Tuesday, May 3, 2011

JE UKIWA WEWE NI MZANZIBAR KWELI UTASHEREHEKEYA SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 1964...?

Idadi hasa ya wazanzibari waliokuwa katika Mapinduzi haijulikani. Inakisiwa tu kuwa ni kiasi ya watu 2,000 hadi 20,000. Hata hivyo, kilicho bayana ni kuwa idadi ya wahanga - miongoni mwa jeshi la serikali ya zanzibar na lile la Mapinduzi ilikuwa ndogo mno. Kiongozi wa Mapinduzi hayo anaripoti kuwa alipokea taarifa ya wahanga hao tarehe 13 Januari, saa 9:30 alasiri baada ya mfalme kulazimishwa na vikosi vyote vya serikali mpya ya zanzibar ambayo ndio serekali huru ya watu wa zanzibar 1963 inayojulikana hata umoja wa mataifa kushindwa. Anaadika kuwa katika ushindi wao wa Zanzibari - yaani ule wa ghala ya silaha na ule wa vikosi vya serikali ya zanzibar  -  upande wake ulipoteza askari 2 na kujeruhiwa wengine 18. Ama kwa upande wa serikali ya zanzibar  katika mapigano haya mawili yaliyopishana kwa takribani masaa 2, majeshi 16 waliuawa na 81 wakaachwa majeruhi.
 
Wakati wa kuziteka ngome nyengine za serikali ya zanzibar  asubuhi hiyo, mauaji zaidi yalitokea. Hata hivyo, hisabu ya jumla ya wahanga wote katika "medali ya vita", ikijumuisha na ya ziwani, ilikuwa ni askari 9 tu waliouawa na 173 tu walijeruhiwa kwa upande wa jeshi la Mapinduzi,na 70 tu waliouawa na 401 walijeruhiwa kwa upande wa vikosi vya serikali ya zanzibar . Askari na wapiganaji wengine 818 wa serikali walijisalimisha aidha wakati ama baada ya mapambano. Idadi hii ya wahanga 653 tu miongoni mwa waliouawa na waliojeruhiwa, kwa pande zote mbili, hailingani kabisa na ile idadi ya maelfu ya wahanga waliopoteza maisha, viungo katika pirika-pirika za muendelezo wa Mapinduzi ya kutaka kuipinduwa serekali ya watu wa zanzibar. 


Viongozi wa Mapinduzi hawakuwa na mpango wa kabla juu ya nini wawafanye "maadui" zao endapo wangeliwashinda. Ukosefu huu wa mpango ulizaa dalili za ukosefu wa nidhamu katika kupeana vyeo vya Mapinduzi, huku uchu, ulafi na uoga zikiongoza nidhamu hii. Uporaji ulianza mara tu baada ya Mapinduzi kutangazwa, bali khofu na mateso dhidi ya wazanzibar  (waliopinduliwa) vikaonekana kuwa vitu vilivyotawala hisia za watu kwa siku mbili mutawaliya zilizofuatia Mapinduzi . Khofu hizi ndizo silizowaruhusu baadhi ya watu wajiingize katika uvunjaji mkubwa  wa sheria, kwa bahati mbaya, kiongozi wa Mapinduzi hayo alionekana kuwa mmoja miongoni mwa   hao. Sio tu kwamba yeye binafsi alishiriki katika ukatili wa hali ya juu, bali pia aliendelea kutumia Redio akitangaza njia ya mikakati ya kuwahamasisha watu wake wamwage damu kwa wingi ili kuwatisha na kuwathofisha wazawa wa zanzibar na kufuata amri yao.
 
