Thursday, February 23, 2012

JOYCE NDALICHAKO NAE PIA AITA ZANZIBAR NI MKOA RAISI SHEIN KUMBE SI RAISI NI MKUU WA MKOA WA PWANI ZANZIBAR DUUUUUUH!!!!!!!


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani NCHINI TANGANYIKA ((Tanzania)) (NECTA) Dk Joyce Ndalichako
HILI NDIO JINAMIZI LILILOWEKWA KTK BARAZA LA MITIHANI KUWAKATA ROHO KIZAZI CHA NCHI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

WASWAHILI WANASEMA BORA MTU AKUNYIME KULA KULIKO KUKUNYIMA ELIMU NA HAPA SASA NDIO TUNAONA KUWA HAWA WAKOLONI WAUSI WANATAKA KUWANYIMA ELIMU KIZAZI CHA ZANZIBAR KWA MAKUSUDI ILA IWEJE ILI TUSIWE NA WASOMI NA TUKIWA HATUNA WASOMI NDIO HIVYO TENA NIKUBURUZWA NA NCHI YATU YA ZANZIBAR MPAKA KIYAMA KISIMAME NAWAPA HONGERA WANAFIKI NA VITUMWA VYA WAKOLONI WAUSI WALIOKUWEPO UNGUJA NA PEMBA MAANA WAO NDIO WANAOKAZANIA TUWE NA MUUNGANO NA HIZI NDIO FAIDA ZA MUUNGANO HII NI BASHRAAFUU TU NGOJENI KARAMU SASA SHAMHUNA ASHACHINJA NGOMBE NI ILE BAHARI SASA BADO KUPIKWA BIRIANI NA KULIWA TUUUUUUU.


