Tuesday, May 24, 2011

JE VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NI VIONGOZI AU NI WASANI WA RAP



Siku hizi, wataalamu wengi wanazungumzia dhana ya utawala bora. Imekwua midomo haipumziki, bila kuitaja ‘utawala bora’. Lakini, kusema kitu chengine na kufanya jambo nyengine kabisa. Aghlabu, dhana hii, kwa nchi kama zetu, huambatana na watendaji wa serikali husika, na pesa, kupata pesa za wafadhili tu. Basi.
Sasa angalieni utawala bora Zanzibar:
1. Jaji ametoa hukumu ya kuwa wenye makontena pale Darajani, waruhusiwe kufanya shughuli zao, na makontena yafunguliwe. Baraza la Mji wa Zanzibar limekataa mari ya mahkama. Kwa ufupi, hukumu,imetolewa kuwa rukhsa kuendelea kufanya biashara hapo. Just mtu mmoja wa Baraz ala Mji amepinga amri hiyo, kwa hisia zake za ukereketwa.
2. Wasomi wetu wenye madigree kibao, awali, wameipeleka kesi ya wanaodaiwa kuchoma moto vibanda vya watoto wa waflme wetu kule Pwani Mchangani, isikilizwe mahkama kuu. What? Mahkama kuu ili kuwaridhia wabwana zetu. Kesi hii mimi niliyekuwa zuzu wa sheria, ninajua kuwa si kesi ya kwenda mahkama kuu — hii ni kesi ya district court au tuseme regional magistrate.
Lakini, kwa vile tunataka kuwaridhia wafalme, lazima tuonekane kuwa ni jambo kubwa, tumevunja na kutia moto palace. Jana, kwa aibu, uamuzi mwengine umetolewa kuwa kesi ihamishiwe mahkama ya Mfenesini. Hivi kweli jaji aliyeichukua kesi hii tokea mwanzo hajui hili. Ina maana ni hatari wanasheria wetu, kuwa basic ya ABCD ya sheria hawaijui.
Hiyo ndio faida ya kuweka watoto wetu ndani mfumo wa sheria. Lakini msisahu kuwa kuanzia mrafjis, mpaka muendesha kesi, anatoka huko huko Tanganyika, ni ama Abraham Mwanpashe au jaji…gani sijui. Tumewaleta wenyewe ili wawahukumu CUF (enzi zile) sasa wanatupanda juu ya kichwa. Bado….tutaona. Na tutazidi kuona. wazee wetu walisema ‘ukitaka nyingi nasaba, utapata mwingi msiba’.
Hivi kweli mtu kama Abubakar Khamis Bakari, Waziri wa Sheria (kutoka CUF: Slogan — Hakiiiiii, hakuliona hili?) kama hakuliona hafai – na ajiuzulu. Udhaifu wa kujua kazi, au vacuum kama jiyo, ndio anakuja Dr.Bilali anasema vile anavyoona yeye kuwa sasa ardhi ya watu wazawa, wapewe jamaa zake wa Kijaluo, na Kimasai n.k. Jamani mtu kwao, Dr.Bilali Mjaluo wa Uganda, lazima atavutia watu wake waje hapa Zanzibar. Watu tusiokuwa na hisia nzuri za kwetu ni sisi wazanzibari tu, tunatiana visu vya roho wenyewe kwa wenyewe.
Hili jengine si letu. Lakini nitalisema. Mauwaji ya Raia Tarime. Ploisi imeuwa, lakini hakuna aliyesmea kuwa kuna ukiukwaji wa haki za binadamu Tanzania. Nilidhani kuwa serikali itawatia mbaroni waliouwa na kushtakiwa. Leo, wanalaumiwa ‘maiti’ kuwa wao ndio chanzo cha vurugu, an Chadema….iwe ndio hivyo, lakini hakuna justification ya kuuwa. Heko Utawala Bora TZ.
Gumzo la mji leo hapa mjini na vitongoji vyake, ni kuhusu kesi ya Pwanimchangani. Ni aibu kwa mahkama, ni aibu kwa wanasheria, ni aibu kwa utendaji mzima wa SMZ-GNU. Ni aibu hata kwa mtu kama Maalim Seif ambaye alisimamia slogan ya HAKI huko nyuma, sasa amebaki kuzungumzia ‘maharamia wa kisomali tu’. Labda sasa tumpangie kazi katika department ya CIA ya ‘counter-terrorism’ aende kumsaka Al-Zawahir, Mullah Omar, n.k
UFAFANUZI KUHUSU ZIARA ZA VIONGOZI/WATENDAJI WA SMZ-GNU PEMBA
Niliposema kuwa ziara zimekuwa nyingi kisiwani Pemba, sina maana viongozi wasiende huko au kuwa Pemba walikuwa wanalalamika kuwa ‘wametupwa na sasa ndio wanaenziwa’ kama walivyochangia wengine. Ninachozungumzia mimi mimi ni kuwa ziara hizi
1.hazizai matunda yeyote 2. duplication ya ziara juu ya ziara – utaona kiongozi mmoja anakwenda Pemba kumtambulisha Naibu Katibu Mkuu, the same week, anarudi na anakwenda tena kumtambulisha mkurugenzi mpya aliyeteuiliwa jama yake n.k
3. Chukulia ziara kama ya Msham Abdulah Khamis – yeye kila siku anakwenda Pemba na kurudi, na analazimisha apatie gari maalum hata kama gari hiyo ina kazi rasmi ya kiserikali, atiliwe mafuta full tank, na lazima akae katika hoteli fulani (Mbuyu Mkavu) na chumba chake hicho hicho; hata kama kuna mgeni atolewe. Na wengine kama yeye.HALI KAMA HII HATUIITI ZIARA, ILA NI MAUDHI.
4. Tuseme ziara ni za lazima – mbona hatuoni report rasmi ya kazi. Mbona hakuna utatuzi wa matatizo ya wananchi kwa hayo yanayokwenda kutatuliwa? zaidi matatizo yanakuwa mengi tu.
5.Imekuwa tena viongozi wote wa SMZ-GNU, wanakwenda pemba kuangalia matofali ya kuchonga Vitongoji na kupiga marufuku. Lakini hawatoi alternative vipi wananchi wa kipato cha chini wafanye ili wasiumie sana na makali ya maisha. Wale wakuja/wageni wa Pwanimchangi watamilikishwa eneo, hawa jamaa wa vitongoji, hapana – WAONDOKE TU. so long hawa ni ‘wapemba’ au ‘watumbatu’ – wakaidi….na watakiona mwaka huu!
Mnajua kuwa kuna mzozo mkubwa katika kisiwa cha Fundo. Hao wanaojiita wawekezaji, wamegawa mipaka ya kisiwa: wamesema mpaka huu wenu wanavijiji; huku kwetu (no flying zone). Kumezuka mtafaruk kuliko ule wa Pwani mchangani. Yafuatilieni, na mtayajua. Na kama kuna mtu anajua zaidi, pia atujulishe. zaidi na zaidi. Seif Ali Iddi alikuwa huko juzi, hakutatua tatizo hata moja linalohusu ardhi, usanii tu.

No comments:

Post a Comment