Tuesday, May 17, 2011

MAJI NA CHAKULA NDIO MSINGI WA MWANADAMU AU VIONGOZI WA ZANZIBAR HAMUJUWI..? ILA MIDOMO YENU NA MATUMBO YENU YANAJUWA SIO..?

vyakula vimeja znz ila havinunuliki kwa bei kuja juu sasa vipo vipo tu kama maduka ya vioo
 
pweza na kombe pia utapata zanzibar
pweza ila pesa wananchi wa znz hawana wanawangaliya tu
viteoweyo vimeja ila pesa ziko wapi zanzibar...?
hivi ni kweli wake wa mawaziri na wabunge bado wanapikiya mawe matuta kama hawa wananchi kama laa kwanini mpaka leo wananchi wanaowachaguwa nyinyi munawapikisha kwenye mawe matatu....?
umeme unakatwakatwa kila siku ili wapewa mawaziri na wabunge kwenye nyumba zao wapikiye majiko ya umeme lakini wananchi waliyo piga kura ya kukuchanguwa wewe mbunge wa znz na muwakilishi wa znz na raisi wa znz unamuwacha anaendeleya kupikiya kuni huu kweli ni utu huu..?
 
je wabunge na wawakilishi munawaza kuja kula mahali kama hapa kama laa mbona bado munawathalilisha wananchi mpaka wanafikia kula hali popote au huyu kijana anaye pika kwanini asijengewe mahali safi akauza chakula ili watu wa znz wasifikwe na maradhi.
wabunge nyumba zenu na wawakilishi nyumba zenu zina makuta makubwa na mataa na maswiming pool sio vibaya maana nyinyi ni viongozi lakini mbona wananchi wenu wanaishi hivi je ungelikuwa wewe unaishi humu na kuna muwakilishi kama wewe na mbunge kama anaishi maisha unayoishi wewe sasa na wewe ndio umo humu je ungelikubali kweli..?
benzi ndio gari ya raisi nasikiya ujerumani ni tax tu si lolote si chochote pia wabunge na wawakilishi munapanda maprado tu je mbona wananchi wenu bado wanasafiri na magari ambayo sasa ulaya ni kama makumbusho tu au ndio munaona raha kuwathalilisha..?
maji na umeme nikitu kinawasumbuwa sana wananchi wa znz ila sijaona hata siku moja mke wa waziri au mbunge akichota maji kwa ndoo vipi wake wa rai wenu muwaadhibu kiasi hichi ingelikuwa ni mkeo ungelikubali wewe mbunge na muwakilishi mkeo au mtoto wako anabeba maji kwa kichwaa..?
nyinyi maraisi sijuwi na wabunge na wawakilishi wa zanzibar endeleeni kuwanyanyasa wananchi na kuwakandamiza na kuwathulumu maana munakusanya makodi makubwamakubwa lakini nchi imerudi nyuma na ilivyokuwa na nyinyi endeleeni kujijengeya majumba na makasri makubwa makubwa na maji na maumeme ambayo hata hamulipi kisha deni munawasingiziya masikini wamungu wakikata kulipa munawakatiya maji na umeme pia endeleeni kuiba na kuza kila kilicho cha serekali ya watu wa zanzibar na kuwawaka wao katika hali ya unyonge na umasikini wanunuliyeni wake zenu mathahabu ya kila aina na peya za viatu na wasomesheni watoto wenu njee na kuwanunuliya kila kitu cha fahari wanachukitaka katika pesa za wanyonge ila mukishamaliza yote hayo kumbukeni ubathirifu wenu muliyo ufanya hapa duniani na kujijengeya majumba makubwa na magari ya kifahari mwisho wenu na wetu sisi wanyonge ni kwenye nyumba hii ambayo allah hajuwi waziri wala masikini wabunge wala mafukara raisi wala mayatima sote tutaingia huu ndio nyumba ya allah aliyotuchanguliya na kuonyesha kuwa sote sisi ni sawa hakuna cha waziri wala mbunge wala raisi.
 
 
bora pesa zako ila kila kitu duka hili kinauzwa bila ya wasi wasi kabisa

No comments:

Post a Comment