Friday, August 24, 2012

TUNAOMBA MUWASAIDIYA HAWA DUNGU ZETU KUTOWA NI MOYO SIO UTAJIRI


Asalamu Alaykum.
Naomba nilete hii makala muisome muone jinsi maradhi yanavyowatesa viumbe wa Mungu, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa mtoto anateseka anasikitisha na kuhuzunisha na huwezi kutupa jicho mara mbili kumtazama na umasikini umemsogeza hadi hapa alipofikia Subhanallah.
“Mama watoto Skuli wananiuliza mbona ngozi yangu ipo hivi” Ndivyo anavyoanza kusema Mtoto Nairat Khamis Ali alipokuja katika ofisi za Mwananchi Zanzibar kwa ajili ya mahojiano.
Nairat mwenye umri wa miaka 7 Mkaazi wa Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba amelazimika kukatisha masomo yake ya Nursery (Chekechea) kutokana na ugonjwa wa ngozi alioupata na kumsumbua kwa muda sasa akisumbuliwa tokea akiwa na miaka miwili.
Nairat ni mtoto mcheshi na mwenye kuongea sana ambapo matumaini yake ni makubwa ya kupata elimu na kuendelea kusoma lakini anasema ikiwa atapata nafuu ataendelea na masomo yake.
“Nataka mie kusoma lakini naumwa sasa hivi nikitibiwa na nikipona nitarudi zangu skuli na pia nilikuwa nasoma chuoni na najua kusoma Quraan lakini sasa hivi ndio nimekuja Unguja kwa kutafuta dawa” alisema Nairat huku akiwa ameinamisha uso mwake chini.
Unapomuona Nairat unajua kama ni mgonjwa na anasumbuliwa na maradhi ambayo bado hawajajua ufumbuzi wake wala dawa kutokana na kuwa kwanza ngozi yake imepiga weusi na imefanya mabaka lakini pia ukimuona machoni utaona vidonda ambavyo vimezunguka katika mdomo wake na katika macho ambapo tayari macho yake yameshaathirika na kuanza kupoteza nuru.
Pia Nairat mdomo wake umejaa vidonda na anashindwa kula kutokana maumivu na kuchonotwa anapotia chakula mdomoni na hivyo muda mwingi hukaa na njaa kwa kuogopa maumivu.
Kutokana na kuwa na vidonda ndani na nje ya mdomo wake, Mama Mzazi wa Nairat aitwaye Khadija Mohammed mwenye umri wa miaka 30 na mwenye watoto wanne anasema usiku kucha Nairat analia na kuugua kutokana na maumivu.
“Wallahi mwanangu usiku yuwalia tu kwa maumivu na hapo nyuma nilikuwa nikimpa dawa angalau akilala lakini dawa zimeniishia kwa kuwa sina pesa” alisema kwa masikitiko Bi Khadija ambaye ana watoto wawili wenye matatizo kama hayo na kuongeza kuwa.
“Kula hawezi kwani akitia chakula tu yuwalia asema aumia lakini maji ndio achwa sana”
Kwa mujibu wa Bi Khadija ambaye amefuatana na watoto wake wawili ambao wote ni wagonjwa amesema analazimika kununua dawa za kupunguza maumivu shilingi 70,000 na kumpatia mwanawe huyo dogo.
Mbali ya Nairat mtoto mwengine ni Bisambe (25) ambaye pia ana ugonjwa wa ngozi kama wa Nairat na anasumbuliwa na hivi sasa ameacha masomo kutokana na kuhangaikia matibabu na watoto wengine ni Yussra (5) na Abdul (2) ambapo wawili hao wadogo bado hawajaathirika na ugonjwa huo. Mwenyeenzi Mungu awaepushe na hao wengine awape tiba ya uhakika wapumzike na mateso wayapatayo inshallah.

KUTOWA NI MOYO SIO UTAJIRI TUNAWAOMBA MUWASAIDI HAWA NI DUNGU ZETU HAPA ZANZIBAR. WAO WANATESEKA NA MARADHI HAWANA HATA SHILLINGI YA KUNUNULIA DAWA.DUNGU WOTE WA ZANZIBAR MULIO HAPA ZANZBAR NA MULIO NJE YA ZANZIBAR TUNAWAOMBA MUWASAIDIYE. ILA SHEIN,MAALIM,BALOZI IDDI PESA ZAKUTEMBELEA MIKOA NA VIJIJINI KWENDA KUTIA FITINA MUNAZO NA HUKU WANANCHI WANATESEKA KAMA HIVI MARAISI WATATU NDANI YA NCHI MTOTO HUYU SI WAKUTESEKA ILA NYINYI SIO MARAISI NYINYI NI MAJINA MIZI ILA M/MUNGU ANAWAONA NA ATAKWENDA KUWASIMAMISHA INSHAA ALLAH SIKU YA KIYAMA MUELEZE UZURI FITNA NA KUJIFAHARISHA KWENU HUKU WANCHI WAKITESEKA.
HAWA NDIO WATU WA KARIBU WAKUWAPA
HUWO MSAADA ILI UWAFIKIA HAWA DUNGU ZETU
KUTOWA NI MOYO SIO UTAJIRI INSHAA ALLAH KHERI
Salma Said,
P. O. Box 1442,
Tel: +255 (024) 223 5219
Mobile: +255 777 477 101
E-mail: muftiiy@yahoo.com

Hassan Mussa Khamis
Mobile: +44 7588550153
email: hassan.mussa@gmail.com
United Kingdom

No comments:

Post a Comment