Thursday, February 16, 2012

KATIBA YA ZANZIBAR NDIO KATIBA YA KUFUATWA NA WAZANZIBAR SIO KATIBA YA VIRAKA NA SHERIA MPYA YA NAMBA 8 HAITUHUSU KITU SISI WATU WA ZANZIBAR.

JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR      KWANZA

JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR LAZIMA IRUDI ILI KIZAZI KIJACHO
KISIZALIWE TENA NCHI JIRANI BALI KIZALIWE NA KUKULIA HAPA HAP
NCHINI KWAO KTK JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.
Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar.
Vipi sheria ya Mabadiliko ya Katiba iweze kufanya kazi Zanzibar wakati Zanzibar ni Nchi iliyo na mipaka yake Kikatiba? Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi wazi katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza kwamba: “Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR”. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba kupitia kifungu chake cha 19-(1) kinachohusiana na makosa na adhabu kwa watakaotoa maoni nje ya hadidu rejea za rasimu ya Katiba: kifungu hicho pamoja na sheria yenyewe ya marekebisho ya Katiba, mwisho wake CHUMBE tuna sema tena na tena mwisho CHUMBE CHUMBE !!
Pili, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi kuwa, Katiba ya Zanzibar ndiyo yenye nguvu za kisheria nchini kote, ambapo ikitokezea sheria yo yote kutofautiana na Katiba ya Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana. Hii ni kuonesha nguvu na uwezo iliyonayo Katiba ya Zanzibar mbele ya sheria namba 8 ya mabadiliko ya Katiba, na kwamba, Katiba ya Zanzibar ndio “(The Grundnorm, which is the highest form of validity, being of the highest authority, providing efficient and affordable legal representation).
Tatu, hata hiyo Mahakama ya Rufaa, nayo haina uwezo, wala mamlaka, wala haki Kikatiba ya kuitafsiri Katiba ya Zanzibar maana Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza katika kifungu cha 99 kinachohusiana na kazi na uwezo wa Mahakama ya Rufaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA((Tanzania)) haiwezi kutafsiri Katiba ya Zanzibar. Kwa maneno mengine, Katiba ya Zanzibar inajitegemea, na kwa mantiki hiyo, Wazanzibari watahukumiwa kwa yao tu, na si kwa sheria ya mabadiliko ya Katiba wala nyengine yo yote ile tuna sema tena mwisho CHUMBE CHUMBE.
Nne, pamoja na vitisho vilivyomo kwenye kifungu cha makosa na adhabu ndani ya muswaada na sheria ya mabadiliko ya Katiba, bado sheria hiyo haiwezi kuwa JUU ya Katiba. Na sheria yo yote, itakayokwenda kinyume na Katiba, sheria hiyo pia inakuwa batili (unconstitutional). Tunakusudia kusema kwamba, hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA ((Tanzania)) ya 1977, yenyewe, ambayo bado inatumika hadi sasa na imeja viraka, inadhamini UHURU wa wananchi kutowa mawazo na maoni yao kwa uhuru kabisa. Kifungu cha 18, kinachohusiana na haki ya uhuru wa mawazo kinaeleza: “Kila mtu – (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake”. Aidha, kifungu kinachofuata cha 19-(1) nacho kinaeleza: “Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo”. Pia, Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano, Sehemu ya Tatu, inayohusiana na haki na wajibu muhimu, inaeleza kwenye kifungu cha 13-(2) kuwa: “Ni marufuku kwa sheria yo yote iliyotungwa na mamlaka yo yote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lo lote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”. Neno ubaguzi, linatafsiriwa na Katiba hiyo hiyo ya Muungano kwenye kifungu cha 13-(5) kuwa ubaguzi ni pamoja na kunyima haki ya maoni ya kisiasa. Kama hivyo ndivyo, sheria ya mabadiliko ya Katiba inakwenda kinyume na Katiba kwa kuikana haki hiyo muhimu ya maoni ya kisiasa.JE MUNATULETEA KATIBA AU MUNATUONGEZEA UDIKTETA NA KUTAKA KUTUMALIZA....?
Tano, UHALALI wa sheria ya mabadiliko ya Katiba hauwezi kupatikana kwa kupitishwa na Bunge pekee. Ni LAZIMA sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba, pia ipitishwe na kuridhiwa na kukubaliwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Baada ya hoja na maelezo hayo, ni ukweli usio na shaka kuwa, sheria ya mabadiliko ya Katiba, sheria namba 8, haiwezi kuwa juu ya Katiba ya Zanzibar, na kwa ajili hiyo, Wazanzibari Kikatiba, tunao uhuru na haki ya kutoa maoni yetu bila ya hofu wala woga; kama ambavyo Serikali yetu nayo kupitia Katiba ya Zanzibar, ina wajibu wa kudhamini uhuru huo. Ikiwa ni kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba, na si ule Muungano wa Katiba pia ni haki yetu ya Kikatiba. Zama za kutishana na kupigana zimekwisha. Hata Rais Kikwete katika hotuba yake alilisema hilo, na namnukuu: “Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya,                                               

 nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Tutofautiane bila kupigana”. Mwisho wa kunukuu. Tunamtaka Rais Kikwete atembee juu ya kauli yake hiyo kama ambavyo nasi tutatofautiana kwa misingi ya HOJA bila ya kupigana.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. KWANZA!

No comments:

Post a Comment