Saturday, September 29, 2012

UAMSHO YAWAELEZA VIONGOZI WA ZANZIBAR SABABU YA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR

waislamu na waznzibar kote nchini wametakiwa kufuata mfumo aliouweka Allah kwa waja wake kwa lengo la kupata mafanikio mema hapa duniani na kujiepusha na adhabu huko akhera




wito huo umetolewa leo na shekh Khalfan Nassor katika mhadhara uliofanyika katika viwanja vya masjid salami magogon wilaya ya maghrib unguja. Aidha amewasihi viongozi walioko madarakan kutumia madaraka yao kwa uadilifu na kulinda haki za wale wanaowaongoza na kusisitiza kuwa mashehe hawana nia ya kuwaondosha madarakani katika nyadhifa zao bali ni jukumu lao kufikisha ujumbe wa allah kwa waumin wote wakiwemo na viongozi.



kwa upande wake amir wa jumuiya na taasisi za kiislamu hapa nchini shekh Mselem bin Ally amesema suala la kudai hadhi na maslahi ya zanzibar kuwa huru sio jambo rahisi na kuwa linahitaji ustahmilivu mkubwa, hata hivyo amewataka vijana kuwa makini juu ya kile alichokiita kuwepo kwa njama za kuvuruga harakati zao za kudai uhuru wa nchi ya zanzibar zinazofanywa na wasioitakia mema nchi ya  zanzibar.



Akibaanisha sababu ya mashehe kushiriki katika kudai uhuru wa nchi ya zanzibar ni kuwasaidia viongozi wenye uchungu na nchi yao kwani wanaonekana kukosa nguvu na ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi katika serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar, hivyo amesema hata zile sababu za kuanza kwa upinzani wa vyama zanzibar kulikua ni ile ile kuitakia mema nchi, kutokana na kushindikana kwa wanasiasa wakuitetea zanzibar ndio maana wananchi wenyewe wameamua kufanya jitihada na juhudi za kuikomboa nchi yao ya zanzibar.

No comments:

Post a Comment