Vingi miongoni mwa vyombo vya nyumba za Zanzibar kwa wakti huo vilijumuisha silaha, miongoni mwao zikiwa bunduki kongwe zilizonakshiwa kwa mkono na ambazo zilikuwa urathi wa kizazi hadi kizazi. Watu walioishi maisha ya nafuu katika sehemu za mashamba, pia walikuwa na silaha walizopewa kwa ajili ya kujilinda. Mambo haya mawili, pamoja na ukweli kuwa wengi wa wakaazi wa mjini walikimbilia kwa ndugu zao wa  mashamba pale ghasia zilipokaribia mji mkongwe yakawa ni kichocheo kikubwa cha mauaji ya maangamizi. Ubinadamu,ukarimu,upendo,maskilizono na umoja wa watu wa zanzibar ambao uliokuwepo kisiwanii humo kwa mara ya mwanzo ukatikiswa najazba ya safisha-safisha ya chuki,ukatili,mauwaji ya wazi wazi,wanawake kuharibiwa na watu wengi wasio na hatia kuliwa isiyopata kuonekana hapo mwanzoni katika upwa  huu wa visiwa bora vya zanzibar. Haya hapa maelezo kutoka kiongozi wa Mapinduzi mwenyewe yakisimulia mkasa huu.
"Vita ni dhamana ya kuogofya na matokeo yake daima ni uharibifu mkubwa. Hakuna chochote kiwezekanacho kuthibitisha hili zaidi ya vita vilivyotokea tarehe 12, Bubwini Kaskazini Unguja, eneo ambao waliishi waarabu wengi. Eneo hili lilikuwa ni kituo cha kuhifadhia silaha ambazo waarabu hawa walikusudia kuzitumia katika mauaji ya maangamizi dhidi ya waafrika.
                                                                                                            
Kwa hakika walipanga kufanya shambulizi  hilo siku ya tarehe 13 Januari. Nilipata habari hizi kutoka kwa kijana aliyekuwa karibu kuuawa na wanajeshi  Wazungu. Wanajeshi hawa walikuwa tayari wameshawaua watu 40 katika eneo hilo na nilikuwa na bahati ya  kuwasili hapo wakiwa wanataka kummaliza kijana huyu kwa risasi. Nilipomsaili zaidi, kijana huyu aliniambia kuwa silaha zilikuwa zimehifadhiwa katika eneo hili na wazanzibar  walishapanga kuzitumia hivi punde tu; pia aliniambia kuwa wengi miongoni mwa wale waliouawa na askari wazungu hawakuwa wakaazi wa nyumba walizokutwa. Habari hizi za uovu zilithibitisha habari nilizozipata hapo kabla na nilichukizwa sana. Niliwaamuru askari wangu wafyatue risasi kila upande na wakiuwe kiumbe chochote kilicho mbele yao- wanaume, wanawanake, watoto, walemavu na hata kuku na mbwa"   
          
Wimbi la mauaji huko mashamba na mashambulizi katika sehemu nyengine zilizochukuliwa kuwa za "maadui" yalikuwa yanatishia sana. Habari zinazosimuliwa zaidi ni zile baadhi ya watu wa zanzibar  wasio na hatia wakiwa na silaha zao duni ambao walihiyari kujifungia katika majumba yao huku umma usiozuilika ukiwazingira. Vikosi vya Askari wa Mapinduzi vilikuwa vikipita nyumba hizi moja baada ya nyengine katika magari ya doria; na walipowasili kwenye nyumba ya aina waliyokuwa wakiishambulia kwa bunduki za automatiki. Akizungumzia ubaya wa "mapambano" haya, kiongozi wa Mapinduzi alisema: "Ni Mungu tu awezaye kuujua ubaya wa mapigano haya kwa wakati huo; risasi zilimiminika mithili ya wingu la mvua, na mashambulizi yalisambaa kisiwa chote".

Baada ya muda. "maadui" waliyakimbia majumba yao kukimbilia vichakani na pengine pwani. Wachache walinusurika kwa kusafiri na vimashua walivyovikuta pwani. Wengine waliuawa ama kuchukuliwa mateka. Mauaji ya wafungwa yalikuwa jambo la kawaida na wengi wao walikufa baadaye kutokana na mateso mabaya gerezani au katika kambi mpya za wafungwa zilizofunguliwa baada  ya kiu ya damu kwisha.


                                                                                                             



Siku mbili baada ya Mapinduzi, mpiga picha wa kitaliano alipiga picha zilizozaa makala hii. Picha hizo zinaonesha misururu mirefu ya wafungwa, watu wakikimbia kupitia pwani, maiti waliozagaa ufukweni, mauaji ya wafungwa, usafishwaji wa miili ya wahanga na makaburi ya halaiki ya watu wa zanzibar wasio na hati waliuwawa.
 



                                    


Makala hii imeandikwa kama ni kumbukumbu ya wale wote waliopoteza maisha yao wakati wa Mapinduzi ya zanzibar ya mwaka 1964.na ndio mwaka ambao zanzibar ilipoteza uhuru wake na kuishia ktk mikono ya wakoloni wausi tanganyika.

                            

No comments:

Post a Comment