Tuesday, July 10, 2012

MARAISI WATATU NCHINI ZANZIBAR WASHINDWA KUJENGA BARABARA NA SKULI JE NI MARAISI AU SAA TU ZA UKUTANI..?



WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameitaka serikali kuharakisha ujenzi wa barabara wa Mbuyu Tende Mkoa wa Kaskazini Unguja ambao upo katika hali mbaya ya kusababisha usumbufu mkubwa wa usafiri kwa wananchi.
Mwakilishi wa Jimbo la Mtemwe (CCM) Abdi Mosi Kombo na Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Kazija Khamis Kona walilalimika kwamba barabara ya Kijini – Mbuyu Tende inahitaji matengenezo ya haraka.
Akijibu suali hilo Naibu Waziri wa wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano, Issa Haji Ussi alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 48.7 ni miongoni mwa barabara zitakazofanyiwa upembuzi yakinifu na sadifu (Feasibility Study) ambayo itakuwa katika kiwango cha lami.
“Mheshimiwa Spika napenda kuliarifu baraza lako kwamba hatua ya mwanzo ya kutafuta kampuni za wahadhisi washauri imekamilika na kuwasilishwa kwa mfadhili wa mradi ADB ambaye amekubali kuendelea na hatua ya pili ya kumtafuta mhandisi mshauri” alisema Ussi.
Akivitaja vijiji vitakavyonufaika na baada ya ujenzi wa barabara hiyo kuwa ni Matembe- Muyuni (kilomita 6.5) Njia nne -Umbuji – Uroa (kilimita 11), Mkwajuni -Kijini (kilimita 5.5), Kichwele – Pangani (kilimita 4), Fuoni Kombeni (kilomita 6.7) na Jozani -Ukongoroni -Charawe (kilomita 15).
Naibu waziri alisem ajenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami utaanza mara moja baada ya kupatikana kwa fedha na kuahidi wajumbe kuwa serikali inaendelea na juhudi za kutafuta fedha hizo kutoka kwa wafadhili wa maendeleo.

No comments:

Post a Comment