Wednesday, May 4, 2011

HUYU NDIYE MWENYEKITI WA JOPO LA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA LA KUANGALIA KURA YA NORTH SUDAN NA SOUTH SUDAN WAKIJITENGA BENJAMIN MKWAPAA JE MBONA HASIMAMI KUJITENGA KWA ZANZIBAR...?


KICHWA KINAUMA MAANA WAZANZIBAR PIA WANATAKA KUJITENGA ILA SIWEZI KUWAWACHA WALE WAJITENGE HATA SIKU MOJA DAAAH...


Mh. Mkapa aliteuliwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Ban Ki-moon kuongoza timu ya watu watatu watakaofualitia na kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini. Mh. Mkapa amesema kura hiyo ni ya muhimu sana kwa hatma ya mamilioni ya Wasudan ambao Januari tisa watapiga kura kuamua endapo eneo la Sudan Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la na amesema la msingi ni kwa watu kukubali matokeo mara kura hiyo itakapokamilika.. Mh. Mkapa aliyazungumza hayo wakati wa mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa,B. Flora Nducha
Wasudan Kusini wapatao milioni 4 kuanzia Jumapili iliyopita Januari 9 wanapiga kura kuamua hatma yao, je Sudan Kusini ijitenge na Kaskazini na kuwa taifa huru au la.
Uamuzi wa kufanyika kura hiyo umo kwenye makubaliano ya amani ya 2005 yajulikanayo kama CPA. Kwa mujibu wa jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo hadi sasa mambo yamekwenda salama salimin, bila purukushani yoyote kubwa ya kutia dosari. Upigaji kura unakamilika Jumamosi hii Januari 15 na kitakachosubiriwa ni kutangazwa kwa matokeo.
Kama Wasudan kusini wataamua kujitenga basi wataandika historia ya kuwa taifa la 54 barani Afrika. Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amezungumza na mwenyekiti wa jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa akiwa mjini Khartoum kuhusu mchakato mzima wa kura hiyo

JE NDIO WANAJADILI ZANZIBAR KUWA HURU
PIA AU NDIO..........?

MIMI SIO RAIS TENA ILA
BADO NASHAINI HAHAHAH

MSIKILIZE MNAFIKI ANAVYO
SEMA NA HALI ANAJUWA KUWA
WAZANZIBAR PIA WANATAKA KUJITENGA
ILA KABANA KIMYAAA..........
Rais Mstaafu Mkapa, ameyasema hayo siku ya jumatatu wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa yake mbele ya Baraza hilo, ikiwa ni siku mbili zimepita tangu kutangazwa rasmi matokeo ya kura hiyo yaliyoonyesha, kuwa asilimia 98.83 ya wananchi waliopiga kura wameamua kujitenga na kuwa na taifa lao.
“ Timu yetu inapenda kuhitimisha kwamba matokeo ya kura hiyo ya maoni yameonyesha matakwa ya wananchi wa Sudan ya Kusini, mchakato mzima wa upigaji wa kura ulikuwa wa uhuru, haki na wa kuaminika”. Anasema Mkapa.
Akasema kukamilika kwa zoezi hilo ni moja ya hatua muhimu sana kuelekea upatikanaji wa amani ya kudumu.
Baada ya matokeo ya mwisho ya kura hiyo kutangazwa na baada ya pande zote mbili kuridhia na kuyakubali, huku Jumuia ya Kimataifa ikiyaridhia, Taifa huru la Sudan ya Kusini litakaribishwa rasmi katika Jumuia ya Kimataifa Julai 9 mwaka huu.
Mkapa ambaye timu yake ilitembelea Sudan ya Kusini mara tano katika kipindi cha kuelekea upigaji wa kura hiyo. Amelieleza Baraza hilo kwamba, katika kutathimini mchakato huo wote, timu yake ilizingatia misingi yote iliyoainishwa katika Sheria ya Kura ya Maoni ya Sudan ya Kusini. Na kwamba Timu imejiridhisha kuwa zoezi lilifanyika katika mazingira ya uwazi wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment