Monday, October 15, 2012

MTOTO WA KIKIRISTO IKOJOLEA QURAAN NA KULINDWA NA JESHI LA POLISI NCHINI TANGANYIKA.


WAKATI idadi ya makanisa yaliyochomwa moto kutokana na mtoto wa kikiristo kukojolea kitabu kitukufu cha Quraan  jana Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam ikifikia saba sasa, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo wameonya kuwa, Serikali ikishindwa kudhibiti matukio ya vurugu za kidini, taifa linaweza kuingia katika umwagaji damu viongozi hao walionyeshe kuitisha serekali.
Vurugu hizo zilitokea juzi baada ya waislamu wa dini ya Kiislamu kujaa katika Kituo cha Polisi, wakitaka wapewe mtoto aliyedaiwa kudhalilisha kitabu kitakatifu cha Quran kwa kukikojolea.
Akizungumzia habari hizo jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa, watu 122 wamekamatwa wakihusishwa na vurugu hizo na 36 kati yao wanahusishwa na uchomaji wa makanisa kwa kukasirishwa kwa kuthalilishiwa kitabu chao cha Quraan kukojolewa na mtoto huyu. “Tumekamata watu 122, kati ya hao 86 walikamatwa kwa kosa la kufanya fujo na wengine 36 tunawashikilia kwa kosa la kuchoma makanisa,”alisema Kamanda Kova.
Wakizungumzia vurugu hizo, baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Kikristo nchini wametishia kuwa matukio ya aina hiyo yakiachwa yaendelee, umwagaji wa damu unaweza kulikumba taifa.
Pia waliwataka wananchi kuheshimu mawazo ya wengine na kutochukulia jambo lolote kwa hasira.Kauli za viongozi hao zimekuja siku moja baada ya viongozi mbalimbali wa Serikali na Baraza la Wanafiki Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam kulaani tukio hilo wakieleza limefanywa kwa jazba na kwamba halitakiwi kufanyika tena nchini.
Kamanda Kova  alifahamisha kuwa katika Kanisa la TAG lililopo Mbagala Kizuiani, gari moja la mchungaji lilichomwa moto na mengine saba yaliyokuwa yameegeshwa eneo hilo yalivunjwa vioo.
Aliongeza kuwa magari matano ya polisi yaliharibiwa kwa kuvunjwa vioo katika vurugu hizo.
Kova aliyataja makanisa yaliyoharibiwa kutokana na vurugu hizo kuwa ni Kanisa la Agape lililopo Kibonde Maji, Kanisa la Wasabato, Mbagala Kizuiani.
Kova aliyataja makanisa mengine yaliyoharibiwa kuwa ni Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme, Mbagala Rangi Tatu ambako walivunja vioo na kuharibu madhabahu na Kanisa la Anglikana Mbagala Kizuiani lililoharibiwa madhabahu, ambayo thamani yake bado haijajulikana.
Mengine ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbagala na Kanisa la TAG Shimo la Mchanga.
Katika makanisa hayo mawili waliharibu milango na kuchoma nyumba ya Mwekahazina wa kanisa pamoja na nguo za kichungaji zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Kamanda Kova alifafanua kuwa hadi jana walikuwa wakiendelea na msako wa kuwabaini watu wengine waliohusika na tukio hilo, akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zilizo sahihi.
Kova alisema mtoto anayetuhumiwa kwa kuikojolea na kudhalilisha Quran hiyo, ambaye hadi sasa anashikiliwa na polisi, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia umri wake.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati polisi wakifanya uchunguzi wa kina.

No comments:

Post a Comment