Thursday, February 2, 2012

BANDARI YA NCHI YETU YA ZANZIBAR NI BANDARI AU SOKO,JAA,DANGURO NA MAGENGE YA MAMA NTILIYE KUTOKA NCHI YA JIRANI TANGANYIKA..?


Hali ya mandhar ya bandari ya Zanzibar mnaiona, kw akila msafiri na mpita njia. Hali ya mandhari ya bandari hii, ambalo ni lango kuu la kuingilia wasafiri, na uchumi wa Zanzibar hairidhishi, na inatisha, na ni AIBU kwa nchi.
Eneo la nje ya Bandari kwa sasa limejaa biashara za kipuuzi, kama kuuza kadi za simu – zimetanda mwanzo hadi mwisho, kuuza supu, maziwa, na aina zote za biashara zisizostahiki kufanywa pale eneo la bandarini.
Kuna mmachinga pale (mfalme wetu) anakuwa na gari lake la kukokota (tram/rikwama), huyu anauza mpaka condom ukitaka, anazo pia packet za konyagi (ulevi) na kila laana unayoijua wewe pale inapatikana.
Inasikitisha sana kuona hali kama hii imepata blessing na SMZ-GNU under waziri Hamad Massoud (CUF). Yeye kwa bahati nzuri au mbaya – ofisi yake ipo mbele ya uchafu huu.
Awali, alianza kuuz amaziwa bibi mmoja kutoka Bara (Tanga) – huyu alikaa chini ya mlango wa kuingilia, na mpaka sasa yupo. Then, walifuata wengine, mpaka machangu doa wapo pale.
Hivi kweli Waziri Hamad Massoud haoni, au dr.Shein, au Balozi na Maalim Seif …wanapita pale kila siku.
Ukiangalia sana, hata usalama wa pale eneo la bandari ni mdogo sana.
Inanishangaza sana kusikia na kuona Dr.Shein anawaita watendaji Ikulu (ikiwemo wizara hii) ya mawasiliano na miundo mbinu – na anawasifu kwa utendaji mzuri. Hivi huu ndio utendaji mzuri? Mbaya utakuwa upi?
Imekuwa fashion Dr. Shein kuziita Wizara na kuwasilisha work plan zake, hivi kweli mambo kama haya hayaonekani au kwa sababu wauzaji na wafanya biashara hii ni ‘wafalme wetu’ kutoka Tanganyika. Nina hakika ingalikuwa jamaa zetu kutoka Kengeja, Tundauwa, Matangatuani, Finya n.k Wallah wangalikuwa wameshafukuzwa pale. Lakini hawa wengi wao wanatokea huko ‘baitil muqadas’ wafalme wetu ama wametokea Tanga au Rufiji au Kilwa, Mtwara, Temeke n.k – untouched family.
Zanzibar, kimtazamo, wa identity imekwisha sana, haina tena nasaba au mpaka wa kujua nani ni nani, imekuwa mkorogo tu, na uongozi/viongozi wanachangai hili, na GNU ndio imekuja kumaliza, na kuimaliza Zenj Empire. Viongozi wake ni corrupt sana sana.
Kama kweli SMZ-GNU ina nia ya dhati juu ya kuweka mipnago mizuri ya bandari – basi wafanya biashara hawa, wakiwemo wauza supu, maziwa, na wale wafalme wetu pia waondoshwe pale eneo la bandari ya Zanzibar. Natoa hii challenge kwa Hamad Massoud, SMZ, Dr.Shein na VP1 and VP 2.((VP2 SIO SANA MAANA TUNAMJUWA NI DUNGU YAO JE NYINYI MULIOBAKIA....? ))

No comments:

Post a Comment