Saturday, March 2, 2013

NCHIMBI KASHINDWA BABA YAKO NYERERE UTAWEZA WEWE HASIDI WA ZANZIBAR..???


SITI binti Saad, malkia wa waimbaji wa kike Wakizanzibari, aliwahi kuimba nyimbo iliyokuwa na maneno: “Unguja ni njema, atakaye naje.” Siti aliyaghani maneno hayo kwa madaha na maringo zaidi ya miaka 60 iliyopita lakini majisifu yake ya kuiringia nchi yake bado yanasibu…
Unguja na Pemba yake zote ni njema. Atakaye naje. Lakini aje kwa udhu na heshima. Aje akitambua kwamba Zanzibar ina maadili yake.
Visiwa hivyo vinaendelea kuwa visiwa vya amani na utulivu. Utulivu huo ndio moja ya sababu zinazowavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia kuizuru nchi ya Zanzibar licha ya shida ilizo nazo za miundombinu.
Jengine lenye kuwavutia wageni ni ukarimu wa watu wake na upendo wao wa kuishi kwa amani. Kadhalika wenyeji wake wana moyo mkunjufu kwa wageni na ndio maana Wazanzibari wakawa hivi walivyo na michanganyiko yao ya damu.
Tena ni watu wavumilivu. Nchi yao iliyo ya Kiislamu ndiyo chimbuko la Ukristo katika Afrika ya Mashariki. Kutoka huko Ukristo ulivuka bahari na kuenea katika eneo zima la Maziwa Makuu na bara ya Afrika ya Mashariki na ni nchi ya kislamu.
Hatusemi kwamba kwa kuwa na taswira hiyo Zanzibar ya leo ni pepo. Wala hatusemi kama hakuna vitendo vya uhalifu vinavyotokea.
Uhalifu upo. Mfano mmoja ni tukio la Februari 17 la kuuawa Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki.na la kupigwa mapanga sheikh Ali Khamis Ali.Hivi vilikuwa ni vitendo vichafu na uhalifu wa kinyama.
Binadamu yeyote yule anayedhulumiwa maisha yake akiwa padri asiwe padri akiwa sheikh asiwe sheikh anastahiki kuliliwa. Na aliyemuua anastahili kulaaniwa na kuapizwa kwa maapizo yote tuyajuayo. Tena asakwe mpaka apatikane ili atiwe adabu kama inavyostahiki.
Hadi sasa hakuna aliyejitokeza kudai kwamba alihusika na mauaji hayo na sababu gani zilizoyasababisha.
Serikali ya Zanzibar nayo hadi sasa haijatwambia mauaji hayo yalitekelezwa na akina nani. Haijatwambia kwa sababu ingali inaendelea na upelelezi na bado haijui wahusika ni nani na sababu gani zilizowafanya wamuue sheikh Ali na Padri Mushi.
Inasikitishakuona kwamba badala ya kusubiri matokeo ya upelelezi unaofanywa baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Muungano pamoja na baadhi ya viongozi wa Kikristo na vyombo vya habari wameyarukia mauaji hayo na wanayatumia kama fimbo ya kuwapigia Wazanzibari.
Mmoja wa viongozi walioshangaza ni Waziri wa Mambo ya ndani wa serekali ya Tanganyika, Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye mara baada ya Padri Mushi kuuawa aliruka na kuanza kutoa matamshi yasio na ithibati yoyote kwamba walioua ni ‘magaidi’.
Hivi karibuni aliuawa mchungaji Mathayo Kachila wa Kanisa la Pentekoste la Assemblies of God huko Geita lakini hatukumsikia Nchimbi akishutumu kwamba Kachila aliuliwa na magaidi.!!!! Wala hatukumsikia akitoa shutuma kama hizo Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga alipomwagiwa tindikali au alipopigwa mapanga imamu wa msikiti Sheikh Ali Khamis Ali na kuuawa hatukumsikia kabisa nchimbi je nchimbi upo...? au hawa sio watu..?
Kwa vile Nchimbi hana ushahidi wa matamshi yake yanakua matamshi ya uchochezi wenye kutia fitina. Dhamira yake ni kuipaka tope nchi ya Zanzibar na kuufanya ulimwengu uamini kwamba kuna mtandao wa kigaidi Visiwani wenye lengo la kuwaua Wakristo.
Nchimbi akijua vilivyo kwamba vyombo vya dola vinavyohusika vilikua vikiendeleana upelelezi na kwamba serikali yake ya Tanganyika imeiomba Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) iisaidie.
