiashara.
“Serikali inaendesha shughuli zake kwa kufuata katiba. Hivyo, mtahudumiwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, la msingi ni kwamba muwe na vumilivu,” alisema Makamu wa rais.
Alisema hapa nchini kila mwananchi ana uhuru wa kufanya kazi mahali popote ilimradi tu havunji sheria na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kumnyang’anya mwingine uhuru huo.
Dk Bilal alitoa ufafanuzi huo kufuatua taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Riziki Juma, kuwa wilaya hiyo imetenga maeneo ya mpakani mwa Pwani Mchangani na Majeta kwa ajili ya watu walioathiriwa na tukio la kuteketezwa kwa vibanda vyao vya biashara.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya, maeneo hayo yatatolewa baada hya Wizara ya Ardhi ya Zanzibar, kukamilisha taratibu za umiliki wa ardhi, ili kuepuka madai kuwa watu hao wamevamia.
Kwa upande wao, wananchi waliochomewa moto vibanda vyao, walilalamikia mazingira mabaya ya mahali walipowekwa kwa muda na kuiomba serikali kurekebisha mahema yanayoyatumia kama makazi katika kipindi hiki cha mvua.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, tayari uongozi umeshatoa taarifa za hali hiyo katika ofisi za Idara ya Maafa na za Chama cha Msalaba Mwekundu, ili zishughulikie mahema hayo.
Zaidi ya 50 wengi wao wakiwa ni wenye asili ya Tanzania Bara walichomewa moto vibanda vyao vya biashara katika maeneo ya Pwani Mchangani.Vitendo hivyo vilivyotokea mapema mwezi huu, vilifanywa na watu wasiojulikana

jibu
mimi kwa ushauri wangu kwanza ni kuwa huyu bilal yeye ni makamo wa raisi wa znz au tanganyika.?pia itakuwa vipi watu hao waliyochomewa vibanda wamilikishwa ardhi je hii ndio azimio la arusha na mapinduzi ya 1964 yanajirudia maana ndivyo walivyofanya serekali ikachukuwa maduka yawatu na nyumba zawatu na mashamba ya watu na kuyagawa kama yao je hatujasoma bado tunarudia yale yale..?
ikiwa ni kuwa wapemba wako dar je nilini ulisikiya mpemba dar akapewa ardhi ya bure na serekali ya tanganyika..? wapemba wote wamimiminika jasho ndio wakanunuwa hizo nyumba na maduka sasa hawa wauza vinyango,bangi,unga yani drugs,pombe na wanawake wao wanajiuza mili yao ndio wanavyotoka jasho na sasa ndio bilal anawapa ardhi za bure..?
ndipo ninapo uliza je hii GNU AU SUKARI tuliyo ichanguwa imekuja kuwakombowa wazanzibar au imekuja kuwamaliza kabisa..?maana haimkiniki bilal kusema kuwa hawa watu wamilikishwa ardhi kisa vibanda vimechomwa moto mimi naona wazanzibar kama tunagojeya GNU AU SUKARI basi naona tutagoja sana maana hawa jamaa wameshapaga long time kuichukuwa znz nzima na wazanzibar wakimbiye ili wao wakichukuwe kisiwa na kweli wanafanikiwa maana zamani kanisa la mkunazini halijai na la shangani lakini siku hizi mpaka nje wako haya basi sisi tuendele na usingiza tu na togo za macho

No comments:

Post a Comment