Tuesday, January 31, 2012

NCHI YA TANGANYIKA INAIZIKA ZANZIBAR HALI YA KUWA ZANZIBAR IHAI HAIJAFA



Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,tuna muita mshirika wetu wa muungano alitukatalia na kutupa munda tutoke haraka na ndio alipotupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingilia. Kwani, zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
MISUMARI YA MWISHO INAPIGWA SASA  NA TANGANYIKA ((TANZANIA)) KATIKA JENEZA LA ZANZIBAR. JE.WAZANZIBAR MPOOOO AU MUMELALA BADOO.. ?

Ombi la Januari 18,2012 la Tanganyika (Tanzania ) huko Umoja wa Mataifa,New York,  kutanuliwa  mipaka yake ya baharini  ni misumari ya mwisho inayopigwa  kufuatia ule wa  kwanza  katika JENEZA la Zanzibar  hapo April 26,1964. Mara tu baada ya  kuapishwa rasmi Mwalimu Nyerere  kuwa rais wa Jamhuri  ya Muungano ya Watu wa Tanganyika na Zanzibar,kanuni yake ya kwanza aliotunga (decree), ilikua kuifuta Tanganyika  kwa njia za  kiinimacho  na kuibua Tanzania ambayo ni ile ile Tanganyika  aliyoifuta lakini imeibuka na mipaka mipya ya aridhini.Ilijumuisha   visiwa vya unguja na Pemba. Sasa inajiandaa kupiga misumari ya mwisho kwa kutanua zaidi mipaka yake ya baharini na kiliomo ndani yake tangu dagaa hadi papa.mashamba mpaka mjini watu mpaka miti hii ni dalili ya azimio la arusha inaletwa tena kwa njia nyengine bila ya wazanzibar kufahamu nini kinaendeleya ila wakipata ruhusa tu tujuwe tumekwisha tutahamishwo zanzibar tukitaka tusitake ili waigeuze watakavyo kufanya ulanisi na kila balaa.
Tangu 1964, misumari mingi imekuwa ikigongomelewa jeneza letu  tena hatua kwa hatua; na sisi wazanzibari  twatazama macho tu.
Kufuatia Muungano uliofanyika bila umma kuulizwa ndewe wala sikio, akiba kubwa ya fedha za Zanzibar katika Bodi ya ile iliokua Jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI  ziliporwa na tunaemwita Mshirika wetu wa Muungano na kuzitia  kibindoni katika Bank yake (BOT) bila ya ridhaa  umma  au ya serikali yatu. Shabaha ilikua  ni kuiua Zanzibar  kiuchumi ili kuidhibiti. Sehemu ya Zanzibar katika  “Currency Board ” ya Jumuiya ile  ilikua 11.2%. Huo ukawa msumari mwengine kati ya mingi katika jeneza letu. Licha ya juhudi nyingi za Viongozi wetu , walishindwa kuzuwia hilo. Kwani wenzetu hizo wanazoziita “KERO” ndio “MISUMARI” wanayoigongomelea JENEZA LETU hadi watapotuzika kabisa.
Msumari mwengine mjarabu kabisa ni kule  kuunganishwa kwa Afro-shirazi party (ASP) na TANU, 1977 kinyume na  Marehemu mzee Karume alivyowausia   wandani wake wasifanye,kwani yeye binafsi hakuridhia hilo katika utawala wake mzima wa miaka 8 .Kwa msumari huo,hatima ya kisiasa ya Zanzibar ilianza kuamuliwa  Dodoma badala ya kisiwandui. Rais wetu Aboud Jumbe alipofanya nyoko huko Dodoma, 1984 , alikiona kilichomtoa kanga manyoya. Kuanzia hapo hata viongozi wetu wa Zanzibar bila ya ridhaa ya Dodoma,ni mwiko  kukalia kiti cha Urais. Wenzetu wanatuchagulia hata   marais wetu-aibu gani hii ?
Msumari mwengine katika jeneza la Zanzibar ni kuondolewa kwa wadhifa wa ” Makamo-rais ” na kumfanya Rais wetu kana kwamba ni   rais wa kilabu cha mpira cha ” MIEMBENI SPORTS CLUB”. Hana nchi hata akiwa na bendera....SASA AMEKUWA BOYAA TU SHEIN SIO RAISI.
Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,ana jiitaa mshirika wetu wa muungano alitutia munda na kuupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingia. Kwani,  Zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
KABLA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA MUUNGANO 2014, MAITI  ya (ZANZIBAR) iwe tayari kuzikwa kupitia KATIBA MPYA YA SEREKALI YA TANGANYIKA. Zanzibar inazikwa kule kule UMOJA WA MATAIFA,NEW YORK, na sio Mwanakwerekwe ambako kaburi lake lilichimbwa  tayari 1964   pale kiti chake kama dola huru huko kilipotoweka kwa  kiini macho. TANGANYIKA((Tanzania)) inajua kucheza turufu  zake huko  ili kuizika Zanzibar katika  kaburi lile lile iliochimba 1964  kufuatia Muungano FEKI.
Baada ya kupora fedha zetu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki iliovunjika ,sasa tunae muita mshirika  wetu wa Muungano amejianda kupora gesi na mafuta yetu kwa  njia ya kuitanua mipaka ya bahari kama alivyotanua mipaka ya aridhi katika ile Tanganyika kubwa  kwa jina la ((Tanzania.)) Wakati maliasili zao kama gesi,Tanzanite, dhahabu, almasi ,makaa ya mawe na nyenginezo, ni  mali zao pekee yao, mafuta na gesi ya Zanzibar na Pemba  eti ni ubia.
VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NA SISI UMMA WA ZANZIBAR,  TUTATUMBUA MACHO MPAKA LINI ? AU
MPAKA TUZIKWE KABISA HUKU SANDA TUMESHASHONEWA  NA TUNAIONA ?
Kuna usemi “Kila  Umma  hupata viongozi  uliostahiki kuuongoza.Ukiwa  Umma  ni ngangari, utapata viongozi ngngari kama akina  Jussa,Hamza na Mansuri -wenye kupaza sauti kuutetea Umma.La ,ukiwa  Umma ni wazembe, watapata viongozi wazembe.
Wazanzibari mpo ?
Tusigeuke  ile hadithi ya Mnyamwezi ” Ninamtajama tu” kumbe mwenzake anamharibu.Eti anatafuta ushahidi.
USHAHIDI kuwa tuna muita mshirika mwenzetu wa Muungano hakuwa na nia njema tangu awali, ilidhihirika pale alipopiga msumari wa kwanza,April 26,1964 kwa kuifuta Tanganyika .
Ilikua tangu wakati ule Viongozi wetu  wawaambie  ndugu zetu kuwa, BILA YA TANGANYIKA, HAKUNA MUUNGANO.Mumeivunja wenyewe. TUNAWEZA HATA KUWAAMBIA HIVYO LEO LAIT”I TUNA VIONGOZI NGANGARI- KERO ZIMETOKA WAPI IKIWA HAKUNA MUUNGANO.JAMANI “SI ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO ?”
Ningelikua mimi ni  Rais wa Zanzibar,ningekwenda Studio za Raha leo na kulihutubia Taifa nikiwaamrisha wabunge wote wa Zanzibar katika Bunge la Muungano huko Dodoma, warudi Zanzibar mpaka  kwanza waziri-mkuu  Pinda,kwanza  awataka radhi  Wazanzibari na Rais wao pili hao wanao jiitaa washirika wetu katika huo Muungano FEKI,waifufua Tanganyika  walioifuta  kwa kini-macho.
Je, Wazanzibar mpo au tunasubiri kuzikwa kabisa  2014?..lakini UBAYAA HATUNA RAISI HAPA ZANZIBAR TUNA BOYAA TU LAELEYA KATIKA MAJI YA ZIWA TANGANYIKA.
ILI KUZUWIA KUPIGWA MSUMARI WA MWISHO KATIKA JENEZA LETU  ,TUDAI TUJADILI KWANZA UHALALI WA MUUNGANO NA KUIULIZA NCHI TULIYO UNGANA NAYO TANGANYIKA IKO WAPI IRUDI NA KAMA HAWATAKI BASI NDIO TUNAVUNJA KABISA MUUNGANO MAANA KWANZA HAKUNA MUUNGANO KUNA UBABE TU TUSIKUBALI KUJADILI KATIBA MPYA MAANA HAKUNA NCHI TULIYO UNGANA NAYO SASA TUNAJADILIYANA NA MTU ASAYE KUWEPO......? PIA TUKUMBUKENI KUWA. ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO !

No comments:

Post a Comment