Thursday, January 24, 2013

SHEHIA YA KENGEJA PEMBA WALIA NA SKULI YAO.HIZI NDIO TIJA ALIZOZITAJA BILALI NA FAIDA ZA MUUNGANO HUU


TIJA NA FAIDA ZA MUUNGANO HUU FEKI ANAO USIFU BILALI KUWA UNAMANUFA

Wananchi wa Shehia ya  Kengeja Mkoa wa kusini Pemba walia na ujenzi wa skuli yao nikizungumzia kengeja nadhani miongoni mwenu  wengi mnaweza kupafahamu au kutokupafahamu.
Kijiji cha kengeja kipo mkoa wa kusini Pemba na nimiongoni mwa kijiji maarufu hapo zamani kwa upikaji wa Tosi pia kuwa na wakaazi wengi sana wa kihindi ndani ya kengeja kuna Skuli iliojengwa mnano mwaka 1945 mpaka leo hii ndio inayotumika kwa ajili ya kutowa elimu kwa wananfunzi mbali mbali.
Hapo mwanzo kabla ya Kuja kwa mapinduzi ilitoa elimu kwa wakaazi wengi wa maeneo jirani kama Vile Mwambe,Mtambile,Kiwani na maeneo mengien ya karibu licha ya kuwa katika maeneo mengi sana ya Unguja na  Pemba kwa sasa kumekuwa kukijengwa skuli mpya siku hadi siku lakini cha kushangaza na cha ajabu kwa skuli hii hadi leo hii  imebaki kuwa na majengo yale yale ya zamani ya 1945 na wanafunzi ndio wanayosomea ingawa hayafai hata kidogo kwa sasa kulinganisha na hadhi yake.
Kitu ambacho ukweli kimnifanya nishindwe kuvumilia sasa kwa vile mimi pia ni miongoni mwa wazaliwa wa kijiji hichi na nimewahi kusoma katika skulii hii ni kwamba wananchi wenyewe wa kengeja wamekuwa akihangaika sana kuhusu suala lakutafuta msaada wa hali na mali ili waweze kujenga skuli yao lakini jitihada hizo ni sawa na kugonga ukuta  kutokana na  kutokuzaa mafanikio yoyote kwao.
Ingawa kuna msemo usemao abebwae hujikaza ndio maana wananchi wenyewe kwa nguvu zao huku wakijawa na imani kuwa baada ya jitihada zao wangeweza kusaidiwa na ndio maana hadi hivi sasa wameweza kuchangia kiasi cha shilingi takribani milioni nane wakisubiri kupatiwa msaada zaidi ili wafanikishe lengo lao la kuwa na skuli mpya na wao kwa faida ya watoto wao au hata kufanyiwa ukarabati lakini hali mpaka sasa bado imebaki kuwa giza sijui ni kwamba hakuna tena wafadhili ambao husaidia ujenzi wa skuli mbali mbali hapa Zanzibar kama zilivoweza kusaidiwe nyengine nyingi za kisiwani Pemba.
Ni suali la kujiuliza hivi hawa wanaotowa misaada ya ujenzi wa mashule wanavigenzo gani ambavyo huzingatia ili waweze kutoa msaada wao pengine sisi hatuna  na tusiweze kusaidiwa hadi leo hii,ukweli inauma sana kuwona takribani skuli nyingi za unguja na pemba kwa sasa zikiwa na mazingira mazur ya kusomea lakini kwa skuli hii hali nikinyume na skuli nyengine ambazo zinaendelea kukarabatiwa pia kujengwa mpya siku hadi siku.
Ni ukweli usiofichika kuona wananchi wakijitahidi kuchaguwa viongozi huku wakiwa na matumaini kuwa watawasaidia katika kuhakikisha kuwa wanapiga hatuwa kimaendeleo ndani ya sehemu zao  lakini wapi sijawahi kusikia kuwa kuna mtu alieweza kufika na kusaidia alau msaada ambao utaisidia katika suala zima la ujengwaji wa skuli hio.
Siwezi kuondoa shukrani zangu kwa mwakilishi wa jimbo la Mtambile ambae pia ni mkaazi wa Kengeja yeye ukweli amejitahidi ni hivi karibuni tu aliweza kutoa msaada wa Set ya Computer na printer yake kwa ajili ya matumizi ua ofisi ndani ya skuli hio licha kuwa muonekano wa majengo ya skuli hio yamechakaa na hayaendani na matumizi ya Computer badala yake palihitajika pajengwe mwanzo.
Nazidi kujiuliza maswali mengi sana kwa upande wa Mbunge wa jimbo hili hivi hii hali ya skuli hii haioni au hajui kama wananchi waliomchagua watoto wao wanasoma ndani ya skuli hii tena kwenye  mazingra magumu ya tafutaji wa elimu,haoni kwamba anapaswa kutoa msaada wake tena wa hali ya juu,amesahau kuwa amepelekwa bungeni kuwatetea wananchi wake nilini amesimama bungeni na kuelezea hali halisi ya skuli hii angalau pengine angeweza kuwapa moyo wananchi wake kuwa anawatetea lakini wahusika ndio hawataki lakini hafanyi hivo.
Ushauri wangu kama ni mzaliwa wa kengeja waiteni viongozi wenu muwape matatizo ya skuli yetu wayapeleke kunako husika tusikae tukatupia lawama Serikali tu wakati hao wahusika wakuuu wakuyafikisha matatizo yetu hawajayafikisha kunakotakiwa nadhani tukifanya hili huwenda tukafanikiwa inshallah.pia NAPENDA KUMULIZA BILALI ALIPOTOWA MAONI YAKE NA KUSEMA MUUNGANO UNATIJA JE HII NI MOJA KATIKA HIZO TIJA ALIZOZITAJA.....?

1 comment:

  1. Kiongoz wetu mkubwa kwa kengeja ni sheha wa shehia hiyo ya kengeja lakin huyu mtu hafai hata kuwepo dunian kwa sasa ajira ngap zina kuja kengeja anaziuza kwa watu wa mbali sana sheha ni mshenz

    ReplyDelete