Monday, May 9, 2011

SEIF ASEMA UGUMU W MAISHA ZANZIBAR. AWASINGIZIYA MAHARAMIYA WA KISOMALI DUUUH AMAKWELI SIKU YA KUFA NYANI MITI HUTELEZA

Maalim Seif
Salma Said, Zanzibar
MAKAMU wa Rais wa Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amejibu malalamiko mbalimbali ya wananchi dhidi yake, viongozi na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuhusu kupanda kwa maisha na kutokuwapo kwa serikali ya kitaifa ngazi za chini.
Akihutubia Mkutano Mkuu wa CUF Wilaya ya Mjini jana, Maalim Seif baadhi ya wabunge na wawakilishi wa CUF hawaonekani kwenye majimbo yao tangu walipochaguliwa mwaka jana.
“Nimesikia malalamiko kwamba sionekani na kwamba, viongozi tumekaa kimya kuhusu operesheni ya Darajani ambako wafanyabishara waliondolewa. Nafikiri ni vuzuri nyie viongozi mkafanya utafiti kabla ya kutulaumu,” alisema Maalim Seif.
Katika kujibu malalamiko hayo, Maalim Seif alisema aliahidi kupunguza bei ya bidhaa hasa chakula iwapo angechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.“Mimi siyo rais, ni makamu na mshauri tu wa rais. Hata hivyo, sisi viongozi tunafanya kazi ili kuleta unafuu kwa wananchi,” alisema.
Kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa, Maalim Seif alisema siyo Zanzibar pekee, bali nchi mbalimbali hali ya maisha inazidi kuwa ngumu na kwamba, limesababishwa na kupungua kwa uzalishaji duniani na uharamia wa Wasomali.
Maalim Seif alitaja baadhi ya mikakati ya kupambana na hali ngumu ya maisha kuwa, ni kushawishi wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza Zanzibar, kuimarisha kilimo hasa cha mpunga wa umwagiliaji.
Pia, Maalim Seif alisema miongoni mwa mambo mazuri ambayo Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaadaa, ni kuzingatia suala la kubinafsisha soko la Karafuu ili wakulima wawe huru kuuza wanapotaka.Kuhusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema katiba imeelekeza kuwa mgawanyo wa nafasi ni ngazi ya mawaziri na naibu mawaziri.
“Nafasi nyengine zote zipo chini ya rais kwa mujibu wa katiba. GNU katika kugawana nafasi imeishia juu tu na ndivyo katiba inavyosema,” alisema.
Alisema amepunguza kazi na amekuwa haonekani hadharani kwa sababu bado anaumwa, huku akiwataka viongozi wengine wakiwamo wabunge na wawakilishi kuimarisha chama na kuwatumikia wananchi.
“Nasikitika, ni kweli viongozi tumelala, sioni harakati ndani ya chama. Vijana na wanawake mmekaa kimya, afadhali ya wanawake. Lazima kazi ya kuimarisha chama iendelee ngazi zote,” alisema.
Alisema baadhi ya wabunge na wawakilishi wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika majimbo yao, lakini amewaonya ambao bado hawajaonyesha juhudi za kuwatumikia wananchi na kwamba, atawabana wamweleze walichofanya



JIBABA 09/05/2011 kwa 7:04 mu · Jibu
Maalimu seif pole sana na Mungu akuafu. Sasa tunachotaka wazenji wekeni bandari huru Zenji hata muone kuwa maisha hayatakuwa rahisi lakini sisi hatujui mpaka leo nikipi hasa munachohofia kufanya hivyo. au kwa sababu kwenu maisha si magumu,cha kushangaza eti maisha yamepanda hivi ni kwa wazanzibari tu mbona Tanganyika mabo yao si mabaya licha ya kuwa kuna mamilioni ya watu, Na ikiwa wewe una ushauri mzuri kwa rasi wako juu ya kuiletea maendeleo Zanzibar kwa nini hujiengui ukawaachia Serikali yao bado tuu unang’ngania au ndiyo na wewe kushapwewa fupa unabebenya huna habari tena na sisi




