Tuesday, May 24, 2011

NCHI YA ZANZIBAR SIO MASIKINI ILA VIONGOZI WAMEWADANGANYA WANANCHI MPAKA SASA WANANCHI WANAMINI KUWA NCHI YAO YA ZANZIBAR NI MASIKINI.

zanzibar hatukuwa tuki ishi hivi hata hapo tulipokuwa tukitawaliwa na mgereza na mfalme ila sasa
ndio tunaishi kama hivi ndio maendeleyo ya miaka 47 ya muungano....?
KUNA UBAYA GANI KWA KILA MZENJI KUISHI KTK NYUMBA KAMA
HII...? KWA NINI MPAKA LEO WATU ZNZ WANAISHI KATIKA VIBANDA
KAMA KUKU NA MAWAZIRI NA WABUNGE NA MARAISI WASTAFUU WANA
MAJUMBA KULIKO HII 5 AU 10 KWA NINI..?
HII NDIO STREET ....?
TUTAISHI HIVI MPAKA KIYAMA AU NI SISI RAI TUDAI
HAKI YETU ILI MAWAZIRI NA WABUNGE NA MARAISI
WASITUFANYE MAJUHA YAO YANAWAENDEYA SISI
BADO TUNALIYA NA NJAA KILA KUKICHAA.

JE KUNA UBAYA GANI ZNZ YETU NCHI YETU YENYE WATU MILLION 1.5 RAI,DUNGU,
FAMILIYA ZETU KUISHI KAMA HIVI KUNAUBAYA NGANI ...?
NANI ASIYETAKA KUWA NA CHOO KAMA HICHI ZNZ HASWA WAKAZI WA MAKUNDUCHI,MWERA,UROWA,MKWAJUNI,DONGE,TUMBATU NANI ASIYETAKA AU VYOO KAMA HIVI NI VYA MARAISI TU NA WABUNGE NA WAWAKILISHI NA FAMILIYA ZAO...?
ni nani na nani mwanamke ambaye yuko hapa unguja na pemba  asiyetaka kuwa na jiko kama hili..? au ni wake wa
raisi waliyo stafuu na mawaziri na wabunge ndio peke yao wenye haki znz yakuwa na jiko kama hili..?

ZANZIBAR inayoundwa na visiwa viwili vikubwa vya Unguja na Pemba, pamoja na ni visiwa vingi vidogo vidogo ni maarufu kihistoria ulimwenguni na ilikuwa ikitajika kwa uchumi mzuri, ambapo sasa imekuwa ikitajwa kuwa moja ya nchi masikini duniani.
Katika utafiti niliofanya kuhusiana na ukweli wa Zanzibar kuwa masikini au la, nimefikia hatima kwamba kamwe nchi hii si masikini kama inavyotangazwa, lakini kuna mambo yanayofanyika na kutoa fursa ionekane masikini na hata kufikia viongozi kudanganyika kuwa kweli umasikini upo Zanzibar.
Katika waraka wa Chowea leo, nitagusia eneo moja tu la fedha kudhihirisha kuwa Zanzibar si masikini na kama kuna umasikini basi ni wa kutengenezwa, wataalamu wa uchumi na fedha waliopo Zanzibar kama hawaelewi hilo, nitakuwa na shaka na utaalamu wao au nitachukulia kuwa hawataki kusema ukweli kuhusiana na suala hili.
Katika dunia ya leo fedha ni nyenzo muhimu ya maendeleo kutokana na mfumo wa uchumi wa dunia ambao umeungana kupitia mfumo wa utandawazi, ambao dunia nzima inategemeana kiuchumi, ikiripuka Japan, Zanzibar inaathirika, uharamia ukifanyika Somalia, Zanzibar itaonja athari, mafuta yakipanda bei Oman, Zanzibar nayo imo kuumia, sikwambii vita vikishamiri Libya na Nchi nyengine za Afrika kwetu nako twaumia.
Zanzibar ni nchi yenye maumbile ya visiwa ina vianzio mbali mbali vya mapato ambapo nitazungumzia vichache na kuonesha vipi vingesimamiwa vyema na kupunguzwa mianya ya kuvujisha mapato na rushwa, vingeweza kudhihirisha kuwa Zanzibar si masikini.
Ikikadiriwa kuwa na watu karibu milioni 1.5, Zanzibar kwa kujipanga vyema na kusimamia kwa umakini sekta za mapato, inaweza kuwaadhiri wote wanaolazimisha ionekane kuwa nchi masikini.
Nianze na chombo kikuu cha ukusanyaji mapato Zanzibar, Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), ambayo mwezi Februari mwaka huu ilitangaza kuvunja rekodi ya makusanyo tokea kuanzishwa kwake mwaka 1998 kwa kukusanya Shilingi bilioni 10.37, sawa na asilimia 107 ya makadirio yaliyokuwa Shilingi bilioni 9.65.
