Monday, March 4, 2013

MAALIM SEIF ASEMA WAZANZIBARI HAWATAKUBALI KUKOSEKANA Z"'BAR YENYE MAMLAKA KAMILI



Chama cha wananchi CUF kupitia katibu mkuu wa chama hicho ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kimemuhakikishia   Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanganyika (Tanzania) , Jaji Joseph Warioba, kwamba Wazanzibari kwa umoja wao hawatokubali chochote kile ambacho kitasababisha kukosekana kwa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mfumo mpya wa ushirikiano na Tanganyika kupitia Muungano.
Maalim Seif aliyasema hayo huko Makunduchi mkoa wa kusini Unguja  alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho,amesema kutokana na matukio ya asilimia 66 ya maoni ya wazanzibar kutaka mamlaka kamili ya nchi yao basi hakun haja ya kutokuirjesha Zanzibar hadhi yake.
Kufuatia mkutano huo Maalim Seif amesema kuwa kwa sasa  Zanzibar haiwezi tena kukubali kukosa mamlaka yake ya kuwa na udhibiti wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa kwani imechoka na udhalilishaji inaofanyiwa na Tanganyika kupitia Serikali ya Muungano.
Aidha Maalim ametolea  mifano mbali mbali ambayo  Serikali ya Muungano imeilazimisha Zanzibar kujitoa  katika Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1993 pamoja na hatua ya hujuma iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, ya wiki iliopita ya kufuta maeneo ya ushirikiano yaliyohusu Zanzibar yaliyokuwa yawe sehemu ya makubaliano katika Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanganyika (Tanzania) na Oman.
Sambamba na hayo  Maalim Seif alitaja athari ya Zanzibar kukosa nafasi ya kufaidika na misaada ya kimataifa katika maeneo yote yasiyo ya Muungano kwani Tanganyika hutumia jina la (Tanzania) kujichukulia nafasi hiyo kwa manufaa na maslahi yake peke yake jambo ambalo limewatoa imani wazanzibar waliowengi kuendelea na Muungano huu uliopo sasa.
Maalim amefahamisha wazi kuwa  kwa sasa Zanzibar inataka kuwa na Wizara na Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na haitokubali chochote chini ya hapo. Amesema kuwa “udhibiti wa mambo ya nje ndiyo kigezo cha nchi kukubalika na kutambulika kimataifa na Zanzibar inataka kurejesha mamlaka hayo na kurejesha kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa”.

No comments:

Post a Comment