  • DUUUUUUH YU NDIYE SEIF AU…….. ATI ANSEMA KUWA WAHARAMIYA WA SOMALIA NDIYO WALIYOFANYA ZNZ IWE NA HALI GUMU HATA HAYAINGI AKILINI KABISA PIA ANASEMA MIMI SIO RAISI SASA KUJA TUKUPE MSEMO WA KISWAHILI USEMAO DALILI ZA MVUA NI MAWINGU WEWE SASA SIO RAI NA HUJUWI TENA UFANYE NINI JE UKIWA RAIS SIUTATUMALIZA KABISA?
    SEIF WEWE UMEKWENDA NCHI NYINGI SANA NA UMEONA VIONGOZI WENGI SANA JE HAYO MAJIMBO YAO ULIVYOKUWA UKIPITAPITA ULIYAONAJE? NA SASA HAO WABUNGE WA CUF NA MAJIMBO YAO WALIYO SHINDA KUMEBADILIKA NINI? SEIF WAZANZIBAR WASHAMKAA NA KAMA WEWE HUJAA AMKAA UTAJIKUTA PABAYA.
    UNASEMA WEWE NI MAKAMO TU NA KAZI YAKO NI USHAURI JE KILA UNAVYO MSHAURI HUYO SHEIN ANAKATA SIO?……KAMA NDIO HIVYO BASI WEWE USIOGOPE KUTANGAZA SEMA KWELI UNAMBIWA MSEMAKWELI KIPENZI CHA MUNGU SIMAMA NA UWAMBIYE WATU WA ZNZ JAMAA KILA NINAVYO MSHAURI SHEIN YEYE HATAKI SASA MIMI SITAKI MIAKA MITANO ISHE NA HAKUNA MOJA LILILOKUWA NAJIVUWA BASI UTAONA WATU WATAKAVYO MFANYA HUYU SHEIN KAMA NDIO CHENI SIJUWI TUTAIKATAKATA MAANA TUSHACHOKA.
    LAKINI UKISEMA MIMI NIMSHAURI TU NA KAMA MUNATAKA MIMI NIFANYE JAMBO BASI NICHANGUENE MIMI WAPI BORA UKALALE USHAKWENDA MPAKA ULAYA KARIBU NCHI ZOTE JE SHEHA TU WA ULAYA AKIDHULUMIWA JIMBO LAKE KUWA HALIKUPEWA HAKI ANAWASHA MOTO MPAKA APEWE HAKI YA JIMBO LAKE SASA MBONA WEWE MAKAMO MZIMA WA RAIS UNATULETEYA LUGHA ZA KIHAFIDHINA HAPA KAMA HUNA TENA LA KUSEMA AU LA KUPINGANIYA ZNZ BASI BORA UJILIYE HILO FUPA LAKO KAMA ALIVYOSEMA MWENZANGU HAPO JUU KULIKO KUSEMA MANENO YASIYOKUWA NA MSINGI WALA FAIDA
    WAZANZIBAR HATUNAHAJA YA SEIF WALA MASHEIN WALA IDDI ZNZ NI YAWAZANZIBAR KWA HIYO SISI WENYEWE NDIYO TUTAIKOMBOWA HAWA WOTE NI WAHAFIDHINA WA TANGANYIKA WASHAPEWA PRADO NA FFU WAKUWALINDA BASI WANAONA NDIO MAISHA WAMESAHAU WANCHI WANAKUFA NA NJAA NA HAWANAPAKUISHI NA MAJI HAKUNA TAA HAKUNA WAO MBONA NYUMBA ZAO ZINA MAJI NA TAA NA KILA SIKU WANAKULA VIZURI NAMASHAVU YANAWATOKA NA MATUMBU KISHA WANATUAMBIYA SISI MAISHA MAGUMU KWAKUWA KUNA WMAHARAMIYA WA KISOMALI NA WAO HAWA VIONGOZI WA GNU AU SUK NDIO MAHARAMIYA WANAOWANYONYA WANANCHI WA ZANZIBAR MAHARAMIYA NYOTE NYINYI KTK GNU


  • No comments:

    Post a Comment