Saturday, March 2, 2013

MUENDESHA MASHTAKA MKUU WA ICC ATUWA NCHINI TANGANYIKA


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda, ametua nchini Tanganyika jana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.
Hatua hiyo ya ICC imekuja ikiwa ni miezi sita tangu Serikali ya Tanganyika (Tanzania) ilipopelekwa katika mahakama hiyo, iliyoko The Hague, Uholanzi kwa madai ya kukiuka haki za binadamu.
Malalamiko hayo maalumu yalipelekwa ICC na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Septemba 28 mwaka jana, baada ya kutokea kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na watu wengine 23.
Taarifa ya LHRC ilieleza kuwa pamoja na watu hao kuuawa, Serikali ilishindwa kuwachukulia hatua wahusika na kubana kimya kama kawaida yao.
Mbali na kuishtaki Serikali ICC, kituo hicho cha Sheria na Haki za Binadamu pia kilipeleka mashtaka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu.


Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk Hellen Kijo-Bisimba, alisema kuwa walifungua mashtaka hayo ili kuzitaka mamlaka hizo za kimataifa kufanya uchunguzi na kuichukulia hatua stahiki za kisheria dhidi ya Serikali ya Tanganyika (Tanzania).
Jana Rais Jakaya Kikwete alikutana na Bensouda Mwendesha Mashtaka Mkuu ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC) na kufanya mazungumzo  akiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi.
Katika maelezo yake Bisimba alisema: “Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanganyika (Tanzania) ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu.”
“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile. Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani,” aliongeza Dk Bisimba,Tulipomtafuta Jaji Werema kuzungumzia ujio wa Bensouda alisema kuwa Mwendesha Mashtaka huyo alikuwa mgeni wa Rais Kikwete, hivyo hawezi kueleza kilichozungumzwa.
“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanganyika  (Tanzania),” alisema Werema.
Kama ilivyokuwa kwa Werema, naye Feleshi alikwepa kuzungumzia ujio huo wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, huku akisema jambo hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Ikulu.LHRC ilichukua hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa mauaji ya raia wakiwa katika mikono ya vyombo vya dola, huku Serikali ikigwaya kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika.


Pamoja na hatua ya kushtakiwa kwa Serikali katika mamlaka hizo, Bisimba alisema kuwa bado wanataka kuona viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa namna yoyote na mauaji ya Mwangosi na raia wengine wakiwajibishwa. 

Alifafanua kwamba kuanzia Januari hadi Septemba mwaka jana, jumla ya watu 24 waliuawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama. 

Dk Bisimba alisema tangu mwaka 2001 hadi sasa, kituo hicho kimekuwa kikifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya mauaji yanayoendelea kufanywa na vyombo vya dola na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. 

Tayari watu wanne nchini Kenya wamefikishwa ICC wakikabiliwa na mashtaka ya kuhusika na vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya watu katika uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.
 E & P
Dondoo
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Septemba 28 mwaka jana kilipelekwa malalamiko Maalum ICC kuhusu mauaji ya watu 24.
Serikali inalalamikiwa kushindwa kuzuia na kuwachukulia hatua wanaohusika na mauaji ya watu 24 waliuawa katika wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensoud pamoja mengine kuulizia

No comments:

Post a Comment