Wednesday, June 29, 2011

JAMAA TANZANIA NDIO TANGANYIKA TUSIFANYWE WAJINGA WASHATUBURUZA MIAKA 47 SASA BADO TU.


TANGANYIKA YA ZAMANI

TANGANYIKA YA SASA WAKISEMA Z;BAR DOGO
KISHA WANATAKA KUJITAWALA WENYEWE KANCHI
KADO KADO KWELI
Kama Koko Abuu Bakari ni Mwana Sheria basi kuna vipengele vya sheria
hakuvipitia vizuri? kwanza ni sheria na haki za mthulumiwa, ambao
Wzanzibar kwa mujibu wa sheria ndio wathulumiwa wakubwa tokea mwanzo wa
huo mfumo mzima na utaratibu wake wa Muungano.
Haiwi nchi dogo kama hizi MALTA, ANDORRA, LIECHTENSTEIN,  LUXEMBOURG,ziko ktk umoja wa nchi za ulaya na wanakila kitu chao na wala hawakulazimishwa kujiuga mpaka wananchi wao walipokubali ndio nchi zikajiuga sio mambo kulazimishwa tu, sasa wahusika wa Muungano ni wzanzibar
wenyewe na hawakuulizwa na hivi sasa koko Abuu Bakari sijamfahamu alipo
sema hata hio mswada wa maoni ya katiba mpya basi wananchi wataangaliwa
maoni yao? alipo ulizwa na muwakilishi wa chake chake kuwa wananchi
wakiamua kusema Muungano basi jee vipi koko Abuu? koko asema eti tutapima na
hayo maoni yenye jee vipi hayato hatarisha ulaji wetu ? maana mimi
naona koko kajibu utumbo?.
Mara zote hakuna mtoto kumzaaa mzee? sasa kati ya Wzanzibar na akina
Abuu na wenzake ipi power? mimi naona koko Abuu nimiongoni mwa watu wenye
kuhitaji sifa kutoka Tanganyika na kuwakandamiza Wzanzibar.
Maana kisheria Wzanzibar Muungano upo au haupo? Muungano mimi nahisi
haupo maana huwezi kufanya ushirika na Kombo kesho ukambiwa umefanya
ushirika na Nyange? ushirika ninao fahamu mimi ni makubaliano yani ni
(agrement) hata ndoa basi zina Agrement M/mungu katuwekea(cheti cha
ndoa) sasa na huu Muungano wetu unao Agrement kama ipo na nisikiavyo
kuwa Agrement ni kati ya Tanganyika na Zanzibar? sasa kinacho
tuchanganya Wzanzibar nikuwa leo twambiwa Tanganyika haipo ipo Tanzania
From no where?.
Sasa kweli koko Abuu Muungano ni halali? na baado tuendelee kulinda na
kuenzi? mimi nahisi koko Abuu unamsadia Aduwi na Mradi wake wakuimaliza
Zanzibar kwa jina la ubatizo Tanzania.
koko Abuu katika huo mkataba wa Muungano(Artcle of Union) kuna kipengele
gani kilicho andika Tanzania? a.) b.) Kama Muungano kisheria ni halali?
Jee ilipo vunjwa Tanganyika na Bunge la Tanganyika na Katiba ya
Tanganyika ambae ndio mshirika wa Zanzibar Memba Baraza la Mapinduzi
au   Baraza la Uwakilishi la Sasa jee Mulishauriwa kisheria au vipi na
kama mulishauriwa uko ushahidi wowote?
C.)  Kama hamukushauriwa jee Bado Muungano nihalali? na Kama nihalali
jee mkataba wa Muungano umetaja Muungano huu sasa ni wa Tanzania na
Zanzibar? Yani mkataba umefanyiwa marekebisha na Sulusi 3 za wahusika wa
pande mbili za Muungano?
Jengine ni kiungo cha Mkataba wa Muungano Arcle of Union? Raisi  Wetu
wa Zanzibar ndio kiungo kikubwa cha Muungano kwa vile Rais kapigiwa kura
na Wzanzibar ambae anawakilishi watu wake sasa kiungo cha Muungano hivi
sasa kinacho wawakilisha Watu wa Zanzibar ktk Muungano ni kipi ikiwa
Rasi wa Zanzibar states yake ktk Muungano ni Waziri asio na wizara
maalum yani hata ofisi Bara hana ya Muungano na ni mjumbe wa baraza la
