Thursday, June 28, 2012

MBUNGE KHATIBU SAID HAJI AJA JUU KWA KUITETE NCHI YETU YA ZANZIBAR


MBUNGE wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF), ametoa mpya bungeni baada ya kudai kuwa Zanzibar imegeuzwa mwanasesere.
Kutokana na hali hiyo, mbunge huyo aliwataka wabunge wote kutoka Zanzibar kutounga mkono Bajeti ya Waziri Mkuu mizengo pinda kama haitatengewa fedha za rada.
Akichangia mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake, mbunge huyo alisema serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kufanya sherehe za Muungano ambazo hazina matunda wala faida yoyote kwa Wazanzibari.
Alisema mambo mengi ambayo Wazanzibari wanataka kuyafanya huwa yanapigwa chenga na kudharauliwa kama mwanasesere na ndio mambo ya msingi na yamaendeleo kwa zanzibar na wazanzibari wenyewe lakini yanapingwa chenga sana na kupotezewa muda na fedha katika sherehe za muungano.
Alidai kuwa kwa muda mrefu Wazanzibari wamekuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) na kuondoa mafuta katika suala la Muungano lakini mambo hayo hayajafanyika, jambo alilosema kuwa ni kuwacheleweshea maendeleo wazanzibari.
“Hoja za msingi za Zanzibar huwa hazifanyiwi kazi lakini hoja zisizo za msingi zinapewa kipaumbele,” alisema.
“Sisi fedha za mfuko wa jimbo za kila mbunge zinatusaidia nini wala suala la malipo ya umeme. Nitawalipia bili Wazanzibari wote, lakini msikubali kupitisha bajeti ya waziri mkuu kama hawatatenga fedha za rada kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar,” alisema Haji.

No comments:

Post a Comment