Tuesday, January 31, 2012

HICHI NI KIKAO CHA VIONGOZI WALAFI WANAFIKIRIA MATUMBO YAO NA KUTAKA KUIBIYA RASLIMALI ZA WAZANZIBAR

IMG_3725
Kikao cha kamati ya pamoja ya serekali ya TANGANYIKA(( Tanzania)) na Serekali ya Zanzibar kimekutana chinI ya Mwenyekiti wanae muita Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa ((Tanzania))sisi tunajuwa ni makamuwa wa raisi wa TANGANYIKA Dr.Mohd Gharib Bilali.Kikao hicho kilicho husisha Mawaziri,makatibu Wakuu,Watendaji wa Serekali Wakiwemo pia Wataalamu Kilifanyika kwenye ukumbi wa Blue Ubungo Plaza Mjini Dar es Salaam.Wajumbe wa Kikao hicho walikubaliana kuthibitisha kumbu kumbu za kikao cha Kamati ya pamoja ya SMT na SNZ cha Tarehe 2 Juni mwaka 2010 kilichokutana Bwawani Mjini Zanzibar.Halkathalika Wajumbe hao walipitia Taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na Kikao hicho ambayo ni ushiriki Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki((hatutaki muungano na tanganyika vipi sasa wanataka kujadili mambo ya afrika mashariki wazanzibar hapa ndio tuelewe kuwa sisi rai hatuthaminiwi wao wanafanya wayatakayo wavimbe mitumbo yao)), Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia,Uvuvi katika ukanda wa Bahari kuu na Ushirikiano wa Zanzibar katika Tasisi za nje.((mbona hawakutaja gesi yao,almasi zao,thahabu zao,tanzanaiti zao wala maka ya mawe yao hawataji kila ukisikia ni mafuta ya zanzibar ndio muungano huwo....?MIJAMBAZI MIKUBWA NYIE SIO VIONGOZI.
Tarifa nyingine ni ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika tasisi za Muungano, Mgawanyo wa mapato na faida yatokanayo na Bank kuu , Malalamiko ya wafanya biashara kutozwa kodi mara mbili waingizapo Bidhaa zao Tanzania Bara,usajili wa vyombo vya moto, likiwepo pia ongezeka la gharama za Umeme wa Tanesco kwenda ZECO uharamia na utekaji nyara meli.
Katika majadiliano hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Dr Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazo husika kutowa maelezo ndani ya kipindi cha miezi mine utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia.((MUNAMSIKIYA ZIMWI HUYU ANAVYOTAKA KUIMALIZA ZANZIBAR..?
Mapema mwana sheria mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Othmani Masoud Othman Taratibu zote na Baraka kuhusu swala hilo zimeshachukuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Mapindizi na Baraza la Wawakilishi na kuliwakilisha Serekali ya Muungano kwa hatuwa za kisheria.
Naye makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisisitiza hoja ya kuwa na ratiba malum ya vikao pamoja na kupunguza urasimu wa utekelezaji wa mamuzi yanayofikiwa katika vikao hivyo vya pamoja.
Balozi Seif alisema itapunguza kero zilizopo na hatimae kuamsha ari ya kuimarisha Muungano kwa pande zote mpili.
Nirahisishieni kazi ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wake wako Solidarity na hakuna mjumbe wa CCM wala CUF katika swala lolote linalohusu Muungano,alisisitiza Balozi Seif.
Katika kikao hicho upande wa wajumbe wa Serekali ya Muungano uliongozwa na Waziri mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda wakati ule wa Zanzibar uliongozwa na makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif Ali Iddi.

No comments:

Post a Comment