Wednesday, June 29, 2011

ZOP YAISAIDIYA VITANDA HOSPITALI YA MNAZI MOJA


Ahsanteni kwa msaada




Hoteli ya Serena Inn ya Zanzibar kupitia Jumuiya isiyo ya
kiserikali, Zanzibar Outreach Program (ZOP) inayojishughulisha
 na huduma za jamii,
imekabidhi msaada wa vitanda 14, magodoro na vifaa vingine
 vyenye thamani ya shlinngi milioni 55 vilivyotolewa msaada
 kutoka Hospitali ya St. Jude ya Uingereza kwa ajili ya
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ya Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar,
 Dk. Malik Abdallah Juma (wa pili kupia), Mwenekiti wa
 bodi ya wadhamini wa ZOP, Maalim Mohammed Idrissa,
 na Meneja wa Serena Inn Daniel Sambai na wafanyakati
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye sherehe ya
 makabidhiano iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena Inn
 Mjini Zanzibar
HOSPTALI ya Rufaa ya Mnazimoja leo ilipata vitanda
 maalum 14 vya wagonjwa ili kuongeza mahitaji ya
 vifaa hivyo kwa wagonjwa.
Vitanda vyenye thamani ya shilingi milioni 55.4 ni
msaada wa taasisi ya kiraia iitwayo
 Zanzibar Outreach Group (ZOP) kwa wagonjwa
wanaolazwa hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa ZOP, Kuki Aggarwal, alisema wakati
wa makabidhiano ya vifaa hivyo kuwa, vitanda hivyo
 vimetolewa kwa taasisi yake na Hospitali ya
St Jude ya Uingereza, kupitia
Aga Khan Foundation huko Zanzibar.
Aggarwal alisema taasisi yake imeamua kutoa
vifaa hivyo kwa Hospitali ya Mnazimoja chini ya
utekelezaji wa mpango wake endelevu wakusaidia
sekta za huduma za afya, maji na elimu.
Msaada wa vitanda hivyo ulikabidhiwa kwa
 Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya
Afya Zanzibar, Dk Malick Juma na Meneja wa
Hoteli ya Serena, Daniel Sambai.
Akiipongeza taasisi ya ZOP kwa msaada huo,
 Dk Malick alisema vitanda ni miongoni mwa
mahitaji muhimu kwa hospitali hiyo ya Mnazimoja
 yenye jumla ya vitanda 400.
Hata hivyo, Dk. Malick hakueleza kama
Hospitali ya Mnazimoja ina upungufu wa vitanda
 au imejitosheleza kwa mahitaji hayo, lakini
 hospitali hiyo hivi sasa inakabiliwa na ukosefu
wa vifaa muhimu katika chumba cha wagonjwa
 mahututi (ICU) bvaada ya mashine zote za tano za
 kusaidia wagonjwa kupumua kuharibika tangu mwaka jana
nivizuri kusaidiya maana hospitali ya mnazi moja
 sio hospitali ni gereji haswa na haya yote yanaletwa
 na mawaziri wasio na huruma wako wapi mawaziri
 wa afya na manaibu wake wanafanya nini...? kuiba
na kujaza matumbo yao toka bajeti itoke mbona hatujawasikia...?

No comments:

Post a Comment