Thursday, May 26, 2011

ZANZIBAR HAINA HAJA YA UMEME WA TANESCO VIONGOZI WA ZANZIBAR FUNGUWENI MACHO MUNACHEKWA ULIMWENGUNI.


hii ndio Dowans ambayo imelala na mamillioni ya wananchi mpaka leo kimya.

hii ndio tanesco inayowanyanyasa wananchi wa znz kwa umeme na kuiba
mamillioni kwa mamillioni wazenji wanalipa na wala hauwashwi tunagaiwa
kama kokwa za tende moja moja siku wakisha pinga tungi ndio wanauwasha

watu tuna lipa mapesa kibao na huu ndio ufungaji wao
wa umeme kuna tafauti ngani na somalia nchi ambayo ina
vita zaidi ya miaka 24 sasa na umeme wanaufunga vizuri kuliko
hivi ni kamaaaaaaaaaaaaaa hata sijuwi niseme nini nituendele kuibiwa tu znz basi.

hawa ndio wanao tuzimiya na kutuwashia na kutunguziya vitu vyetu.

mwenye nyumba hajuwi kama na yeye ashajitiya msibani wanamungia harahara
ili wanze kumnyowa hizo pesa zake waone hata mavazi yao yanaonyesha kuwa
ni wezi tu sio watu wa umeme.


mafaili mengi simu za mkononi mbili mbili koti na tai kubwa na umeme hauwaki daaaaah.

kila siku kwatengezwa na znz umeme hakuna jamaa bado tu tunawategemeya wakoloni wausi mpaka lini..?




2011 ndio kwanza mawaya yananinginiya mpaka kwenye kuta na mabati bado tu znz hatuwatupili mbali
na kuanzisha wetu wenyewe maana tulikuwa nao umekwenda wapi..?na ni nani aliyesema tuanze kuletewa
kutoka kwa hawa watang..?

aibu gani hii waya hazina umeme mpaka watu wanageuza ndio
kamba nzuri za kuanikiya nguo wazenji amkeni amkeni.


katika harakati za jinsi gani tuwadanganye wananchi ili tuzidi kula au mushashiba.bado bado mzee tunataka zaidi.

TANESCO Managing Director ENG. William    Mhando ona jitumbo lilivyokuwa kubwa mpaka
vifungo vya koti havifungiki kwa kula haramu na jasho la masiki kuwalipisha umeme ambao
hata hauwashwi.

NINA WEKA HIZI PICHA KWA MAKUSUDI MAANA VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR WASHAKUWA KAMA ILIVYOSEMA ((QURAAN SUMUN BUKMUNI UMIYUNI FAAHUM LAAA YAARJIUNI)).
NA KAMA SIO KWELI NINAYO SEMA HEBU ZNZ IWEKEANI UMEME KAMA HUU TUONE KAMA TUTAPATA TABU TENA.

munasafiri kila siku munakwenda nchi za nje sijuwi munakwenda kuficha
hayo mamillioni muliyo iba kama alivyofanya mubarouk,ben ali na gaddafi.
maana huko ulaya kila mahali siku hizi wanajaribu kutumiya windpower
kama hamujuwi basi ndio huu hapa ni umeme ukiweka maguzo matatu unguja
na matatu pemba kwisha fitina ya umeme hatuna haja ya umeme wa tang.

ona ulivyo mzuri green hakuna uchafu znz itazidi kughara lakini najuwa viongozi wa znz
mpaka mume wenu mtanganyika awambiye ndio mufanye kama sio hivo mutanyamaza tu.

nyinyi majuha muliyo jazana baraza la wawakilishi fumbuweni macho ulimwengu usha amka nyinyi bado tu munaona kuwa na prado na nyumba 6 za wizi na viwaja vya wizi na umeme
wa mgao ndio maisha ona mambo haya.

ona kitu hichi nyinyi bado tu TANESCO TANESCO TANESCO mume  kama hamukusoma humo ndani ya baraza la wawakilishi hata sijuwi mulifika vipi na kuwa mawaziri na wabunge ahh nimekubuka munarithishana kama nyumba yenu jaji mkuu hakuondoka mpaka kamuwacha mwanawe kwenye kiti na nyinyi ndio hivyo hivyo ndio znz ikadidimiya.

hebu wekeni haya matatu unguja na matatu pemba tuone kama tutasikia mtu anasema
sina umeme kitu kinatumiya upepo tu na lini znz tulikosa upepo.?

oneni funguweni macho viongozi wa znz ni bahari hii na umeme
unapatikana na sisi unguja na pemba tumezungukwa na bahari
au znz sasa ni ethiopia ndio ambao hawana bahari..?

tumezungukwa na bahari ona mambo haya bado tu munahanithiwa
na watanganyika kwa umeme..?

oneni mambo sio nyinyi munajazana baraza la wawakilishi na hakuna hata moja
mwenye fikra za kutatuwa umeme haya mimi mwananchi nawapa fikra sasa nyinyi
timizeni kama kweli ni viongozi au ni wezi tu mumeka hapo na kuiba basi.

cheki vitu hivyo ni umeme sio tanesco mpaka lini maguzo yanaoza waya
za ninginiya mpaka za uwa watu kwa mgao kama tende cheki vitu hivi shein
na seif na wenzenu nyote humo ndani ya baraza munasinzia tu kama pono.

baraza la wawakilishi amkeni munasinziya sana nyinyi majuha humo ndani kazi kulala tu hamuna nyumba za kulala mpaka mulale baraza la wawakilishi..?bahari hii na umeme pia.
je znz hatuna bahari sisi tuna  mito au maziwa..?

