Thursday, June 30, 2011

NCHI YA Z;BAR INA BALOZI TANO TU NCHI ZA NJE NA ZOTE NI DOGO KWA NINI NA Z;BAR NI NCHI...??



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba ni Wazanzibar watano tu ambao wana hadhi ya kuwa mabalozi kamili wanayoiwakisha Tanzania nje ya nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed aliliambiya baraza la wawakilishi. Kati ya Wazanzibari hao wawili tayari wamestaafu kazi akiwemo aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia balozi Ali Karume.
Aboud alisema hayo wakati alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa ni wazanzibari wangapi ambao ni mabalozi kamili wanayoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na vigezo gani vinavyotumika katika kuwachaguwa.
Akifafanua zaidi Aboud aliwataja mabalozi hao kuwa ni Balozi Mohamed Mwinyi Mzale ambaye anaiwakilisha Tanzania huko Sweden, balozi Ali Shauri anayeiwakilisha Tanzania Misri,balozi Omar Ramadhan Mapuri aliyeko China pamoja na Ali Karume aliyekuwa Italia na Hussein Said Khatib huko Oman ambao tayari wamestaafu kazi.
Alifafanua na kusema kwamba vigezo vya mtu kuwa balozi kamili anayeiwakilisha Tanzania ni kufuata ngazi mbali mbali ambazo zipo katika wizara ya mambo ya nchi za nje ikiwemo vyeo na elimu.
Aidha alisema uamuzi wa kuteuliwa kuwa balozi unatokana na rais wa nchi ambapo akiamuwa kumteuwa mtu kuwa balozi basi anakuwa balozi na kumtangaza.
Aboud alisema Zanzibar haina sifa kuwa na ofisi kamili za ubalozi wa nchi za nje ziliopo Tanzania ambapo kwa mujibu wa sheria za kibalozi,makao makuu ya nchi ndiyo huwepo ofisi za kibalozi.
Kwa sasa Zanzibar zipo ofisi ndogo za ubalozi wa nchi za nje ikiwemo ubalozi wa China.India pamoja na ubalozi wa Misri,Oman pamoja na Msumbiji na nchi za Skandinavia. Mambo ya nchi za nje.


mnataka kutuambiya wasomi wote waliyo jaa znz hakuna anaewezakuwa balozi nchi za nje sio..?  au hamutaki kuwachanguwa wasomi munampango wa kupeleka waume WA DADA ZENU NDIO WAWE MABALOZI WA ZANZIBAR NCHI ZA NJE...? MUTAHONGANA VYEO MPAKA LINI JAMAA HII 2011 ULIMWEGU USHABADILIKA SO TENA HUYU NI MTOTO WA CHACHI NA HUYU NI WAHALO SASA NI WASOMI TU NYINYI BADO NA UZEMBE WA KUHONGANA VYEO KISA KAMUOWA DADA YAKO DUUUUUH

TANGANYIKA VS ZANZIBAR
MABALOZI WA TANGANYIKA ULIMWENGUNI

No comments:

Post a Comment