Tuesday, June 26, 2012

MAALIM SEIF UMEMPONZA JUMBE KWA NYERERE NAONA SASA UNATAKA KUTUPONZA WAZANZIBAR KUENDELE KUTESWA NA MAKABURU WAUSI TANGANYIKA

JE DUWA ZA MAISARA ZANZA KUMUINGIA PIA MAALIM SEIF...???????????

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewahakikishia Wazanzibari kuwa hakuna mwananchi atakayeadhibiwa kwa kutoa maoni yake kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwapo atatoa maoni hayo kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
Amesema Tume iliyoundwa kwa ajili hiyo, itakuwa ikipokea maoni yote yatakayotolewa na wananchi, na kutoa wito kwa wananchi kutogomea utoaji wa maoni, na badala yake wajitokeze kwa wingi kuwasilisha maoni yao kwa kadri wanavyotaka mabadiliko hayo yafanywe.
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ametoa wito huo kwa nyakati tofauti alipokuwa akitembelea majimbo ya uchaguzi ya Chumbuni na Kwamtipura katika Wilaya ya Mjini Unguja kuangalia uhai wa Chama hicho, ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kutembelea majimbo mbali mbali Unguja na Pemba.
Amesema njia pekee ya kuondoa kero za Muungano ni kwa wananchi kujitokeza kutoa maoni yao mbele ya Tume ya kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba, na kwamba maoni yao yatazingatiwa, kuheshimiwa na kufanyiwa kazi kwa kadri watakavyoyatoa.
Amefahamisha kuwa wananchi watakuwa huru kutoa maoni yao, na kuwataka kuepuka jazba na kuvumiliana wakati wanapowasilisha maoni hayo, ili kuepusha malumbano yasiyokuwa ya lazima na ambayo hayatoisaidia nchi kwa njia yoyote, bali kuitia doa ambalo linaweza kuchukua muda mrefu kufutika.
Maalim Seif amewatahadharisha wananchi kuepuka vitendo vya vurugu na kuienzi amani iliyopo ambayo ni moja kati ya mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa serikali yenye mfumo wa umoja wa kitaifa

No comments:

Post a Comment