Monday, January 21, 2013

MASULTANI WA KITANGANYIKA WALIO ITAWALA ZANZIBAR KIMABAVU KWA NUSU KARNE SASA NDIO HAWA.


MASULTANI WA KITANGANYIKA WALIO ITAWALA ZANZIBAR KIMABAVU KWA NUSU KARNE NDIO HAWA.                  HAWA NDIO WATUMWA WA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA-Sheni, Bilali, Nahodha, Suluhu, Khatibu, Sefu(2), Kificho, Vuai, Mwinyihaji, Aboud.


Serikali ya Muungano wa Tanzania imejipanga vyema kuona ifikapo mwaka kesho Tanzania inapata katiba  mpya itakayowaongaza Watanzania wote.Tanzania kimantiki ni Muungano wa Nchi mbili zilizokuwa huru hapo awali ambazo ziliamua kuungana pamoja kwa maslahi ya Wananchi wake na kuzaliwa Taifa jipya ambalo leo hii linajulikana kama Jamhuri ya Watu wa Tanzania.
Inawezekana kabisa kwamba Waasisi wa Muungano huu ambao ni wawaili kama mboni ya macho, mmoja kati yao ama kwa kukusudia au bahati mbaya inawezekana hakuwa na nia safi na mshirika mwenzake. Hii ndio sababu hadi hii leo bado Watanzania na hasa Wazanzibar wananyanyasika katika Muungano huu ambao leo hii unatimia karibuni nusu karne huku ukigubikwa na matatizo kadhaa wa kadhaa kwa Washirika walioungana.
Ukweli kuhusu Muungano huu ni kwamba hauwezi kufichika tena kwa kutumia nguvu za dola na wakati mwengine kupoteza maisha ya Wazanzibar kila pale mtu au kikundi cha Watu wanapohoji uhalali wa kuwepo kwa Muungano huu.Muungano huu tokea kuasisiwa kwake imekuwa ni majanga na vilio kwa Wazanzibar ambavyo havina mnyamazishaji,ila yeyote anaesikitika na kuomboleza basi hukiona cha mtema kuni.
Asilimia kubwa ya Wazanzibar hawana imani wala shida ya kuwa na Muungano huu kwani faida zake ni chache kuliko madhara yake,kwa lugha nyepesi niseme kwamba Wazanzibar walio wengi hawautaki Muungano huu.Kinachoendelea kwa sasa ni bwana kumlazimisha mbuzi kunywa maji mtoni bila hiari yake mwenyewe jambo ambalo sioni kama litawezekana na kuwa na mwisho mwema.
Ni kweli kwamba kuna baadhi ya Wazanzibar wanautaka Muungano huu uendelee kama ulivyo,lakini hawa ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na matakwa ya walio wengi hapa Zanzibar.Kikundi hichi ni wale watu waliopandikizwa tokea kuasisiwa kwa Muungano huu yaani kiasili ni kutoka Tanganyika na waliletwa Zanzibar kwa kazi maalum ambayo leo hii wamefanikiwa kuifanya na kuifanya Zanzibar kuwa mtoto wa kambu na kaa la moto kwa wenyeji wake.
Kundi la pili lenye msimamo wa kutaka Muungano huu uendelee ni Viongozi wa chama Tawala ambao njaa zao zinawasumbua sana na kupenda sana  kwao ul-wa bila kujali maslahi ya Nchi na Wananchi wake. Kundi hili ni Vigogo ndani ya Serikali ambao kupata kwao dhamana hiyo wanategemea Serikali ya Muungano na ndio maana ukaona Viongozi wa Serikali ya Zanzibar hawana maamuzi ya aina yeyote yale isipokuwa wanafuata amri na maelekezo kutoka kwa Watawala wao yaani Tanganyika.
Upande mwengine kuna wale wanajipendekeza ili waonekane watendaji wazuri na Watiifu kwa Tanganyika lengo hapa ni kupata maslahi binafsi,bila kujitambua kwamba wanauza utu wao pamoja na jamii yao kwa maslahi duni. Maslahi ambayo kiongozi wa Kizanzibar anashindwa hata kumsaidia mwanawe aliemzaa sikwambii umma unaotaka kuongozwa kama Taifa.
Pia kuna kikundi chengine ambacho kila kukicha huimba na kuutukuza Muungano huu kama vile lulu na almasi, kwa kusema Muungano una faida kubwa kwa kujinasibisha kwao kwamba wameoa au kuolewa lakini pia wengine wamenunua vijishamba na kuekeza vijumba vyao hapo Tanganyika, hawa wako tayari hata Zanzibar itoweke lakini wakinge mali zao na maslahi yao tu,huku wakijua fika kwamba Tanganyika inaikalia Zanzibar kimabavu na kuinyonya rasilimali zake.
Hivi sasa Wazanzibar wameshachoka na madhila haya ,ila Watanganyika kwa kukinga maslahi yao  wanazidi kutafuta mbinu nzuri zaidi za kuwamiliki na kuwatawala Wazanzibar wanatumia mbinu mbali mbali ili ionekane kwamba Zanzibar inafaidika na Muungano uliopo. Serikali ya Tanganyika hivi sasa imekuja na  janja nyengine mpya ya KATIBA MPYA,hapa ndipo Wazanzibar na Zanzibar itakapomalizika,kwani hivi sasa inatuta lakini pigo hili ni la mwisho kuelekea kudhimu.
Katiba hii mpya haina faida wala lengo la kuwakomboa Wazanzibar isipokuwa kuwachimbia kaburi la moto wasitoke tena humo ndani kwa kuwapa Wazanzibar matumaini ya pepo huku wakijua fika kwamba hawakusilimu na  wala hawakuamini Mola mmoja,jee hiyo pepo walio ahidiwa na Tanganyika itapatikana vipi ?. Muundo wote wa Tume hii na Viongozi wake ni wale wale Vibaraka ambao siku za nyuma walikuwa wanamsujudia na kuabudu kauli na maneno ya Mwalimu Nyerere . Sasa ikiwa Tume ya katiba hao ndio Viongozi wake Wazanzibar wanategemea nini katika kupata haki yao kama Nchi huru ? Tunajidanganya au tunadanganywa!!!!!
FAIDA YA MAPINDUZI DAIMA NA MUUNGANO FEKI NDIO HII NUSU KARNE NCHI INANUKA KAMA KIDONDA HAKUNA LINALO KUWA ZAIDI YA WATU KUZIDI KUWA MASIKINI.

No comments:

Post a Comment