Saturday, April 21, 2012

KILEMBWE CHA FIRAUNI BALOZI SEIF ALI IDDI

          
HATUTAWAVUMILIA WANAOPINGA MUUNGANO ((NYOKA NI NYOKA TU HATA UMFUNGE NA KUKU BADO NI NYOKA NDIO HUYU BALOZI IDDI HILI NI JOKA TENA KUBWA KWELI KWELI NCHI HII YETU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR IKIPATA UHURU TU KAMA BADO WAPO ZANZIBAR WOTE HAWA WAPANDISHWE MAHAKAMANI

Kundi la watu wanaotaka kuitishwa kura ya maoni kuamuliwa juu ya Muungano uwepo au usiwepo wakiwa katika viwanja vya baraza la wawakilishi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitawavumilia wanaharakati au kikundi chochote kinatakachohatarisha amani kwa kisingizio cha kupinga Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kutumia mihadhara na makongamano.Hayo yameelezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichomalizika juzi huko Chukwani Mjini hapa.
Balozi Seif alisema Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar haitaki kupoteza amani na utulivu na kurejea katika vurugu na uhasama uliojengeka katika jamii kwa maika kadhaa. Napenda niweke wazi msimamo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakivumilia kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi wetu” alisema Balozi Seif.Alisema serikali haiku tayari kurudishwa nyuma ambako wananchi waliishi kwa khofu kubwa huku chuki na uhasama zikiwa zimetanda miongoni mwao.
“Hatutasita kuvizuwia vikundi vyovyote vinavyoendesha mihadhara au makongamano tutakayobaini yanahataridha usalama wan chi yetu. Na hili hatutakuwa na muhali na mtu yeyote Yule” alisema Balozi Seif wakati wa kufunga baraza.Alisema kuna kikundi cha watu wachache wanaoendesha makongamano kwa lengo la kuwakashfu na kuwatukana viongozi, badala ya kutumia jukwaa hilo kwa shughuli za uelimishaji.
 Alisema lengo la serikali zote mbili ni kuona watu wanajitokeza katika tume iliyoundwa na Rais Kikwete kwenda kutoa maoni juu ya katiba na sio kutumia majukwaa kwa kuwapotosha watu na kupinga Muungano.Alisema masuala ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yana nafasi yake ya kujadiliwa na kwamba wanaotaka kufanya hivyo fursa hiyo wataipata kupitia mchakato ujao wa kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba.Alisema awali waliamini kwamba wanaoendesha makongamano hayo wana nia njema ya kutoa elimu kwa umma lakini badala yake wamekwua wakitumia makongamano na mihadhara hiyo kwa kuwakashifu viongozi, kejeli na matusi kwa viongozi na watu wenye kuunga mkono Muungano.
Kauli ya Makamu wa Pili wa Rais, imekuja wakati tayari wanaharakati wanaopinga Muungano na wanaotaka kuitishe kura ya maoni ya kuwauliza wazanzibari iwapo wanataka kuendelea na Muungano uliopo au hawautaki wamo katika mikono ya jeshi la polisi baada ya kushikiliwa hapo juzi katika viwanja vya baraza la wawakilishi.Wanaharakati hao 12 juzi walikamatwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kukataa kutii amri halali ya jeshi hilo mbele ya viwanja vya baraza hilo kabla ya kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ambaye walitaka kumuelezea lengo lao la kufika hapo.Kwa mujibu wa barua yao waliomuandikia Spika Kificho, na kutiwa saini na kiongozi wa kundi hilo, Rashid Salum Adiy ilisema wazanzibari wana haki ya kikatiba kudai uhuru wa Zanzibar na hivyo wanachotaka ni kuitetea nchi yao kwa mujibu wa sheria zilizopo ambapo.Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alikiri kwamba wanaharakati hao walipanga kumwona Spika kwa lengo la kushinikiza baraza lipitishe uzimio kuruhusu wazanzibari kupiga kura ya maoni ya kuukataa au kuukubali Muungano.
Kamishna Mussa alisema sio tatizo wananchi kudai haki hiyo ya kura ya maoni lakini kinachotakiwa ni kufuata taratibu na sheria za kuweza kufika katika viwanja hivyo vya baraza la wawakilishi na sio kwenda bila ya taratibu.“Sio shida wananchi kwenda pale lakini napenda watambue kwamba Baraza la Wawakilishi sio viwanja vya sikukuu, kama kila mtu anaweza kwenda tu na kusherehekea” alisema Kamishna huyo.
Alisema watub wanaweza kudai haki zao bila ya kuvunja sheria na jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na vitendo vyote viovu na vyenye kuhatarisha amani ya nchi.Aidha alisema wananchi wanaodai kuukataa Muungano wanaweza kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na wale wenye kuunga mkono Muungano pia wanaweza kufanya hivyo lakini kwa kufuata misingi ya sheria zilizopo na jeshi lake halitamvumilia mtu ambaye anakiuka sheria kwa kisingizio kama hicho.“Wanaopinga Muungano wanaweza kupinga lakini kwa kufuata taratibu maalumu na sheria na wale wenye kutaka Muungano pia wanaweza kuunga mkono lakini kama hatuwezi kuwaachia wneye kupinga kwa kusababisha fujo na hivyo hivyo hatuwezi kuwaruhusu wenye kuunga mkono kwa furaha zao wakenda uchi eti kwa sababu wanaunga mkono…lazima sheria na shuruti zitimizwe na sisi tupo hapa kwa ajili ya kuwashurutisha wale wasiotaka kufuata shuruti” alisema Kamishna Mussa.Uchunguzi wa Gazeti hili umegundua kwamba tayari wanaharakati hao wameshahojiwa na jeshi la polisi ambapo baadhi yao walikataa kutoa maelezo akiwemo kiongozi wa kundi hilo hadi hapo wakili wao atakapofika kituoni.

No comments:

Post a Comment