Thursday, January 19, 2012

KAMA SEREKALI YA KINAFIKI GNU HAIWEZI KUVUNJA MUUNGANO BASI WANANCHI TUVUNJANI AU TUNAOGOPA....?

 Hiloooo suala la bahari kuulaenda umoja wa mataifa (U.N)                                                                                                                                                            Kudai mipaka ya bahari ni hatua ya kunyang’anywa na kuchimbwa
      mafuta yetu Z’bar.
Ndugu zangu wazanzibari,AMKENI JAMAA AMKENII
Serikali ya Tanganyika yenye jina la Tanzania imekua na utaratibu wake siku zote mambo ya muungano kuamua wao peke yao bila hata kuyajali mawazo ya wazanzibari au kuwashirikisha Serikali ya Zanzibar, nasema haya kwakua imezoeleka hivyo katika mambo mengi tunayopitishiwa kwa sindikizo la muungano, haya ni matunda ya ubwege na upumbavu na ujuwa wakuto kusoma alioufanya Karume kuunganisha Nchi kibubusa bila kuangalia hatma ya taifa kwa baadae wala kuwashirikisha wananchi wa zanzibar matokeo yake tumetawaliwa kuanzia 1964 mpaka leo hii 2012 tuko chini ya utawala wa kikoloni wakitanganyika.

Kwa mujibu wa mkataba wa muungano katika mistari ya mwanzoya nakala hiyo inazungumza kuwa Mataifa haya mawili yaliungana kuunda jamuhuri moja (Nchi Moja), nah ii ilithibitishwa na Kikwete baada ya Pinda kusema Zanzibar si Nchi, yeye akasema mataifa haya mawili yaliungana kuunda taifa moja na akaengeza kuwa “ukiwa ndani ya Tanzania Zanzibar ni Nchi ukitoka Nje Zanzibar si Nchi” kauli hizi na nyenginezo za viongozi wa Tanganyika zinaonesha wazi kutoitambua Zanzibar kama ni Nchi hadi hii leo, Marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar syabezi ila hayana faida yeyote kwakua bado tupo palepale serikali ya MKOLONI MWEUSI  inafanya itakavyo na haiwi lolote, na wasiwasi wangu mkubwa hii katiba mpya pia inakuja kutubamiza na kuyameza marekebisho yaliofanywa na Baraza la Wawakilishi ya kwamba Zanzibar ni Nchi.
Katika mambo ambayo yaliwakera watanganyikani kuibadilisha katiba yetu na kusema kwamba Zanzibar ina mipaka yake ya asili, hili ndio kusudio la mada yangu, kwakua katiba ya Jamhuri ya muungano ya sasa inatamka wazi kuwa eneo la na mipaka ya Tanzania ni eneo lote la Tnganyika na eneo lote la Zanzibar, hapa ikiimanisha serikali ya muungano inaweza kufanya lolote bila ya kuwashirikisha SMZ na ndio maana mambo yote wanafanya watakavyona SMZ haifanyi kitu.IMELALA TU KAMA MAJIBWA KOKO MKIA KTK YA MIGUUU
Kwa mfano, katiba ya jamhuri ya muungano inatamka wazi mafuta na gesi ni mali ya muungano,wenzetu wanafaidika na gesi kila leo mabilioni kwa mabilioni bila ya hata senti tano kupewa Zanzibar, na sasa wanayanyemelea mafuta yetu kupitia mipaka ya bahari ili wayachimbe kirahisi. SMZ wao wamebaki “mafuta si mali ya muungano EHEE ABAA MAFUTA SI MALI YA MUUNGANOO MAFUTA SI MALI YA MUUNGANOO MPAKA LINI MAMBO HAYA yatolewe lakini hadi sasa wenzetu hawajataka kwakua watazipoteza pesa za mafuta ya wzanzibari”.
Awamu ya Raisi Amani walijaribu kutaka kufanikisha hili wakashindwa, waliunda kampuni ya mambo ya mafuta ya Tanzania, wakawapa vibali wachimbaji ili waje Zanzibar kuchimba mafuta kwa bahati Waziri Mansoor Yusuf akalivalia njuga suala hili likakwama, na Baraza la wawakilishi likatamka wazi “ Hata kama kuna tone moja tu la mafuta basi litachimbwa na wazanzibari wenyewe” lakini hatua hii ya serikali bado haijakwamisha azma ya mtawala MKOLONI MWEUSI  kwa Zanzibar.
Mwaka jana tumeshuhudia sote Pinda alienda kukagua meli za mafuta na hili halikuwa suala la kupuuzi labda Pinda alienda kutembea tuu lahasha ilikua tayari mipango yao wanakamilisha na ndio maana inaombwa mipaka ya bahari ili uchimbaji uanze, na kama si leo basi kesho ilimradi hilo limo katika mipango yao. U.N. ni marekani, hapa naona mmarekani nae anataka fungu lake aidhinishe mipaka ya bahari ili watu wachimbe mafuta nayeye aingie kwenye mgao.
Mipaka ya ya bahari yaTanganyika ni midogo sana tokea asili kwakua Nyerere aliiba majangwa tu ili kujilimbikizia eneo kubwa la mitaa za mraba, baadae ili kuipata bahari akafanya jitihada za makusudi kufanikisha muungano leo ndio hayo tunayaona, serikali ya SMZ haina nguvu hata ya kujikuna ipo ipo tu na wala haifanyi kitu kwakua wanaotuongoza ni wale wale CCM, si serikali ya umoja wa kitaifa bali ni serikali ya Paa moja la Kitaifa, na wanawaridhia watanganyika walitakalo, wanaokumbuka sera za Rais Shein alipokua akiomba kura wazitafute zilikua zinazungumzaje kuhusu mafuta na muungano watapata jawabu.
Tukitaka salama na Nchi yetu tujitoe kwenye muungano, wenzetu hawana nia safi ya umoja na udugu, wanalotaka wao ni kututawala ili milele tubaki maskini wa kutupa,na rasilimali zetu wazitumie wao na baadhi ya wanafiki wa Zanzibar kwa maslahi ya matumbo yao.
AGIZO:
Serikali ya Zanzibar kupitia Baraza la wawakilishi tunataka msimamo wenu juu ya hili wacheni kujadili kuhusu maposho ya wastaafu jadilini mambo ya maana mipaka ya Nchi yetu na rasilimali zake ziko kwenye hatari, eti posho la simu la mstaafu kwa mwezi liwe laki tano jamani huo ni mshahara wa wafanyakazi wa4 wa kawaida, wateteeni wanyonge wekeni pembeni maslahi yenu binafsi ili Nchi iwe huru kwanza kisha tukijitawala wenyewe haya yote yatakuja bila ya shida maana tutakuwa na mafuta hata wastafuu wakitaka laki7 sio neno mafuta ni kitu kikubwa oneni QATAR INAVYOTIGISHA ULIMWENGU WACHINI UJINGA FUATILIYENI KUJIKOMBOWA KWANZA ILI ZANZIBAR IWE HURU.
Kila la kheri Zanzibar,
Umoja, ,mshikamano,uhuru

