Thursday, June 2, 2011

SHAMSI VUAI NAHODHA ATAKA WATANGANYIKA NAO KUWA NA VITAMBULISHO ((KUAMUA MIKOPO YA WANAFUNZI)) KAMA NCHI YA ZANZIBAR ANANIA GANI HUYU..?

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha
 WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amesema serikali itatumia vitambulisho vya taifa kubaini wanafunzi wa vyuo vikuu wanaostahili kupewa mikopo.  Nahodha alisema wapo baadhi ya wanafunzi ambao hawastahili kupewa mikopo hiyo, lakini wamekuwa wakipewa.
 “Kuna wanafunzi ambao wanachukua mikopo wakati hawastahili kupewa, hivyo basi kwa kutumia vitambulisho vya taifa, itasaidia kubaini wasiostahili kupewa mikopo,”alisema.  Nahodha aliyasema hayo juzi katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa kituo cha televisheni cha ITV na kufafanua kwamba suala la kutengeneza vitambulisho vya taifa limefikia kwenye hatua nzuri.
Alifafanua kwamba Aprili 21, mwaka huu serikali ilisaini mkataba na kampuni ya Malaysia kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho hivyo na kwamba sasa wanatafuta fedha ili kuanza shughuli hiyo.
Alibainisha kuwa utekelezaji wa mradi huo ni mgumu kwa kuwa Tanzania ina watu 26 milioni ambao wanastahili kupewa  vitambulisho. Alisema vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa kwa wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara kwa sababu taarifa zao zinatambulika.
 Waziri huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa  kwa polisi endapo watabaini kuna wahamiaji haramu katika maeneo yao ili wachukuliwe hatua za kisheria.   Katika hatua nyingine, Nahodha alisema serikali inaanza kuwarudisha kwao  zaidi ya wakimbizi 37,000 wa Burundi walioko kwenye kambi ya Mtabira, mkoani Kigoma.  
Alisema Serikali itaawaondoa nchini wakimbizi hao kwa awamu na kila mwezi wataondoka wakimbizi 10,000 na kwamba  hadi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wameondoka wote.Alisema tayari wamefuata sheria zote stahili za kuwaondoa wakimbizi nchini na kwamba endapo watagoma kurudi kwao hatua za kisheria zitafuatwa.


ONENI JUHA HUYU anataka kuanzisha vitambulisho miaka yote bara hawakuwa na vitambulisho ktk mikopo ila sasa yeye kapelekwa bara anawauwa wazenji wenzake bila ya kujuwa. maana hapo znz mpaka leo kunawatu wamenyimwa vitambulisho kabisa hilo la kwanza. pili wanataka kuwanyanyasa watoto wa kipemba watakaopasi wasiwape mikopo kumaliza masomo yao. tatu wameona znz imeanzisha vitambulisho vya urai na wao wanataka kuwa navyo ili wakija znz wanasema sisi sote ni watanzania.ila sisi znz tunajuwa kuwa wao ni watanganyika na sisi ni wazanzibar.mzee karume aliunganisha nchi ya znz na tanganyika mpaka leo mateso tunayoyapata m/mungu ndie ajuwae.jumbe kaunganisha vyama mpaka leo ccm ya znz ni kama tambara la kupingia deki ccm ya bara ili iweze kuishi mahali pasafi na bora zaidi na huyu sasa anawanzilishiya vitambulisho vya kusoma ili waiyuwe elimu ya watu wa znz kutokuja tanganyika na niwatu wetu ndio wanawatumiliya kutumaliza au shamsi na wewe ushajenga dodoma ndio maana uko tayari kutumaliza wazenji sio..?ona alivyo juwa anasema tanzania ina watu millioni 26 wewe juha tanganyika peke yake ina watu zaidi ya millioni 40 na hapo bado hujaihisabu znz pia ukisikiya ubaguzi ndio huu kitambulisho kwa wanafunzi na wafanya biashara ndio nini kama ni vitambulisho wapewe watanganyika wote kuanzi mtoto anaezaliwa leo mpaka kizee cha miaka 100 au 200 wote wapewe vitambulisho hii ndio haki ulimwenguni kote.wewe juha na ndio sheria ya nchi kuwatambuwa wananchi wake na wasio kuwa wananchi wake sio uwape wafanya biashara na wanafunzi na wengine hawana. sasa sindio ubaguzi huwo sasa juha wewe umesoma wapi..? ahh nimekumbuka munagaiyana vyeo tu wenyewe kwa wenyewe hata kama hamukosoma munapeyana tu kama chupi.wazenji tuamkeni viongozi kama hawa hatuwataki kabisa znz kama tunataka maendeleo la kama ndio bado tunataka kuburunzwa sawa.

1 comment:

  1. Huyu hana lolote,anajipendekeza sana ili apewe nafasi ya kuwania urais wa zanzizbar na yuko tayari kuimaliza zanzibar apate kitumbua chake

    ReplyDelete