Nalazimika kuipongeza ZRB kwa hatua hiyo ambayo inaonesha mwanzo mwema, ukizingatia kuwa utafiti wangu unaonesha hiyo ni angalau ya nusu ya kile am,bacho kingekusanywa na Bodi hiyo kila mwezi kwa kipindi kirefu sasa.
Aidha ni faraja kusikia kuwa ongezeko hilo limechangiwa pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa mapato ya Mawizara ya Serikali kufikia Shilingi bilioni 1.3 ni hatua japokuwa bado ni kidogo mno tukiangalia uhalisia wa uwezekano wa mapato ya mawizara hayo.
Upande mwengine ulioelezwa kuongeza mapato hayo ni vianzio vya sekta ya utalii, kwa vile idadi ya watalii imeongezeka, jambo ambalo kila mmoja wetu amelitarajia lakini kwa kiwango kikubwa zaidi ya kilichopatikana.
Kwa bahati mbaya tumeishia kupata taarifa za mwezi huo wa Februari, ambapo ingekuwa vyema wananchi wakaeleweshwa mwenendo kila mwezi, ili wapate kupima hali inavyokwenda.
Kwa ukimya huo hivi sasa kutakuwa na mawazo ya kutungatunga na ya redio vifua kuhusiana na ukimya huo, wako wataosema inaonesha yameshuka ndio maana ZRB ikaona haya kutangaza na wengine kuweza kuhoji iwapo hayatopanda mwezi Aprili, ambapo Zanzibar ilikuwa mwenyeji wa tamasha la michezo la Pasaka na kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wakati huo nyumba za wageni zilifurika, mikahawa ikauza chakula kingi na abiria kwenye magari, boti na kwenye ndege waliongezeka zaidi ya maradufu, biashara ndogo ndogo nazo zikaongeza kipato alhamdulilahi, tabaan mapato yawe yameongezeka si vinginevyo.
Niliposema kilichokusanywa na ZRB kinachoelezwa kuwa ni kuvuka lengo ni nusu tu ya ambacho kingekusanywa, kutokana na sababu anuai ikiwemo kufanyika kwa makadirio kimazoea ya chini (under estimate) ambayo si halisia, pengine kwa kuendelea kufanya kazi kimazoea au wahusika kuogopa kuwajibika kwa kushindwa kufikia kiwango cha makadirio watayoweka.
Chengine kilicho wazi ni kutozingatiwa kwa mabadiliko ya thamani ya dola, ambayo ukiitizama unaweza kugundua kilichokusanywa hakikufika hata lile lengo la awali la shilingi bilioni 9.65 na ongezeko hapo likawa ni kupanda kwa thamani ya dola, wataalamu hawa wa ZRB hili wanalielewa fika.
Mapato haya pia yamepungua kwa kuendelea kuwepo mianya mingi ya uvujaji mapato yakiwemo ya fedha za nyumbani na za kigeni, kupitia udhibiti dhaifu wa mfumo wa utolewaji risiti, kumbukumbu za uongo ziwekwazo na wafanyabiashara wakiwemo wenye mahoteli ambao wana madaftari mawili ikiwemo la kulipia kodi na usajili halisi wa wageni, hili nalo si jipya na maafisa wa ZRB wanalielewa na inaonekana limewashinda hali leo kuliondosha moja kwa moja.
Taarifa za wageni wanaoingia uwanja wa ndege zinatafautiana kati ya wakusanyaji mapato na uhamiaji, hali inayoonesha ujanja na udokozi wa mapato, jambo ambalo linahitaji pia kufanyiwa kazi.
Bado kuna minada mingi isiyo rasmi inayofanyika kila Pembe ya Unguja na Pemba, ambayo kikawaida ilitakiwa kulipa kodi lakini ukweli ni kwamba Serikali haiambulii hata peni.
Nyumba za kulala wageni ‘gest house’ bubu nazo zimeenea na zinafanya biashara kwa murua bila kuwepo wa kuzihoji ulipaji kodi wao, hali kama hiyo pia ikiwa kwa teksi bubu, huku wenye kufanya kazi hizo kirasmi wakibinywa.
Kianzio chengine cha mapato Zanzibar ni asilimia 4.5 ya pato linalopatikana kupitia serikali ya muungano, ambacho kikisimamiwa vyema na kupatikana kitaratibu kinaweza kuvimbisha mfuko wa Zanzibar kifedha, hivyo wakati umefika wa taasisi husika kuwa makini ‘serious’.
