Saturday, August 25, 2012

MASHEIKH WAKAMATWA TANGA-SENSA YAKIONA KIYAAMA MKOA WA SUMBAWANGA NA TANGA


IKIWA ndio siku ya sensa imewadia, bado hali si shwari Waislamu wakibaki na msimamo wakutokuhesabiwa.
Katika kukabiliana nahali hiyo, kumekuwa na kamatakamata wakiandamwa      wale wanaotuhumiwakusambaza vipeperushivinavyowakataza Waislamu kuhesabiwa     au       kuwashawishi      kwa namna yoyote.Habari kutoa mikoa,wilaya na vijiji mbalimbali,zinaonyesha kuwa badala yaserikali kutafuta namna yakutuliza mambo, imekuwa ikichukua hatua ambazo zinawafanya hata wale Waislamu ambao walikuwa hawana msimamo juu ya ususiaji huo, sasa waungane na wenzao.Habari kutoka Tanga zinafahamisha kuwa jana umati mkubwa wa Waislamu  ulifurika katika kituo cha Polisi Chumbageni kuju hatmaa ya masheik wao walio  kuwa    wamekamatwa wakidaiwa kuhamasisha watu kususia sensa.Waliokamatwa walikuwani Sheikh Chambuso, Ustadhi  Hamad Ayoub, Fadhil Chambo, Hussein Idd na Mwalimu Kassim Amar.“Mfumo kristo upo kazini,sheikh Chambuso na mwalimu Kassim Amar  wamekamatwa kwa   kuwaeleza Waislamu     wa    Tanga     vijijini    dhulma     iliyopo   nchini dhidi ya Waislamu.Wameshikiliwa katika kituo cha Polisi Mtandikeni, Duga Maforoni toka jana usiku wasaa tatu. Waislamu simameni  kuwahami Askari hawa wa Allah,Makamanda  wa            Mtume              (s.a.w). Fikisha ujumbe huu kwa  nduguzo Waislamu.”Ujumbe huu wa maneno ulioanza kusambaa jana saa nne usiku, ndio uliowavuta  mamia ya Waislamu jijini  Tanga leo asubuhi baada yakupata tarifa kuwa Masheikh hao walikuwa wameletwa Chumbageni.Hadi tukienda mitamboni ,Masheikh hao walikuwa wameachiwa na kusindikizwa na maandamano hadi Masjid Quba ambapo Waislamuwa likariri msimamo wao wakususia sensa.Katika maelezo yao walisema kuwa walimfahamisha wazi Mkuuwa Kituo cha Polisi kuwa si kweli kuwa serikali haina dini, bali dini ni ya serikali ipo na ndiyo hiyo ya watu ambao wao ndio wenyekusikilizwa, huku Waislamu
Na Mwandishi Wetu
wakipuuzwa, kubaguliwa nakudharauliwa.Kwa mtindo huo ndio maana Waislamu wameona serikali iendelee na hato wathamini katika zoezi hili la sensa.Kwa upande wa Wilayani Same, habari zinafahamishakuwa     Mratibu      wa     Sensa aliye   katika kituo cha Kisiwani‘amelikoroga’ baada ya kuwakosesha Walimu          kuswali          swala ya Idd.Habari zinasema kuwa ilitolewa maelekezo kuwa hakuna cha kuswali Idd, bali semina kwa walimu waliopangwa kuhesabu watu itaendelea kama kawaida wakati swala ya Iddi   inaendelea.Hata baada ya Walimu Waislamu kulalamika, bado Mratibu alisisitiza hakuna cha kuswali  Idd.Habari  zilizokuwa zimevujaHabari zilisema kuwa huo ulikuwa mkakati uliowekwa toka Wilayani kuwa wakikosa kuja katika       semina        hiyo       iwe       sababu   ya kuondolewa.Walimu hao walifika na kwa mshangao, Mratibu alipoita majina na kuona Waislamu wapo akasema hakuna semina watu warudi nyumbani  wakale Idd.Hata hivyo, wakati huo swala ilikuwa ishamalizika watu wanarejea kutoka misikitini. Mpasha habari wetu anafahamisha kuwa walimu Waislamu walikuja juu na wakataka kuwa maadhali wamekoseshwa swala, basi semina iendelee.Tukio hilo limewafanya Waislamu wengi kuona kuwa ni jama dhidi ya Waislamu hivi sasa gumzo idadi kubwa ya  Walimu Waislamu  mjini Same walioomba    kuwa   wahesabuji walivyo achwa na kuchukuliwa Wakristo watupu.Kwa upande mwingine inafahamishwa kuwa hali sishwari Sumbawanga   ambapofutari  iliyoandaliwa na Mkuuwa Mkoa ilidoda baada kususiwa    na Waislamu.Tukio hilo lilitanguliwa nalile la futari iliyoandaliwa na Katibu wa Tawi la Mkoa (RAS)16.Agosti.2012 ambapo  baadaya watu kumaliza maakuli,Mkuu wa Wilaya ya Nkasi alisimama na kuzungumza lakini akabaki akishangaa baada ya kujikuta akiachwa    pweke baada ya kundi la Waislamu kunyanyuka nakuondoka mara tu alipo anzakuzungumzia sensa.Habari za tukio hilo la Waislamu kugomea Sensa mbele ya mkuu wa wilaya na (RAS) katika hafla ya mwaliko    wafutari zilisamba kwa kasi na   kuwa mada ya Khutba za sala ya Ijumaa takriban Misikiti yote Sumbawanga mjini msisitizo ukiwa Waislamu kukataa kuhesabiwa.Khatibu       wa         Ijumaa        Msikiti     wa Qiblatain, Abdillah Salim Kanazawa, alielekeza Waislamu nini umuhimu wa Shura na nini madhara yaku    pinga Shura.Baadhi ya Maimamuakiwemo Imam Rajab waliwasisistiza Waislamu kuwa kinacho hitajika ni umoja nakupigania     haki        na heshima        ya      Uislamu         na Waislamu.Katika kuhakikisha wapo pamoja na wanasaidianakwa lolote litakalotokea,kumetolewa namba za simu kwamba mahali popote mtu atakapobughudhiwa kwa kukataa kuhesabiwa apige ili ipigwe Adhana katika Misikiti mbalimbali waislamu wakusanyike na kuamua lakufanya.Ilikuwa ni baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa naye akaandaa futari katika jitahada za kupoza mambo.Hata hivyo pamoja na kuandaliwa watu wa TV na magazeti, futari        ilidoda          baada   Waalikwa Waislamu walio      wengi          kususia         ya          kwa kujua kuwa agenda itakuwa sensa.Futari hiyo ilifanyika Agosti18, 2012.Katika   tukio   jingine   kutoka    Sumbawanga  Mjinii, mtoto mmoja wa chini ya miaka10 aliwaacha hoi wahesabuji  waliokuwa katika zoezi lamajaribio baada ya kukataakuhesabiwa na kusema kuwa  akihesabiwa atakuwa kafiri.“Baba kasema sisi waislamu hatuhesabiwi Baba kasema ambaye atahesabiwa atakuwa kafiri.”Alisema mtoto huyoaliyekutwa akiwa peke nyumbani na kutimua mbio akiwacha maofisa wa sensa

No comments:

Post a Comment