mawaziri . Jee bado Muungano ni halali.......?????
Na ikiwa tuchukulie anae wakilisha Muungano ni Dr Bilali sheria gani na
ridhaa gani ya kuwawakilisha wazanzibar? kama mimi siko ktk ccm/cuf au
ktk chama chochote jee bilali kapata ridhaa gani kwangu mimi Mzanzibar
aniwakilishe wakati mimi sio ccm wala sina chama?.
Na kama Muungano koko Abuu ni halali kisheria Yapi mambo yasio ya Muungano
Bara na yanasimamiwa na katiba gani isio ya Muungano ikiwa Tanganyika
ndio haipo? b.) Jee nivikaao vingapi vilivyo kwisha kaa  Baraza au Bunge
linalo jadili mambo na rasilimali za Tanganyika lililokaa kujadili
mambo yao ya sio ya Muungano?.
Na jee koko Abuu bakari SMZ na wajumbe wa Baraza la Uwakilishi na
Wanasheria kwa vile Muungano ni halali Jee tumerizika kuwa na mshirika
mpya Tanzania badala ya Tanganyika? na kwa zamira gani na nia gani kufaa
kwa Tanganyika ikawa haitajwi wala kusikika tena kama Zanzibar lengo na
mazumuni ni nini?.
Au nikupata mwanya wa kuwa utaifa wa Zanzibar na kuwa na sera ya
serekali 1 Tanzania lakini power tafauti? Hivi sasa kilicho badilika ktk
Serekali ya Tanganyika ni jina tuu nisawa na Zaire ya zamani kuita
Kongo lakini nembo za nchi nizile zile za awali za Tanganyika kama nembo
ya Taifa ya Adam na Hawa? na Katiba ya Tanganyika ndio hii hii ya
Tanzania kuna vipengele tu flani vimebadilishwa lakini haiizuru
Tanganyika.waz;bar tunasema imetiwa viraka teleeeeeee
Jee koko Abuu na Wajumbe wa Baraza Mumerizika na mapungufu yote mazito na
makubwa kuwa bado Muungano ni halali na tuwenzi na kuudumisha? kwa nini
Tanganyika isiwepo kama kweli Muungano ni halali.
Mimi nahisi Muungano umeshapoteza uhalali wake tokea kufa kwa Tanganyika
na nyiyi viongozi au munao jita wana sheria kuna mpango wakutupeleka
ovyo kutokana na maslahi yenu mulio wekeza Bara ya kibiashara, sisi
hatuko tayari Wzanzibar kuza nchi kwa maslahi ya wafanya biashara waloko
Bara au kusema ukivunjika Muungano watakwenda wapi? warudi nyumbani
bado tunawahitajia,la kama hawataki watakuwa kama dugu zetu waliyokuweko,OMAN,U.A.E,U.K,HOLLAND,CANADA,U.S.A. N.K , jee nibora kurudi nyumbani au kubakia ugenini huko tanganyia...????
Zanzibar itajengwa na Wzanzibar wenyewe wenye ari na uchungu wa nchi yao
na kila Wzanzibar wakiondoka basi ndio hasara ya Zanzibar maana mipango
ni kuingiza wageni kwa wingi na kuua Uzawa wa Kizanzibar, Zanzibar ni
ndogo hata ukilinganisha na Mkoa wa Murogoro una watu wengi kuliko
Zanzibar kwa hio kupotea kwa Identite ya Kizanzibar nimara moja tu.
Haingii akilini kabisa kwa mtu mwenye akili timamu kuwa watu million 44
kughaghania kuungana  na watu million 1.2 nikuonyesha wazi kuwa wanalao jambo mbona hawaugani na kenya,uganda,malawi na zambia na hizi ni nchi walizo shikana nazo haswa kimipaka hii sio halali ni thulma na uonevu mkubwa.
Mungu ibariki Zanzibar na ujalie imani nzuri viongozi wetu wabadilike ili kuinusuru Zanzibar na kizazi chake kisijeuangamia na asiye badilika basi wewe muhukumu hapa duniani na kesho akhera pia kama wanavotuthalilisha sisi na wao wathalilishe hapa duniani tukiwaona na kesho akhera pia..

No comments:

Post a Comment