Thursday, January 10, 2013

DIKTETA MAZRUWI ASEMA KARUFU ZIUZIWE ZSTC ASIYETAKA KARAFU ZAKE ZITAIFISHWE AKIKAIDI APINGWE RISASI .


ALISEMA MCHELE WA MAPEBMBE BASI ZANZIBAR KUMBE DOMO TU LA KUTAKA MADARAKA NA KUTAKA KUWANYONYO WAZANZIBARI NA KARAFU ZAO.


Moja ya ‘milestone’ waliyokuwa wanaringia sana GNU ni kupandisha bei ya karafuu. Na wananchi wa Zanzibar na hasa Pemba ambalo zao la karafuu linazaliwa kwa wingi, walikuwa wakipiga vigelele kwa furaha.
Kwa kiasi kikubwa, bei mpya iliwakomboa wananchi wa Zanzibar; na hali ya umasikini kidogo ilipungua, makali ya maisha yalipungua; ingawa bei za bidhaa muhumi ilizidi kupanda.
Hali imebadilika, na bei ya karafuu imekuwa haijulikani iko juu au iko chini katika soko la duni [sina takwimu sahihi, anayejua atupatie data hizo muhumi, bei ya karafuu katika global market].
Kwa vile serekali haitaka kusema ukweli kwa wakulima ni bei ngani wao wanauza huko nje, wakulima na wachuuzi wa zao hilo, wamekuwa wagumu kuiuzia serikali (ZSTC), na wametafuta mbadala wake ‘wanaujua wenyewe’.
Sasa imekuwa balaa, Waziri Wa Biashara, Mstahik Nassor Mazrui anasema ‘lazima wakulima wauze karafuu zao ZSTC, na wasiotaka kutii amri hiyo ama wakamatwe, au karafu zao zitaifishwe, na kuamrisha vikosi vya vya SMZ viwe ‘vigilant’ wawasakame, na wawakamate na kuwachukulia hatua za kisheria’. Very authoritarian language — na lugha za kibabe, jeuri za kiutawala.
Kutokana na ‘fatwa; hiyo ya dikteta huyu mpya wa karafu za zanzibar Mazrui, matukio mengi mabaya yameaanza kujitokeza hasa Pemba, kukamatwa watu bure bure, hasa maeneo ya mwambao wa bahari,KMKM kuwatupiana risasi  wenye vyombo vya baharini kama vile ngarawa, mashua, jahazi n.k.bila ya kuwa na uhakika kama wamebeba karafu au laa wao wanafyatuwa tu.
Inasikitisha kusikia na kuona amri kama hizi anazitoa mtu kama Mazrui, mtu /mfanyabiashara, mwenye asili yeye, babu zake, wazee wake wote wamekulia na kutokana na bishara ya karafuu, anaijua A-Z kama dr.Shein anavyoijua hosp ya Mnazi Mmoja na kuiwacha ikinuka na iko ubavuni kwake kwenye ikulu na wala hajali inanuka — dam dam.
Mazrui na Mohammed Aboud (super boy) wanaijua biashara ya karafuu kama majina yao — mmoja wa Mkanjuni akitokea kwenye asili Mitamani, mwengine wa Wara (wawi).
* Mazrui anaijua vizuri sana karafuu ni nini – enzi zile wakulima wakipewa majamvi, kapu na magunia bure – leo zinaanikwa chini,kwenye mchanga na mavumbi magunia ni mapolo ya mapembe (recycable…..?). Leo yapo wapi hayo, wakulima wanaumia na mtutu wa bunduki unawasubiri.
Kama mantik ya Mazrui ni hiyo, kuwa lazima tutumie MTUTU wa BUNDUKI kwa kila national program, kwa kila kitu katika maisha yetu — kuanzia kuandika sensa bunduki, kuandika kura na kupiga kura bunduki, kuandikisha National ID bunduki, kutoa maoni ya katiba bunduki — yote haya lazima UTUMIKE MTUTU WA BUNDUKI  ndio tunakwenda. Kweli tutapiga hatua kiasi gani katika nchi hii ya zanzibar...?
Mimi natoa challenge kwa Mazrui kama kweli bingwa, kwa nini haingilii kupandishwa kwa bei ya bidhaa muhimu hapa Zanzibar — mchele, sukari, unga wa ngano n.k hizi bidhaa zinapanda kila siku kama vile unavyoona shares zinavyoshuka na kupanda pale New York Stock Exchange. Hakuna jutification ya kupanda bidhaa kiasi hicho — kisingizio ‘dola imepanda, dola imeshuka’.yagujuuuu
Pili, kama yeye hodari sana — mpaka leo Zanzibar tunakula low quality mchele wa mapembe, na yeye alisema ‘mapembe yatakuwa basiiiiiii’ naona ndio kwanza yamezidi.
Juzi tu bandarini umekamatwa mchele tani 45 wote mbovu, unga tani zaidi ya 50 wote mbovu. Haya yamemshinda, lakini kuwahilikisha jamaa zetu, wakulima wa karafuu anaweza kuamrisha vikosi vya SMZ iwatandike bakora sawa sawa je kunatauti ngani wakati wa JOHN OKELLO 1964 na sasa ikiwa miaka hiyo ni bakora na mtutu na sasa bakora na mtutu je tafauti iko wapi.....?
Jamani kuongoza sio kutumia mtutu wa bunduki, ni busara zaidi – inatakiwa ujue source ya tatizo, na kulitatua katika misingi ya busara ya umahiri zaidi. Sisi kila kitu MTUTU WA BUNDUKI, mara moja hata chanjo za watoto vikosi vya SMZ vilikuwa vinapita kila nyumba kulazimisha watoto wachanjwe, dawa ya kuulia mbu, pia ilikuwa vikosi vya SMZ vinalazimisha lazima upigiwe dawa. AKILI ZETU ZIMEFUNGIKA HAPO, KUWA MTUTU WA BUNDUKI NDIO SULUHISHO, basi hata kupigiwa dawa ya mbu, au chanjo.
Mimi naona kama SMZ ni jidikteta lisilo jali wananchi wake kabisa, tumewafanya wananchi/raia wamekuwa sugu sana kiasi ambacho kimezaliwa kitu ‘lawlessness’ katika jamii zetu. Imezaa usugu wa watawaliwa (wananchi) na usugu wa watawala — kuwa wao ndio wao tu, ambayo huzaa jeuri na kiburi cha utawala ila kila lenya mwanzo lina mwisho iko siku SMZ ITAKUWA WATU HATA HAWAIJUWI NI NINI ITAONDOKA KAMA ALIVYO ONDOKA GADDAF NA WENGINE IKO SIKU YENU.

No comments:

Post a Comment