Tuesday, January 17, 2012

KARUME ASEMA UHURU WA 1963 ZANZIBAR ULIKUWA WA BANDIA HAHAHA HAHAHAAH


HII NDIO BENDERA YA UHURU WA ZANZIBAR 1963

HII NDIO BENDERA ILIYOKUJA KUINGOWA
UHURU WA WAZANZIBAR MANA ALIKUJA NAYO
JOHN OKELLO NA HUYU JOHN OKELLO SIO MZANZIBAR ALIKUWA NI NYIKA WAKUTOKA UGANDA SASA MAPINDUZI HAYO UNAYOSEMA NI HAKI KWELI NI YA HAKI YA KULETWA NA WANYIKA NA MACHONGO AU YALE TULIYOPEWA NA MUENGEREZA NDIO YA HAKI..? WEWE UNASEMA NINI..?
Mh.Karume sherehe za Mapinduzi miaka 46
  • Adai uhuru wa 1963 ulikuwa bandia!?
RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, amesema kauli ya ‘mapinduzi daima’ isiwatishe wananchi, kwani maana yake halisi ni kuwapatia wananchi wa Zanzibar mageuzi ya kimaendeleo.
Dk. Karume, alieleza hayo jana wakati akifungua jengo jipya la skuli ya Mwembe Shauri, iliyojengwa kwa msaada ZAYADESA, kwa kushirikiana na serikali Mbunge, Mwakilishi na wadau wengine.
Alisema kwa muda mrefu wapo baadhi ya watu wamekuwa na wasiwasi juu ya kauli hiyo kwa dhana wanazozijua wao, ambapo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani dhamira ya serikali ya juu ya kauli hiyo ni kuwapatia wananchi maendeleo daima.((ZANZIBAR ILIKUWA NCHI YA KWANZA KUWA NA UMEME WA TAA ZA BARABARANI KABLA HATA YA LONDON SASA HATA UMEME HAKUNA MAENDELEYO NGANI UNAYOYASEMA...?
Alisema serikali ya ukoloni haikuwapa fursa wananchi wote kupata nafasi ya kusoma kutokana na kuwapo kwa skuli chache na idadi ya wanaopata elimu ilikuwa ni ndogo, huku serikali hiyo haikuwa ikichukua
bidii kufanya mabadiliko yoyote katika sekta hiyo.((MUWONGO MNAFIKI MKUBWA MAMA YANGU KASOMA MPAKA KAMALIZA NA NI MUAFRO SHIRAZI WALA HAKUBANGULIWA WALA HAKUSUMBULIWA ILA MIJITU MINGINE ILIKUWA MIVIVU HAITAKI KUSOMA UNASEMA NINI WEWE...?
Alisema baada ya Mapinduzi 1964, serikali iliyoingia madarakani iliweza kuibadili sekta ya elimu kila mwaka kwa kutoa elimu bure, jambo ambalo limeongeza idadi ya skuli na kutoa nafasi zaidi kwa wananchi wa Zanzibar kupata elimu.((SAWA HAYA MBONA WAKIMALIZA FORM4 NA FORM6 HAWANA HATA KAZI YA KUFANYA BASI..?MBONA WATU WANAMALIZA KUSOMA FORM6 NA FORM4 HAWAJUWI HATA KUZUNGUMZA KIENGEREZA AMA KWELI MUMEIBADILISHA SEKTA YA ELIMU NA KUTUFANYA WAZANZIBAR MAJUWA.
Kutokana na kuwapo kwa hali hiyo Dk. Karume, alisema ndio maana serikali ya Zanzibar imekuwa ikisema mapinduzi daima kwa vile hayo ni maendeleo ambayo yamepatikana baada ya Mapinduzi kwani kabla ya hapo hayakuwapo(( HAYOO YA UJUWA SIO....?
Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inapenda kuona inawapatia wote fursa za kupata elimu na ndio maana imekuwa ikichukua juhudi kujenga majengo mapya na ya kisasa ili wananchi watumie fursa hiyo bila ya ubaguzi kama ilivyokua wakati wa ukoloni.((SASA NDIO KUNA UBAGUZI JINA MOHAMMED,ALI,ISMAIL KATAKATA ILA FAKI,JECHA,PANDU WANAPASI AU SIO..?
Alisema Zanzibar tangu kuanza kutekeleza sera ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Zanzibar imekuwa nchi ya mfano ikilinganishwa na nchi nyengine katika bara la Afrika.((HAHAHAHAHHAHAH UNACHEKESHA SANA TENA SANA HAHAHAHAHA KAMA NCHI NGANI YA AFRIKA MUNAYOTAKA NYINYI KUPINGIWA MFANO ..?HAHAHA
Alisema hiyo tangu kutangazwa kwa malengo ya Milenia zipo juhudi mbali mbai ambazo serikali imezichukua kuibadili sekta ya elimu kiasi ambacho tayari imeweza kuifikia dhamira hiyo.
Akizungumzia juu ya uhuru unaodaiwa kupatikana mwaka 1963, alisema hilo halipo kwani ulikuwa ni wa bandia na aliyepewa uhuru huo ulikuwa ni utawala wa kisultani.((ALAA SIKILIZA HII SAUTI NI YA KISULTANI KWELI AU....?

Kutokana na hali hiyo, Dk. Karume, alisema uhuru wa Zanzibar ni wa 1964, ambao ulitokana baada ya kuondolewa madarakani utawala wa mkoloni.((UNASEMA KWELI KWA HIYO UNAFURAHIYA KULIWA KWA WAZANZIBAR 1964 NA KUHARIBIWA DADA ZETU NA MAMA ZETU NA MACHONGO WALIYOLETWA NA NYERERE SIO..?
UHURU HUU UNATAMBULIWA NA NYINYI SIO DUNIA
WALA MWENYEZI MUNGU BABA YAKO YUKO WAPI..?
TUBU KWA MOLA WAKO KABLA HUJENDA NA WEWE PIA.

AMANI KARUME UKIWA HUMU NDANI MAPINDUZI DAIMA HAYATA
KUSAIDIYA WALA KISONGE KAA UKITAMBUWA HILO.
Alisema uhuru huo ndio ulitambuliwa na dunia nzima yakiwemo mataifa ya Afrika, huku nchi zilizokuwa zikiitawala Zanzibar ikiwemo Uingereza ndio iliyochelewa kuutambua uhuru huo.
Mapema Dk. Karume aliifungua rasmi jengo la skuli ya Mwembe Shauri ambapo katibu Mkuu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mwanaidi Saleh, akitoa maelezo ya kiufundi alisema thamani yake hadi
linakamilika ni shilingi milioni 222,492,444.
Alisema kati ya pesa hizo serikali ya Zanzibar imetowa shilingi milioni 122,813,524 na ZAYADESA imetoa shilingi 99,678,920 ikiwa ni mchango kwa ajili ya kununulia vifaa pamoja na kuwalipa mafundi.
Mapema Mwalimu Tatu Suleiman Ubwa, akisoma risala ya Walimu wa skuli hiyo waliishukuru Jumuiya ya ZAYADESA na serikali kwa kufanikisha ujenzi wa skuli hiyo na kuiomba kuangalia uwezekano wa kujenga skuli nyengine inayofanana na hiyo kwenye eneo hilo.
Katika sherehe hizo pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAYADESA, Mama Shadya Karume, Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Abdalla Juma na Mwakilishi Nassor Salum ‘Aljazira’.

No comments:

Post a Comment