Tuesday, May 31, 2011

KIKWETE NA SHEIN WANATAKA KUUPITISHA MSWADA WA KATIBA MPYA-MAFUTA ILI WAIMEZE ZANZIBAR

tukiwachia wabara waichukuwa nchi yetu ya znz na kuitumiliya kama kipato chao sawa na sisi hatuna kazi wala bazi mpaka vijana wote wamevamiya unga na bangi kwa hali ngumu ya maisha.
kitu hicho kinasubiri mafuta. je nani asiyetaka nchi yake kuwa na maisha mazuri..?
ona meli za kuja kununuwa mafuta hizo hapo znz ikiwa hatuto kubali mswada na muungano feki haya ndio
tutakayo yakabili siku za mbele tukiwa na mafuta zanzibar laa tukikubali mswada na muungano tutaishia kuona tu haya ila pesa hatutazishuhudia jiulize T.R.A. wanakusanya kodi za wazenji zote zimekwenda wapi..? ndio kweli ikiwa mafuta yako hawa jamaa wa bara kweli watatuambiya tushauza mafuta hizi pesa zenu..?MAWEEEEEE
ikiwa mafuta yatapatikana zanzibar hizi ndio mali zitakazo kuja kununuwa mafuta zanzibar.
ona mambo haya unafikiri mzenji ataruhusiwa hata kukaribia tukisha ukubali mswada tu
basi tumekwisha maana ndio watajazana hapa kila kazi itafanywa na wao je sisi hatutaki kazi..?
 
Huu ndio uchibwaji wa petrol ambao unawatowa roho watanganyika wanataka kuwa lakini petrol ya zanzibar iwe yao na sasa kikwete na shein wanazungumza chini kwa chini kupitisha mswada wa katiba
maana katibu tuliyokuwa nayo sasa hawawezi kuchukuwa petrol ya watu wa zanzibar wazenji amkeni.

Pamoja na kuwa usiri umezidi kutawala katika mpango wa kutengeneza katiba mpya ifikapo 2014, timu ya Kikwete zinazuru sana Zanzibar na kuonana na viongozi wa SMZ (zaidi upande wa CCM) na kushawishi kuundwa haraka kwa katiba mpya.
Kwa habari tulizopata ni kuwa suala hilo sasa wamekubaliana liondoshwe kwa wananchi, na sasa cabinet ministers wa Zanzibar, ndio wataamua, na kupeleka mapendekezo yao serikalini – then, bungeni, kama ndio msimamo au uamuzi wa Zanzibar.
Jamani, tusifanye maskhara. Jamaa hawa wametukalia kooni. Hawatuachi. Kinachotakiwa ni MAFUTA ya ZANZIBAR tu, na sio ‘katiba mpya’.
Unajua katiba ya sasa ni vague (haina mashiko ya kisheria) juu ya suala la mafuta. Linaelea kisheria, si la Muungano wala Zanzibar. Wanalazimisha tu kuwa ni la Muungano. Ila Katiba mpya itapotengenezwa, hapo litakuwa la Muungano kihalali kabisa.
Katiba ya sasa – inaipa nafasi kubwa zaidi Zanzibar kuukataa Mungano kisheria; kulidai suala la mafuta kama lao (Zanzibar) kisheria zaidi. Kwa sababu Muungano hauko kisheria/kihalali. Mafuta yameingizwa kinyemela tu, kiwizi-wizi tu. Kwa sasa hivi, Zanzibar ina position nzuri ya kudai haki zake zote ndanbi Muungano. Lakini ikifanywa katiba mpya, tumekwisha. Mungano utahalalishwa zaidi, na rasilimali zote, zitakuwa zao.
Cabinet ya Zanzibar, kwa tulivyosikia, watakaa rasmi, baada ya kikao cha bajeti — Bunge na BLW. Hapo ndio utaanza mchakato wa kupata katiba mpya. Na Cabinet ya Zanzibar itaridhia suala hilo, kwa mantiki kuwa ‘mawaziir wote ni wamechaguliwa na wananchi wao/waiga kura…ni wajumbe wa BLW. Hiyo ndio logic yao. Kisheria, sio hivyo. Suala la Katiba ni la wananchi. sio la CCM wala CUF wala GNU au Kikwete na Shein. Na Kwa Zanzibar ni nyeti zaidi — ni suala linalogusa utaifa wa wananchi wa Zanzibar.
Jamani tuwe smart — tuikatae katiba mpya kwa hali yeyote ile na muungano pia tuukatae kwa hali yoyote ile. JK anataka sifa, analazimisha by 2014, katiba mpya iwe tayari. TUIKATAE, TUIPINGE NA TULAUMU HATA KAMA WATANUNA.
Tusikubali kufanyiwa kiini macho na JK wala Shein. Otherwise, tutaikosa nchi yetu ya ZANZIBAR.
J.KIKWETE NA KATIBA YAKE FEKI KAMA
MUUNGANO FEKI WA NYERERE JAMAA
YANAJIRUDIYA MAMBO HAYA AMKENI
katiba

No comments:

Post a Comment