Monday, June 4, 2012

INTIMIDATION OF YOUR LEGAL RIGHT!!!! JESHI LA WAKURIA SASA LAPIGA MABOMU OFISI ZA WAKILI NCHINI ZANZIBAR


Rais wa Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Awadh Ali Said akiongea katika sherehe za kuadhimisha siku ya sheria duniani katika bustani ya Victoria

Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), kwa masikitiko makubwa, kinaomba kuwasilisha kwako malalamiko yetu kufuatia kitendo cha Polisi kupiga mabomu ofisi ya wakili ya AJM Solicitors iliopo Amani, Zanzibar. Jumatatu tarehe 28 Mei 2012 majira ya asubuhi katika Mahakama ya Mwanakwerekwe iliopo nje kidogo ya Manispaa ya Zanzibar, walifikishwa katika mahakama hizo watuhumiwa kadhaa kwa mashtaka mbalimbali yahusuyo uvunjifu wa amani. Hii ilikuja baada ya Jeshi la Polisi kuamua kumchukuwa kutoka msikitini Sheikh Mussa Juma Issa, Imam wa msikiti wa Kwa Biziredi majira ya saa 1.30 usiku wa Jumamosi 26 Mei 2012. Wafuasi wake walimfuata hadi polisi Madema alipowekwa ndani. Baada ya muda kupita na taarifa kuenea ndipo wananchi walipoanza kumiminika kituo cha Polisi, Madema wakisubiri kujua khatma ya kiongozi wao.
Watuhumiwa waliokamatwa Jumamosi tarehe 26 Mei na Jumapili tarehe 27 Mei 2012 walifikishwa mahakamani asubuhi ya tarehe 28 Mei 2012. Kama sote tunavyoelewa, ni msingi mkuu wa sheria zetu kwamba mtuhumiwa huwa hana hatia yoyote mpaka pale Mahakama itakapotamka hivyo baada ya kesi kuendeshwa kisheria. Na ni haki ya kikatiba kwa mshtakiwa kupata utetezi wa kisheria kutoka kwa watu wanaotambuliwa na sheria kuwa mawakili. Wakili Abdulla Juma Mohamed wa AJM Solicitors & Advocates Chambers ni wakili wa utetezi katika kesi ya Jinai inayotokana na MAD/PCR/45/2012 ya Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Janet Sekihola) na pia kwa kesi nyengine ya Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Mohamed Ali) inayotokana na MKD/PCR/05/2012 inayomkabili Mbarouk Said Khalfan na Mussa Juma Issa. Wakati watuhumiwa katika kesi ya kwanza wanashtakiwa kwa uzembe na ukorofi (kif. 181(d) Sheria ya Jinai 6/2004), kesi ya pili ni ya shtaka la mkusanyiko usio halali (kif. 55 na 56 Sheria Nam 6/2004).
Baada ya kesi tajwa hapo juu kuakhirishwa, Wakili Abdulla Juma aliondoka na kuelekea katika Mahakama ya Ardhi, Vuga Zanzibar. Majira ya saa 6.30 mchana ofisi yake ya uwakili iliopo karibu na Amani Roundabout, ilishambuliwa na Polisi ambao waliingiza mitutu ya bunduki ndani ya madirisha na kupiga mabomu ya machozi. Sisi tunaamini kabisa kwamba askari waliofanya hivi wamefanya wakijuwa kabisa kwamba kitendo chao kinakiuka maadili yote ya kazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora.
ZLS inalaani kwa nguvu zote kitendo cha Polisi cha kupiga mabomu ofisi ya wakili. Tunasema kitendo hiki kinalitoa thamani Jeshi la Polisi na kinaondosha imani ya wananchi kwao na pia kuharibu uhusiano wa karibu unaopaswa kujengwa baina ya raia na jeshi la polisi kupitia dhana ya “Polisi Shirikishi”. Sisi kama maofisa wa mahakama tunasikitishwa sana na hali hii na tunakutaka ufanye uchunguzi na watakaobanika kufanya kitendo hiki wachukuliwe hatua zifaazo. Tunaamini kwamba utendaji kazi wa Polisi hauendi kiholela – kila kikundi kinakuwa chini ya udhibiti na uangalizi wa Jeshi la Polisi kama taasisi. Hivyo hakutakuwa na ugumu wowote kumtambua askari aliefanya uhalifu huo. Vyenginevyo utatujengea imani kwamba kitendo hiki kina baraka zote za Jeshi la Polisi.
Wako katika kuheshimu Sheria za Nchi,
SIO BARAKA TU ZA POLISI BALI HATA RAISI MAANA YEYE AMEWASIFU ANASEMA WAMEFANYA KAZI NZURI YA KUZUI FUJO BASI NDIO WANAENDELEA HIVYO KUFANYA KAZI NZURI KWA RAISI.TUSIENDE MBALI MUNAKUBUWA WALIVYOULIWA WATU PEMBA JE NI JESHI AU POLISI YUPI ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA YALE MAUWAJI ZAIDI YA KUONGEZWA VYEO WAKURIA HAWA KISHA RAISI WETU ANASEMA WEMEFANYA KAZI NZURI SAWA KIYAMA PIA UMUAMBIYE M/MUNGU HAWA WAMEFANYA KAZI NZURI MIMI NILIPOKUWA RAISI WA ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment