Saturday, March 23, 2013

RAISI WA CHINA XI JINPING-(BANDARI YA BAGAMOYO)ATATUWA NCHINI TANGANYIKA NI ZIARA YAKE YA KWANZA BARANA AFRIKA



Dar es Salaam. Rais wa China, Xi Jinping anatarajiwa kuwasili nchini Tanganyika kesho kwa ziara ya siku moja, ambapo pamoja na mambo mengine atasaini mikataba 17, kati ya nchi hiyo ya china na Tanganyika, ukiwamo wa ujenzi wa Bandari  mpya ya kisasa ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani.je nini thamira ya nchi ya Tanganyika kujenga bandari hii..???                                                                                                                                                                                    Ujenzi huo utakaofanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China, utakwenda sambamba na ujenzi wa barabara inayounganisha bandari hiyo na Reli ya Kati na Mamlaka ya Reli ya Tanganyika na Zambia (Tazara).              Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ujio wa rais huyo aliyechaguliwa wiki mbili zilizopita, utakuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yetu ya Tanganyika.
“Mbali na mkataba huo pia tutasaini mikataba wa kidiplomasia. Vilevile, China imefungua soko la Watanganyika kuuza tumbaku nchini humo na mkataba wa kuliendeleza Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC),” alisema Membe.
Waziri huyo alisema kiongozi huyo wa China pia atafungua jengo la kisasa la mikutano la Mwalimu Nyerere.
“Kwa kuwa anakuja Afrika kwa mara ya kwanza huku Tanganyika ikiwa nchi ya kwanza, Jinping pia atatoa hotuba yake juu ya msimamo wa China kwa Tanganyika na Afrika kwa jumla,” alisena Membe.
DR KUMBI SHEIN JE KIKWETE KAJA KUKUOMBA RUHUSA YA KUJENGEWA BANDARI BAGAMOYO..???

No comments:

Post a Comment