Kwa vile mapato yakusanywayo Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yanabakia Zanzibar kama vile VAT, PAYE, eneo hili nalo moja kwa moja linaingia kwenye vianzio vya mapato vya Zanzibar, hivyo linahitaji kusimamiwa vyema na kuangaliwa kwa umakini, badala ya mtindo wa sasa wa kuridhika na kinachopatikana, huku mabilioni yakikosekana kutokana na sababu mbali mbali.
Kwa upande wa TRA hapa ndio Zanzibar hufanyiwa kiini macho na fedha nyingi kukosekana, kwani fedha zinazokusanywa ni sehemu tu hubakia Zanzibar kikweli kweli na nyengine huvushwa hadi Tanzania Bara kupitia njia mbali mbali za kijanja na zinazojulikana, lakini wanaonewa haya kuambiwa.
Ni kujikosesha mapato kuliko wazi kupitia TRA kwa Zanzibar kumezea baadhi ya kodi ambazo ni stahili yao kutobakishwa Zanzibar kama vile kodi za mishahara za wafanyakazi wa taasisi za Serikali ya Muungano waliopo Zanzibar ambao hutumia huduma zote Zanzibar, ikiwemo, Mawizara, Mabenki, Viwanda na vyombo vya dola.
Aidha mamilioni ya kodi zote zinazolipwa na wananchi wa Zanzibar kwa siku kupitia matumizi ya simu za mkononi kwa makampuni ya simu zilizosajiliwa Tanzania bara, nazo hazibakii Zanzibar, ambapo utaona wazi kuwa umasikini unaosemwa Zanzibar ni wa kutekelezwa.
Ni juzi tu tulisikia uongozi wa TRA ukijisifu kuwa umekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 61 katika kipindi hichi cha mwaka wa fedha 2010/2011, ambacho ni sawa na asilimia 88.7 na kujigamba itafikia 100% mwezi ujao.
Naomba kueleza kuwa hiyo inamaanisha TRA Zanzibar inakusanya wastani wa shilingi bilioni 5 kwa mwezi, jambo ambalo tabaan wasomaji wote mtakubaliana nami ni masihara hata kutangaza hadharani.
Kwa taasisi kama hii kushindwa na ZRB kwanza si sahihi na pia inaonekana viashiria vyote nilivyovieleza kuwa kinakusanywa kingi na kubakishwa Zanzibar kichache ni za ukweli na kamwe kwa namna hii chombo hichi hakiisaidii Zanzibar na malengo ya kuwepo kwake visiwani yanakosa mashiko.
Aidha TRA upande wa Zanzibar nayo ingeweza kukusanya zaidi kwa maslahi ya Zanzibar, lakini kasoro zote nilizoainisha kuikwaza ZRB pia zinaiathiri Mamlaka hii na zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Watendaji wa masuala ya kodi waache kuwa wanasiasa au wakilazimika kuwa wanasiasa basi wasimame na filisofi isemayo ‘siasa ni uchumi’, hivyo kusimama kidete bila kuona haya, aibu wala woga kupatikana kodi hizo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya Saba iliyo katika mfumo wa umoja wa kitaifa, inatumainiwa sana kimaendeleo na wananchi wa Zanzibar na yenyewe imeahidi kuyafikia matumaini hayo, ambapo mengi yake yanategemea zaidi pato la serikali.
Kuziimarisha huduma za kijamii kama vile elimu, afya, maji safi na salama, miundombinu bora ya kujenga mazingira ya kuongeza pato la wananchi na kuwaondosha katika dimbwi la umasikini kunahitajika fedha.
Zanzibar fedha zipo na njia bora za kukusanya fedha hizo zinafahamika, kinachokosekana ni uwajibikaji na uwajibishwaji, umakini zaidi, pamoja na uzalendo kwa watendaji.
Wananchi wa kawaida ambao ni wanyonge na masikini kwamwe hawakwepi kulipa kodi kutokana na kuwekwa utaratibu mzuri wa kuwalazimisha kuwajibika kama raia, kupitia mikato ya mishahara kwa walioajiriwa, pamoja na matumizi yao ya bidhaa mbali mbali.
Kibaya ni kuwa hapa kwetu m,atajiri na wenye vyeo na mamlaka ndiyo wakwepa kodi, kutokana na kupata misamaha ya mambo mbali mbali na wafanyabiashara kuwa na mbinu za kukwepa kodi kupitia rushwa, umaarufu, jambo ambalo ni kinyumenyume katika zile nchi tunazozisifia na kuziita tajiri, ambako mwenye kupata kingi ndio mlipa kingi.
Kwetu kuna kundi zima la mhimili wan chi ambalo ni la wanasiasa ati wao hawalipwi kodi mbali mbali, wakati ndio wenye kupokea mishahara ya juu zaidi nchini, halafu tuseme Zanzibar ni masikini kama hatuifanyi sisi kuwa hivyo.
