Tuesday, May 17, 2011

OMAN AIR YAANZA SAFARI ZAKE ZANZIBAR

 NDEGE ya Shirika la Oman Air ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar  ikitokea Oman ikiaza safari zake Nchini leo.   
 ABIRIA wa kutoka Oman wakiteremka katika Ndege ya Oman Air baada ya kuwasili Zanzibar leo saa 12.15 Asubuhi ikitokea Nchini Oman.

 WAZIRI wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Hamad Masoud akisalimiana na baadhi ya abiria waliowasili Zanzibar wakitokea Nchini Oman baada ya Shirika hilo kuaza Safari zake hapa Zanzibar
 WAZIRI wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Hamad Masoud  akisalimiana na Rubani wa Ndege ya Oman Air Mehdi Hamoud  Al- Said, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  Abeid Amani Karume Zanzibar, ikitokea Oman ikiwa ni safari yake ya kwanza leo na zitakuwa safari nyingi baada ya hii kati ya zanzibar na Oman.    
 ABIRIA wa Oman Air wakitowa Majengo ya Uwanja wa Ndege Zanzibar baada ya kuwasili leo Asubuhi saa 12.15, wakitokea Oman.


 BAADHI ya Abiria wa zanzibar wakijiandaa kupandaa Ndege kuanza Safari yao Nchini Oman, baada ya Shirika la Ndege la Oman Air kuaza safari zake Zanzibar leo ikitokea Oman moja kwa moja.   
 ABIRIA  wkipanda katika Ndege  baada ya Oman Air kuaza Safari zake Zanzibar leo ikitokea Nchini Oman. 
 NDEGE ya Shirika la Ndege la Oman Air ikiaza Safari yake Kurudi Nchini Oman  baada ya kushusha abiria wa Zanzibar baada ya kuwasili Uwanja wa Zanzibar ikiaza Safari zake kati  Zanzibar na Oman
 BALOZI wa Mdogo wa Oman  Zanzibar Shekh. Majid Ahmeid Al- Laaban akihutubia wakati wa Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Oman Air ikiwa ni sherehe za Uzinduzi wa Shirika hilo kuaza Safari zake kati ya nchi ya zanzibar na Oman. 

No comments:

Post a Comment