unaona umeme wa windpower kwenye bahari kule na hapa check barabara ilivyotulia je
kwa nini zanzibar isiwe kama hivi..?itakuwa mukiwachakuwibaa mamillioni na kujenga nchi itakuwa hata kuliko hivi ila uroho umewaja na tamaa na mukifa munaviwacha hapa hapa viongozi wangapi walikuwa wakiba na kuwanyanyasa wazenji na sasa wamo makaburini wanaiyona joto ya jiwe na nyinyi endeleni tu.

ona taa za barabarani solar plat mtu

barabara ya kwenda jagombe tuwekeni kama hizi au mwera

mji utapendeza mpaka mashambani pia

kitope mfenesini uruwa pwani mchangani kama hizi tu

hata taa za barabarani pia zina tumiya solar plat hakuna haja ya mawaya

foro kama kawa mzee juwa tu BLW hata hizi pia hamuwezi kununuwa..?

shangani malindi na kiponda mkunazini kilimani kama hizi vichochoroni juwa tu

ona hapa hata india vijijini wamewekewa itakuwa znz jamaa serekalini punguzeni kuiba daaah.

shein na seif oneni mambo haya michezani kunatisha siku hizi kupita

nchi nyengine africa zisha anzaa je sisi tutakuwa
wa mwisho au ndio sio nchi ni mkowa wa pwani..?

hakuna hata sababu moja ya kuwa znz isiwe na taa za barabarani au kwenye vichochoro ona mambo haya.

hata mitaani pia tuwekeni kama hizi hazitaki mafuta ya taa hii ni juwa tu shein na seif.

marikiti pia kunatisha usiku taa kama hizi mchana kutwa zimepingwa na juwa usiku zinawaka tuu

au hivi barabara zote za unguja na pemba ndio kujenga nchi ati.

kwanini barabara zetu zote unguja na pemba zisiwe na taa kama hivi

au hivi kwanini...?

ona india hapa barabara mbovu lakini taa ile pale juu znz tunaweza tukawa zaidi hivi barabara na taa mukiamuwa au ndio tutakuwa kama tunaishi maisha ya 1725 iliyopita.

haya oneni hii ndio solar plat inatumiya juwa na kukupa umeme ndani ya nyumba je viongozi wa znz hakuna juwa pia znz..?

ona mambo haya bado tu munataka kunyanyaswa na tanesco..?

hata muza chips basi yuko powa na gari lake na chumba humohumo na jiko
na hana haja ya umeme wa tanesco vipi nchi nzima ya znz ibembeleze tenesco.?

hakuna mawaya kuninginiya wala maguzo ya oil chafu kujazana na wana umeme
ona juu ya paa ndio solar plat hiyo kama nyinyi viongozi hamujuwi sasa je..?

hata umeme huu pia SMZ AU GNU AU SUKARI pia hamuwezi kuwapa
wananchi..?ni juwa tu basi au znz sasa hakuna juwa kuna mabarafu tu..?

viongozi wa znz munachekwa nchi za nje nyinyi hamujuwi ila munachekwa tena sana
nafikiri hata dungu zetu waliyokuwepo nje sasa washanza kuona aibu kusema wanatoka
znz maana kitu umeme na maji sio kitu kikubwa kabisa ktk miaka hii.

jua tu na watu wanakula umeme mpaka wanachoka znz kunajuwa na joto
kiyama lakini munasema hakuna umeme watali wanawacheka nyote viongozi
wanawaona ikiwa viongozi majuha haya hao rai watakuwa vipi basi.

jua tu shein jua tu seif na umeme unapatikana vipi bado mumelala?

kwa viongozi wetu walivyo na roho mbaya watajinunuliya wao kwanza
na waume waliyo waowa dada zao wawe na umeme kisha 2060 ndio labda
rai wa kawaida tutakuwa nao.

wenzetu huko ulaya nasikia hata hawana juwa kama la hapa na wanaumeme
sisi hapa znz juwa hutoka mpaka watu wakazimiya darajani mpaka atiwe maji ndio
inuke mtu lakini ajabu hakuna umeme viongozi munafanya nini..? mulizo iba haziwatoshi tu.

hii ni nyumba huko ulaya ona hatengemei serekali ana feni lile linazunguka na kumpa umeme ndio windpower ile na ana trei juu ya paa ina mpa umeme na serekali znz haiwezi munashindwa na rai wa kawaida huko ulaya ndio nikasema munachekwa na watali ikiwa umeme unakatwa katwa na maji ati hayatoka mpaka usiku wa manane.

ona hapa hii picha plat zake za juwa zimefinikwa na mabarafu lakini ana umeme kwa kijamuangaza kidogo tu kinachotoka sisi znz juwa mtu mpaka usiku joto hulali kama huna feni ikiwa umeme uko au kipepeyo ndio ulale  na znz  hakuna umeme jamaa aibu znz aibu viongozi bora hata musijite viongozi

ona ni usalama hata kwa rai hakuna mawaya ya kuninginiya ovyo
na watu wana umeme wametulia

ona hapa ni jangwa na watu wameweka na nchi yao ina umeme viongozi znz amkeni

viongozi oneni mambo haya juwa umeme juwa umeme hata muangaza kidongo tu umeme

je bado tu hamujuwi mufanye nini viongozi wetu wa znz...?

juwa tu na watu znz nzima itakuwa na umeme mpaka tutawauziya hao watanganyika.

SMZ AU GNU AU SUKARI kama hamuja amka wala hamuta amka tena.

No comments:

Post a Comment