Monday, July 23, 2012

SHEIN NA WEWE PIA UJIUZULU HUO UWAZIRI WAKO USIO KUWA NA WIZARA MAALUM

Inasikitisha sana kuona kuwa suala la kuzama kwa meli hii ya pili ambalo limepoteza watu zaidi ya 200, limechukuliwa kirahisi na serikali  hii ya mapinduzi daima na sasa inapinduwa tu maboti ikiuwa.
Kujiuzulu kwa Hamad siyo mwisho wa sakata la tukio hilo, pamoja na lile la kupigwa watu mabomu ya gesi wakiwa msikitini wakiwaombea marehemu dua kutokana na msiba huo. Siku ya Ijumaa ni siku tukufu kwa waislamu na ilikuwa ndiyo fursa ya mwanzo ya viongozi wa dini kuchukuwa nafasi ya kuwaombea dua waliokumbwa na janga ambalo ukiangalia kwa kina, uzembe wa serikali hii ya mapinduzi daima.
haikuwa jukumu la waziri peke yake bali ni jukumu la serikali yote pamoja na Baraza la Wawakilishi, ambalo limefikisha kuchangia bajeti za ofisi ya Sheini na za Seif Iddi na kuzipitisha bajeti zao bila kuuliza nini kimefanywa na serikali kuhusiana na fedha zilizochangwa kusaidia maafa Zanzibar, wakati meli ya Spice Islander ilipozama na bila hata ya kuona haya seif iddi ashaanza kupokea pesa za rambe rambe nyengine za mv skagit.Kama kweli wa semavyo kuwa wameunda serikali na uongozi bora au kama wanavyoita “Utawala Bora”, basi Dr. Sheini alivunje  Baraza lake la Mawaziri, Baraza la Wawakilisi na yeye Dr. Sheini mwenyewe pia AJIUZULU WADHIFA WAKE ALIYO PACHIKWA NA SEREKALI YA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA KISHA WAKAMFANYA KUWA WAZIRI HANA WIZARA MAALUM AJIUZULU HUO UWAZIRI WAKE USIO KUWA NA WIZARA MAALUM.
Tukio la kuwapiga mabomu wananchi katika ibada na Sheini akashindwa kutoa ufafanuzi, pia ni kitendo haki wezi kudharauliwa na wananchi, na hana budi kutoa maelezo na kujiuzulu mara moja. Matukio kama hayo: Kuzama kwa meli zaidi ya tano sasa na kupigwa watu mabomu misikitini wakiwa na lengo la kuwaombea dua marehemu, ni vitendo vya kikatili na halijawahi kutokea hata katika nchi za kikafiri kama Amerika na Ulaya.
TUNATAKA SHEINI AJIUZULU HARAKA KWA KUFUATA UTARATIBU KAMA ALIVYO FANYA WAZIRI MASOUD NA KISHA YASIMALIZIKIE HAPO ASUBIRI KUJIBU MASHTAKA MAHAKAMANI KWA NINI ANAWAPIGA MABOMU RAI WAKE WAKIWA KATIKA IBADA..? AJIBU SHTAKA HILO MAHAKAMANI.HILI LIWE FUNZO  KWA VIONGOZI WENGINE NA UTARATIBU WA UTAWALA BORA NA DIMOKRASI.
Wazanzibari wamechoka na dhulma zinazofanywa na viongozi wote wa serekali ya mapinduzi pamoja na raisi huyu wa kupachikwa ambaye ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum.

No comments:

Post a Comment