Friday, January 25, 2013

HILI NDIO BARAZA LETU LA WAWAKILISHI KAZI KUCHEZA MDUWARA,SUMSUMIA NA KANGA MOKO SIO KUTETEA WANANCHI NA NCHI YA ZA,BAR LAAA



Wazanzibari tujiulize kwa pamoja kitu gani ambacho baraza la wawakilishi  wanashindwe kuchukua maamuzi magumu katika kulinda, kusimamia, mustakbali na maslahi ya nchi na wananchi  wa Zanzibar....?Hatuoni kwmba baraza  hili limekosa ridhaa na uaminifu kwa wananchi..? Jee baraza hili kwanini linashindwa kulinda mali za nchi..?Sababu kuu za 
kuanza kujiuliza haya masuala (3)
Baraza limesikia kilio cha wananchi wa visiwa vya unguja na pemba kwamba Muungano huu hawautaki wa kikatiba wa miaka 49 wamechoka nao ni nusu karne na hakuna moja lililo nufaisha Wazanzibari.Wanataka muungano wa mkataba wenye kuheshimiana, wenye maslahi kwa pande zote mbili zilizoungana, Wanataka kila taifa liendeshe shughuli zake za ndani na kimataifa yani nje bila kuingiliana katika uendeshaji wa kazi za serikali hizi mbili.
Wanataka kila taifa liwe huru katika kujiamulia mambo yake wenyewe, isiwe tukitaka kwenda kununuwa omo kenya lazima tukaulize dodoma je tukanunuwe omo ....? laaa tunaka kununuwa tunanuwa tu. haya ndio maoni yaliokushanywa na chombo cha kisheria kilichopitishwa na bunge la Jamhuri ya Tanganyika na pia kuungwa na kupata baraka za baraza la wawakilishi(tume ya jaji Warioba) Jee kwanini baraza la wawakilishi haliitishi kura ya maoni kumalizia pale ambapo wananchi walishapaanza..? au nyote humu ndani ni majibwa koko....?
Tujiulize tena nini baraza hili wanasubiri..? hakuna haja ya kusubiri na kuendelea na huu mchakato wa katiba ikiwa mshiriki mmoja wa muungano amesema kwa asilimia 67 % kwamba anataka muungano wa mkataba Inaonekana baraza hili la wawakilishi halina mamlaka yoyote ya kusimamia haki na maamuzi ya wananchi wa Zanzibar limekuwa ni kama banda la kucheza karata na bao la kete. Baraza linaendeshwa kwa nguvu za DODOMA  ambacho chama kinanguvu kuliko chombo kilichochaguliwa ama kihalali au kwa mizengwe.
Tunaliambia baraza la wawakilishi liitishe kura ya maoni au waitishe kikao cha dharura kujadili maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya sio kusubiri mpaka wakoloni tanganyika waje na msaada wa kupinga kikao chochote kile cha kujadili matokeo ya maoni ya wananchi kuhusiana na hii katiba mpya naikiwa bara latishindwa kufanya hivyo basi Wazanzibari tusisubiri tena maana misra mubaraka hakuondolewa na baraza kaondolewa na vijana barabrani niwakati wa kujitolea na kujuwa ima ya mussa au ya firauni tu sasa masheikh walio kuwa wakisema kweli washawafunga jela na sisi ndio tu kae tu kama mayatima mpaka lini au ndio tuishi hivi hivi mpaka miaka mingine 49 imelizike....?
Hii ni wake up call kwa baraza linalojulikana baraza la kuwatetea Wazanzibari katika hali yoyote, tunataka kuona hii mitumbo iliyo jazana humu kufanya kazi zake sio kusinzia tu,na kupiga kelele kwamba Tangnyika wanatunyonya wakati uwezo wa kuondoa unyonyaji munao lakini hamufanyi.Tunakuambiyeni wajumbe mitumbo mikubwa na vicha vya samaki tumieni nguvu zenu za kikatiba kuitisha kura ya maoni kuhusiana na huu muungano feki. Kama baraza hili lina nguvu kisheria na haliingiliwi katika maamuzi yake na chombo chochote kile basi wakati umefika kwa kusikia kauli za wajumbe hawa ikiwa ccm au cuf, wakati umefika laaa kama nyote humu ndani ni vipusa kazi kutia hina na piko na kujiremba na maskara huku mukiweka viluwa na asimini katika kitanda ili bwana wenu tanganyika akija afurahi na kuwa kuna kuna nyinyi basi sawa nyamazeni maana ndio bwana wenu sio.
Tumemsikia Mh. Amani Abeid Karume anasema kwamba yuko teyari kusimamia Serikali katika kipindi cha kuandaa Muungano wa mkataba ikiwa dr kumbi shein aliye wekwa na dodoma madarakani atakuwa hajiamini na hana uwezo wa kusimamia Serikali kwa kipindi hicho cha mpito. Jee kwanini hamuchukui maamuzi magumu kumalizia pale ambapo wananchi na viongozi wengine wamekufikishieni...? Waswahili husema kwenye miti hakuna wajenzi, usemi huu unakubalika hakuna mwenye hoja ya msingi kuupinga Wawakilishi tunakuambiyeni muchukue maamuzi magumu kama mupo katika hicho chombo kwa ajili ya maslahi ya nchi na wananchi wa visiwa hivi vya unguja na pemba au nchi hii ya Zanzibar.” La leo lifanyike leo, Wananchi wanakufa na njaa, maradhi, ukosefu wa elimu, miundombinu, uhusiano wa kimataifa, uchumi na sarafu” Marehemu Mzee Karume alisema koti likikubana…..livuwe mambo 11 yaliokubaliwa katika muungno sasa ni mambo48 na toka tungane nao sasa ni miaka 49 inamanisha kila mwaka wameongeza moja na kulifanyia kazi vizuri ili watuangamize wajube bado tu hamja amkaa..?
Huku koti likizidi kupanuliwa na Watanganyika, kwenu linabana kwao wanalipanua na yao yanawaendea vizuri sisi tumo tu muungano weeee katiba weee muungano weee katiba weee. Nakuambiyeni wachangiaji muwaulize wajumbe hawa wa baraza la wawakilishi wanasubiri nini, au hawana uwezo, wanaogopa tanganyika asije akawaekea vikwazo vya kiuchumi....? ikiwambia kuanzia sasa hatuwaletei tena BATATA NA MAHARAGE NA VITUNGU HAHAHAHAHAHA

No comments:

Post a Comment