2 comments:

  1. Umeandika mengi, lakini all in all Zanzibar sio nchi, ila yenyewe inajiita nchi. Hata Idd Amin alijipa vyeo vya kijeshi, lakini vyeo vya kujipa havina maana yoyote kama wengine hawakutambui!

    ReplyDelete
  2. umesema iddi amani yule ni mtu sio nchi sasa usimfananishe mtu na nchi ungesema uganda ilijita nchi na ilikuwa sio nchi watu tungelikuelewa lakini unasema iddi amini si nchi kwanza jifunze kiswali vizuri inaonyesha sio lugha yako.pili umesema nimeandika mengi ndio je yana ukweli au hayana ukweli...? kama yana ukweli basi hakuna tatizo maana mimi nataka tu ujumbe na ukweli uwafikiye watu la kama hakuna ukweli nikosowe zanzibar haijiti nchi ila wazanzibar ndio wanaita kuwa ni nchi yao na hao hao wazanzibar ndio wanajuwa kama ni nchi ila imenyanganywa uhuru wake na kuletwa propaganda zisizo za msingi ila kila la mwanzo lina mwisho na mwisho wa uwongo wa kitanganyika kutaka kuitawala zanzibar umeshafika mwisho ndio maana wengi wenu munaumiya sasa kuona yule aliyekuwa amelala ashamka.

    ReplyDelete