Baadhi ya wazee ambao walishiriki katika kongamano la kutathmini matokeo ya mtihani yaliotangazwa na baraza la elimu Tanzania (NECT) ambalo limewafutia jumla ya wanafunzi 3303 kwa madai ya udanganyifu wengi wao wakielezwa ni kutoka Zanzibar
Na Ally Saleh
Wiki iliyopita ilikuwa ni kubwa kwa habari za matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne kwa taifa lakini zaidi kwa upande wa Zanzibar. Ni hizo zilitikisa bahari ya Hindi hadi visiwa vikawa vinatetemeka. Ilibidi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Joyce Ndalichako afanye ziara ya kuja Zanzibar kuelekezea nini kimejiri mpaka yakatokea yaliotokea ambayo wazee na wanafunzi bado hawajaamini.
Chanzo ni habari za kufutiwa na matokeo na kufungiwa kufanya mitihani kwa wanafunzi zaidi ya 3,000 kote Tanzania kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa ni udanganyifu unaotokana na mfanano usio wa kawaida.
Lakini pia ikaelezwa kuwa kuna mambo mengine yasio ya kawadia yaliotokea kama vile wanafunzi kuandika matusi, kuchora picha kadhaa lakini pia kuandika nyimbo za Bongo Fleva, si matunda ya kizazi kipya bwana. Basi hiyo ikawa ndio habari.
Ila kwa Zanzibar, kama mshirika kamili katika Muungano, wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli za sekondari wakaona maelezo ya Mama Ndalichako hayakutosha na nafikiri habari hii akaijua na akaamua kuja Unguja, lakini basi hapa akaonana na waandishi wa habari, waalimu na maafisa wa Serikali.
Katika kongomano la siku moja liloitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo WAHAMAZA wazee, wanafunzi na wamiliki wa skuli walisema wangefurahi wangekutana nae wao Mama Ndalichako na mzee mmoja akasema “angetafuta mahala pa kukimbilia.”
Kwa nini akasema hivyo? Amesema hivyo kwa sababu anaamini kuwa Mama Ndalichako hakutoa ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kumekuwa na udanganyifu na baya kuliko yote ametoa maelezo aliyoyaita kuwa ni ya jumla jumla, mzazi Ahmed Ali alisema.
Mzazi Ahmed kama watu wengi katika kongamano hili alisema Mama Ndalichako ametoa maelezo mengi ya kujilinda na akikwepa kabisa kukubali ukweli kuwa mtihani ulivuja na hicho ndio sababu ya yote yaliotokezea ambayo yeye anadai hajui chanzo chake.
“Nasema mtihani ulivuja kwa hakika. Mimi mwenyewe niliupata nikiwa katika cyber café moja mjini Dar es Salaam. Na nakala ya mtihani huo ambao ulikuwa kwa Kiingereza na uliokuwa ukisambazwa kwa internet ninayo mpaka leo.”
Washiriki wengi walisema Mama Ndalichako anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa sababu mtihani ulivuja na kadri anavyojitetea na kutoa maelezo ndivyo ambavyo anazidi kujizonga na kujikaanga.
Moja katika maelezo ya Katibu Mtendaji ya kuwepo kwa udanganyifu ni kule kutokea kuwa kumekuwa na karatasi za majibu ya wanafunzi zikiwa zimeandikwa na watu kadhaa na akisema anashindwa kuelewa hilo limetokezeaje wakati wanafunzi wanaodaiwa kuhusika hawakuwa wamekaa jirani kwenye vyumba vya mitihani au chumba cha mithani kwa sababu hakueleza kuwa hilo limetokea shule moja au shule kadhaa.
Kisha akatoa mifano kadhaa iliyoonyesha kuna baadhi ya karatasi za maiibu ambazo wanafunzi waliandika neno kwa neno jambo ambalo halina jawabu nyengine zaidi ya kuwa kulikuwa na udanganyifu tena wa hali ya juu.
Wazee na waalimu walikiri na wala kuwa kulikuwa na udangayifu lakini hoja yao ni kuwa udanganyifu huo ulitokana na kuvuja kwa mitihani ambao sio tu iko chini ya dhamana ya Mama Ndalichako lakini pia inalindwa chembilecho mtu mmoja “ kuliko hata ulinzi anaoupata Rais Kikwete au Dk. Shein.”
Kwa hivyo hoja ya wazee ni kuwa mitihani ilipatikana mitaani. Wanafunzi wakaifanyia kazi. Vitabu vya majawabu vilipatikana mitaani. Wanafunzi wakavitumia kuandika jawabu zao. Na kwa bahati mbaya kila eneo la jawabu akapewa mtu mmoja na ndio maana kitabu kimoja kikaonekana na hata za watu tofuati lakini hati hizo hizo zikaonekana kwenye vitabu vyengine.
Inawezekana kabisa kuwa baadhi ya waalimu na shule zilishiriki katika mchezo huo, walisema washiriki na kwa hivyo ni muhimu kutoa maelezo ya shule kwa shule na mwanafunzi kwa mwanafunzi ili kila mtu ajiridhishe na sio maelezo ya jumla kama aloyatoa, walisema washiriki. “ Kila mzazi anataka kuona mwanawe alishiriki katika visa hivyo au la. Na kila shule inataka kujua shutuma dhidi yake,” alisema Mzee Ali Hassan, Mlezi wa Laurette International.
Walimu na wamiliki wanasema wanajua mitihani ilivuja kwa sababu waliona jinsi ambavyo maafisa wa usalama walivyopekua wanafunzi wao na Mama Ndalichako akikataa hilo ni “kwa sababu ya kulinda kitumbua chake. Lakini kwa hili kitumbua hicho kimeshaingia mchanga na hakiliki” alisema Mwalimu Ameir Hassan.
Wazee na waalimu walishangaa kwa nini Mama Ndalichako alikuja Unguja bila kujitayarisha kujua idadi kamili kuhusu wanafunzi waliohusika kwa upande wa Zanzibar na walikasirishwa na jawabu yake nyepesi tu, “ Sijafanya hesabu ya mkoa kwa koa,” na washiriki wakasema yale yale ya kuona Zanzibar kama mkoa au mikoa mengine tu.
Na ndipo hapo hisia za Muungano zilipokuja na watu wakajaribu kunasibisha tukio hilo na matatizo na kero za Muungano. Walifika hata kuhoji idadi ya Wazanzibari katika Bodi ya Baraza la Mtihani na wakaenda mbali zaidi kuhoji iwapo chombo hicho kikiwa ni cha Muungano kimetoa ajira ngapi kwa Wazanzibari leo au hata jana na juzi kwa sababu kimeundwa tokea 1973 pale jambo hilo lilipofanywa kuwa la Muungano.
Litolewe katika Muungano watu walisema, Tuwe na Baraza la Mitihani letu watu wakapiga kelele suala hili lazima liwe katika ajenda wakati wa Mjadala wa Taifa wa Mabadiliko ya Katiba ambao uko njiani unakuja.
Wengine wakasema tukio hilo lina udini. Matokeo mengi yaliofutwa hapa Zanzibar yanahusu vyuo vya Kiislamu na kudai shule kadhaa za Kikristo huko Bara zinapasisha hadi mwanafunzi mmoja kuwa na kikapu cha alama za “A” lakini hapatiwi shaka au baadhi ya shule kupasisha darasa zima lakini hapatiwi ila katika matokeo kama hayo.
Halili kadhalika walizungumzia juu ya kutokuwepo hatua zinazofanana kwa kesi za aina moja ambapo mwaka jana baada ya kufutwa matokeo ya Darasa la Saba wanafunzi iliamriwa warudie mitihani, lakini pia kuukubwa wa adhabu ya wanafunzi na Professa Abdul Sheriff akiandika katika mtandao alisema, “ Haiingii akili utoe adhabu sawa kwa aliyeandika matusi, aliyechora picha na aliyedaiwa kudanganya katika mtihani.”
Pia yalikuwa ni maoni ya wadau kuwa kufungia wanafunzi kufanya mithani kwa miaka mitatu ni kuwahujumu kisaikolojia lakini pia wakasema ni mbinu za makusudi kuwakosesha Wazanzibari fursa ya kukuza wataalamu wake, maana kitachotokezea athari ya muda mrefu kwa Zanzibar kielimu lakini pia kijamii.
Hivyo wito ukawa kwamba hilo ni janga la taifa. Kama si kwa Tanzania basi kwa hakika ni kwa Zanzibar na kwa hivyo washiriki wakataka hatua za haraka zichukuliwe ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete kumuwajibisha Mama Ndalichako, kuunda tume kuchunguza tukio hilo na kutafuta suluhu ya kudumu ya kuvuja mitihani.
Lakini pia waliitaka Serikali ya Zanzibar kuchukua hatua kwa upande wake na sio kulaza shingo kwa maamuzi ambayo yanaathari kubwa kwa Zanzibar kama nchi. Lakini kubwa zaidi waalimu na wazee hao wamemtaka Mama Ndalichako aje Zanzibar kukutana nao uso kwa uso wakisema hawakutendewa haki kwa yeye kupita katika vyombo vya habari. “ Yeye ni mzazi na aje kwa wazazi wenziwe.”
SHEIN TWAMBIYE UKWELI ZANZIBAR NI NCHI AU MKOA WA PWANI ZANZIBAR...???
AU NDIO KUKU WA IKULU WASHAKUFANYA MASIKIO YAKO YAZIBE UWE HUSIKI
LOLOTE LINALOTOKE HAPA ZANZIBAR......???

No comments:

Post a Comment