Tuesday, August 14, 2012

MAALIM ASEMA WAKTI UMEFIKI WA ZANZIBAR KURUDISHA KITI CHAKE UN


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuna haja kubwa ya Zanzibar kurejeshewa kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa wilaya na majimbo na wananchi kwa ujumla katika ukumbi wa Benjamin Mkapa, kisiwani Pemba jana.

Alisema Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa nchi huru iliyokuwa na kiti chake UN na sasa wakati umefika wa wazanzibari kurejeshewa kiti chao cha (UN) alielezea kuwa Zanzibar ikiwa na kiti chake maalum cha (UN)basi mamlaka kamili ya Zanzibar yatarudi  natutakuwa na nguvu umoja huo.ikiwa tutarejesha kiti chetu katika umoja huo.alisema maalim

Maalim Seif alisema hoja kubwa ambayo Wazanzibari wanatakiwa kujadili katika mchakato wa maoni ya Katiba mpya ni muundo na mfumo wa Muungano.

“Zanzibar tunayo Katiba yetu ya mwaka 1984 ambayo imejitosheleza kwa mambo yetu ya Zanzibar, lakini suala kubwa kwenye mabadiliko hayo kwetu sisi litakuwa ni la Muungano na hili haliwezi kuepukwa,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwataka wananchi kuangalia maslahi ya nchi yao kwanza katika mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba na kuacha tabia ya kutetea misimamo ya vyama badala ya maslahi ya nchi na wananchi wake.

“Katiba ya nchi ni mali ya wananchi siyo ya chama chochote, lakini najua kila chama kina katiba yake na hiyo ndiyo itabakia kuwa katiba na mwongozo wa chama husika, kwa hivyo ndugu zangu naomba tulifahamu hili na tuangalie maslahi ya nchi yetu kwanza,”zanzibar kwanza alisema Maalim na kupigiwa makofi na wanachama.

“Mimi najua wapo wanaotaka serikali moja, wengine mbili, tatu, nne, na wengine muungano wa mkataba, lakini wengine wanataka waachiwe wapumue…Yote hayo ni maoni na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila ya kulazimishwa, na nendeni mkatoe maoni hayo kwa uwazi,” alisema Maalim Seif.kumbukeni zanzibar kwanza.

No comments:

Post a Comment