Wednesday, December 26, 2012

FATHER AMBROS AJERUHIWA KWA RISASI KWA MAKUSUDI ILI MAKANISA YAPEWE ULIZI ZAIDI NA SMZ NCHINI ZANZIBAR



Watu wasiojulikana leo wamemjeruhi kwa risasi Father, Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae Nchini Zanzibar nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amejeruhiwa kwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.
Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.
“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.
Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumjeruhi kwa risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kujeruhiwa kwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.
“Kamanda Azizi pia alisema Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini lakini tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu na pia hatuna vipeperushi vya aina yoyote vinavyoelezea kuwatisha viongozi wa dini kwa hivyo tunachukulia hayo ni matukio ya kihalifu na wala hatuamini kwamba matukio haya ni ya dini fulani” alisema Kamanda Azizi.
Akielezea kuhusiana na hilo Kamanda Aziz alisema jeshi la polisi limejipanga na kuzidisha ulinzi katika maeneo yote ya makanisa ambapo kumesambazwa polisi wa kutosha kwa kuwa wanajua wakati wa sherehe mambo ya kihalifu hujitokeza.
“Sisi kawaida huwa tunaweka ulinzi siku za sherehe zozote lakini ulinzi upo wa kutosha” alisisitiza Kamanda Aziz. kwamba makanisa yote yamewekewa ulinzi wa kutosha kabisa ila wahalifu wanajuwa mbinu gani na saa ngapi na watafanya uhalifu huo wapi,  lakini wahalifu wanapotaka kufanya uhalifu huwezi kujua wataufanya wapi mpaka waufanye.

No comments:

Post a Comment