Wakati masikio na matarajio ya wananchi wa Zanzibar kwa uongozi wa awamu ya saba yakisubiri kuanza kwa bajeti mpya ya 2011/2011, taasisi za uchumi na ukusanyakaji mapato ni lazima zijiimarishe ili kuiwezesha serikali kufikia malengo yake na kufikia matarajia ya wananchi.
Kwa vile suala la kuongezwa mishahara ni moja ya mambo ambayo hayawezi kuepukika katika mwaka wa fedha ujao, mapato zaidi yatajitajika kutokana na kuongezeka wenye vyeo vikubwa na vilio kwa watendaji wa ngazi za chini, pamoja na mikakati ya kuhakikisha wataalamu hawakimbii nchini kufuata mishahara minono nje.
Tunaokumbuka bajeti ya mwaka wa fedha unaomalizika wa 2010/2011, ilikuwa ni shilingi bilioni 444.637, ambapo shilingi bilioni 251.204 zilipangwa kwa kazi za maendeleo na shilingi bilioni 193.433 zilipangwa kwa matumizi ya kazi za kawaida, ambazo tabaan mwaka huu zinahitaji karibu mara tatu yake.
Inatia moyo kusikia washirika wa maendeleo nao mwaka huu wameongeza mchango wao wa misaada ya kibajeti kwa Tanzania (GBS), ambapo bila shaka Zanzibar ikiwa sehemu ya Tanzania nayo itapanda fungu kubwa zaidi litalochangia kuinua bajeti hiyo ya 2011/2012.
Hiyo ni habari njema lakini zinapaswa kufuatiliwa kwa haraka ili zifanyiwe taratibu kwenye upangaji wa bajeti ya Zanzibar ambayo naamini mchakati wake umefika mbali, kabla ya kuja taarifa hizi.
Si vibaya kwa Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kupanga hesabu zake na kuchukua sehemu ya GBS kuziongezea ‘ceiling’ taasisi za Serikali, badala ya mtindo wa zamani wa kuliweka fungu lote hili kwenye mfuko mkuu wa Serikali, kila linapochelewea kufika nchini.
Hapa kwenye GBS mwaka huu kunatakiwa umakini zaidi kwa Zanzibar, ikizingatia kuwa baadhi ya nchi kama vile Switzerland na Uholanzi, hazikuingiza mchango wake moja kwa moja kwenye mabilioni hayo ya GBS na badala yake itasaidia kupitia miradi itayofadhiliwa na nchi hizo nchini.
Kama hivyo ndivyo kuna umuhimu wa Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kupitia Idara yake ya Fedha za Nje iziarifu sekta husika na miradi itayofadhiliwa na mataifa hayo, ili kujiandaa kutumia msaada huo na kama haipo basi taasisi za Zanzibar zikiwemo za Serikali na watu binafsi zipewe taarifa kuandaa maombi ya miradi kupitia ufadhili ya uholanzi na au Swiss, ili kutumia fursa ya fedha hizo za bure.
Itakuwa hasara kubwa kwa Zanzibar kukaa kimya kusubiri ndugu zao wa Tanzania Bara kuwakumbusha ilhali wamesikia wenyewe au kukaa kusubiri itolewe kwa upande wa bara halafu tuanze kulaumu na kupiga kelele kuwa tumetengwa au kuonewa, katika dunia ya sasa kila mmoja hulia ‘mamaangu’.
Eneo jengine ambalo ni muhimu kuthibitisha kuwa Zanzibar inaweza si masikini ni matumzi ya fedha za mifuko ya mamilioni ya AK na JK, ambayo lengo lake ni kuinua hali za maisha ya wananchi kwa kuwapa mikopo ili waweze kuendesha ujasiriamali kwa kujiajiri na hatimae kutokomeza dhana ya umasikini nchini.
Hadi sasa wakati mfuko mwengine wa Rais wa awamu ya Saba wa Zanzibar wa mamilioni ya Dk.Shein ukiandaliwa kama ilivyobainishwa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman, bado haieleweki yalikokwenda mabilioni ya Kikwete na Karume, ambayo ukopeshwaji wake ulikumbana na vikwazo lukuki na kushindwa kuwafikia wananchi.
Kabla ya kurukia mfuko mabilioni ya AS, kuna haja ya kufanyika tathmini ya mfuko wa AK na JK, halafu kuzigawa fedha hizo kwa kuanzia vyenginevyo itakuwa tunafurahisha masikio kwa kutangaza kuwepo mabilioni yasiyotumika ilivyokusudiwa.
Kwa jitihada, umoja, umakini na uzalendo kamwe Zanzibar haiwezi kuwa miongoni mwa nchi masikini.
 

No comments:

Post a Comment