Inavyosemekana ni kuwa mashirika kadhaa ya kigeni ya upelelezi na ya kijasusi yameombwa yaisaidie serikali katika upelelezi huo. Nimedokezwa na chanzo kimoja nje ya Tanganyika kwamba Shirika la Ujasusi la Israel, Mossad, ni mojawapo ya mashirika hayo.
Mwaka juzi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliizuru Kenya. Baada ya ziara yake ofisi ya waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga ilisema kwamba Netanyahu aliahidi kusaidia kuunda ‘muungano dhidi ya itikadi kali ya kidini (ya Kiislamu)’ utaoziunganisha nchi za Kenya, Ethiopia, Sudan ya Kusini na Tanzania.
Mwaka jana nilitahadharisha kwamba kuna watu nchini wasioridhika na Maridhiano yaliopatikana nchini Zanzibar. Niliandika kwamba wakitakacho watu hao ni kuzusha fujo hapa nchini Zanzibar zitazoweza kuisambaratisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hata kuzusha hali zitazosababisha nchi isielewane na kuanza kuwa wenyewe kwa wenyewe na kusahau lengo kuwa la kutaka Zanzibar kuwa nchi kamili yanye mamlaka kamili.
Mkakati wao ni kuwatumia vijana wachochee fujo kwa kuwatomeza wenye jazba wachome moto makanisa ili ulimwengu uamini kuwa kwa Wakristo na Wabara Zanzibar hapakaliki.
Watasema kwamba wenye kuleta fujo hizo ni wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho. Halafu watawahusisha viongozi wa Jumuiya hiyo na mtandao wa kigaidi wa al-Qa’eda na kwa mpigo mmoja watawahusisha viongozi wa CUF na Uamsho na harakati zao.
Tangu nitoe indhari hiyo shutuma zote hizo zimetolewa hata kabla ya kuuliwa sheikh Ali na Padri Mushi. Na sasa zinazidi kushadidiwa.
Wenye kutoa shutuma hizo wanatumai kwamba wataweza kuwafanya wakubwa wa dunia hii waiangalie Zanzibar kwa jicho jingine. Wanachotaka hasa ni kuzizima harakati za kuujadili Muungano feki na kuudhoofisha mshikamano wa Wazanzibari.
Wengine wenye kushtusha ni waandishi wa habari walioamua bila ya kufanya utafiti wowote kwamba magaidi wenye funganisho za kimataifa ndio waliomuua Padri Mushi, kwamba magaidi hao wanahusika na Uamsho. Na kuna waliosihi jumuiya hiyo ipigwe marufuku.
Ukweli ni kwamba kwa muda unaokaribia miezi sita viongozi wote wa Uamsho wameshikwa na wako jela wakisubiri kesi walizoshitakiwa. Muda wote huo wafuasi wao hawakufanya fujo. Wameusikiza (wametii) wito wa viongozi wa kisiasa Visiwani wakiwataka wawe watulivu.
Waandishi wengine wakafika hata kudai kwamba hao ‘magaidi’ wana wenzao ndani ya Serikali ya Zanzibar.
Huo ni uzushi na uzandiki usiofaa kuandikwa na mwandishi yoyote wa maana. Ukweli tuujuavyo ni kwamba hakuna ushahidi wowote wenye kuonyesha kwamba kuna mtandao wa kigaidi Zanzibar wenye kuwalenga Wakristo.
Kitisho cha ugaidi kipo Tanganyika kenya uganda na ulimwengu nzima na kinatokana na magaidi wa wasio julikana wenye kutishia amani ya kanda ya Afrika ya Mashariki.na hata ya asia na bara la ulaya na afririka ya kusini Lazima taifa liwe macho kukikabili lakini tusikikuze kuliko kilivyo.
Ukweli mwingine ni kwamba Waislamu wa Zanzibar, ambao takriban ni asilimia 98 ya wakaazi wa visiwa hivyo, wataendelea kuishi kwa amani na ndugu zao wachache Wakikristo na Wakihindu.
Ikiwa nia ya maadui wa Zanzibar ilikuwa kuyatumia mauaji ya Padri Mushi na sheikh Ali kwa kuliharibu jina la nchi ya Zanzibar na kuyadanganya mataifa ya nje kuhusu ugaidi basi hawakufanikiwa na kina nchimbi na wezako hamukuanza nyinyi vitimbi vya kuichukia nchi ya Zanzibar kanza baba yenu nyerere na leo hii yuko wapi...? je Zanzibar iko wapi nchimbi..?
Madola ya Magharibi hayakushtushwa na matamshi ya Nchimbi na ndio maana hayakutoa taarifa za kuwazuia au hata kuwatahadharisha wananchi wao wasiizuru nchi hii ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment