Saturday, August 6, 2011

SHAMSI VUAI NAHODHA ASEMA HIYO NI SEHEMU YA TANZANIA.

 NYOKAA
SERIKALI haina mpango wa kurudisha utaratibu wa zamani wa wananchi wa Tanzania Bara kuingia Zanzibar kwa kutumia pasipoti.Taarifa hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, wakati alijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwanamrisho Abama (Chadema), aliyetaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kurudisha utaratibu huo ili kudhibiti wimbi la watu wanaoingia Zanzibar na kufanya uhalifu.Nahodha amesema, hakuna ulazima wa kutumia hati ya kusafiria kwa Watanzania Bara wanaokwenda Zanzibar kutokana na ukweli kwamba, hiyo ni sehemu ya Tanzania.
Amesisitiza kuwa, raia yeyote wa Tanzania ana uhuru wa kwenda sehemu yoyote ya
nchi bila ya masharti.Katika swali la msingi, Mwanamrisho alikuwa ameomba kujulishwa juu ya kuongezeka
kwa wimbi la mauaji na ujambazi katika mji wa Zanzibar na kauli ya Serikali katika kutokomeza hali hiyo.
Hata hivyo, Nahodha alikanusha kuwapo kwa wimbi la mauaji na ujambazi na kusema
hali ya uhalifu Zanzibar ni ya kawaida na ni ndogo ikilinganishwa na miji mingine ya Zanzibar.
Ameongeza kuwa, takwimu zinaonesha kupungua kwa matukio ya mauaji na ujambazi
akitolea mfano kuwa, katika mwaka 2008 kulikuwa na matukio 15 ya mauaji  ni kidogo au anathani huyu wazenji ni kuku tu waache wauliwe..?na 15 ya ujambazi. mimi nauliza watu 15, mwaka 2009 kulikuwa na mauaji 22 na matukio 6 ya ujambazi, mwaka uliofuata kulikuwa na mauaji ya watu 15 na tukio moja la ujambazi.“Na hata katika mwaka huu wa 2011, kumekuwa na tukio moja tu la ujambazi na
  5 ya mauaji. Hii inaonesha jinsi hali inavyozidi kuwa shwari tofauti na
Mheshimiwa Mbunge anavyoeleza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la mauaji na ujambazi Zanzibar,” amesema Waziri Nahodha.

No comments:

Post a Comment