Wednesday, March 6, 2013

SCHOLARSHIP ZA BABU SULTAN QABOOS WAZANZIBARI WAMBIWA MPAKA WAWE NA VITAMBULISHI VYA KITANGANYIKA NDIO UPEWE.DUUUUUUH



Tumefurahi sana kupata fursa hii adhimu kupatiwa msaada wa elimu ya juu kutoka serikali ya Oman (sultan qaboos scholarship) kwa Zanzibar. Misaada hii inalenga elimu ya juu – kuanzia kiwango cha degree ya pili hadi Phd.Ninachokifahamu ni kuwa baada ya miaka kama mitano hivi na ushei, tutaanza kuona matunda yake, na ile ‘roll out’ plan yake itaendelea. Mimi mtazamo wangu ni kuwa Zanzibar itapiga hatua kielimu sana — tutatoa wataalam na wasomi, the, watarudi nyumbani (kama watarudi) halafu watasaidia wenzao.
Hata hivyo, kuna harufu tayari kuwa misaada hii inaaza kutumika vibaya, na imeanza kuchakachuliwa na watendaji wakuu serikalini. Namsifu sana Prof.Idrissa Rai kwa uwezo wake wa ubunifu na maarifa kwa masuala kama haya. Yeye anaona mbali sana, na maskini, hana tamaa wala hisia za rushwa, lakini majuntar wa SMZ-CCM watamuangusha na kumtia aibu mbele ya hadhara ya duni na academicians wenzake. Prof.Rai, ukweli hasa hana tamaa wala khulka hizi za rushwa na ila mbaya. Ni mtu mzuri na msafi, ni mwanataaluma na mtaalamu. Anaipenda Zanzibar yake,but amezungukwa na na majuntaris.     
1. wanachukuliwa watoto wa wenyewe kwa wenyewe (wakubwa serikalini au CCM) na kuwapatia nafasi hizi. Hawa hawana sifa, ila vinatafutwa vyeti feki na kufanywa kuwa wamepasi kupita kiasi. Serikali ya Oman imeweka msisitizo kuwa wanataka watu wenye viwango na sio kutoka ‘maskani za CCM’.                                                                                        2. Umri: Aghlab wanataka umri kati ya miaka 25 kwa master degree na nafikiri kama 35 kwa Phd. Kinachofanyika, ni kuwa vizee vinabuni vyeti fake vya kuzaliwa na kujidogosha (kujipunguzia umri) ili na wao wapate kusoma na tabaan flus nje nje za Qaboos.Ushahid — hebu tembeleeni pale ofisi ya Mrajis wa Vizazi na Vifo (registrar general office) mkaone mambo — hapo ni pesa, toa rushwa upatiwe cheti cha kuzaliwa — hata kama unataka kuwa miaka 18, utakuwa tu. Hii ndio hali tuliyonayo hapa Zanzibar.
3. Urasimu katika kuchagua majina: hata kama unazo sifa – kama hujulikani — sahau, na kama ni mwanamke (unajua tena nini kitafanyika………hutaki kutoa vya watu usipatiwe). Kwa wanaume, kidogo lazima upitishe rupia, ili uondoshe udhia.  Je, kweli Zanzibar tutasonga mbele na kupiga hatua kama hali yenyewe ndio kama hii..?? Mjue kuwa Watanganyika hawajalifurahia suala hili. Na wao wanapenyeza watu wao. Kigezo sio Zanzibar ID, ila ni TZ ID. Upo hapo.? kwa hivyo, Mtanganyika yeyote anayo haki ya kusoma kupitia scholarship hii...? Utamjuaje Mzanzibari..? Kama yupo mtu anielezea (nakusudia kwa mazingira ya sasa hivi….kuwa mpaka Warwanda,Burundi, Waganda,Wakenya n.k.  wanazo Zanzibar  ID.Kama hatujaamka, sidhani kama tutaamka tena maisha. Juzi Maalim Seif anasema kuna njama akina Membe wanataka au wameshazuia misaada kwa ajili ya Zanzibar (refer mkutano wa Makunduchi na hotuba yake ambayo pia amegusia suala la OIC). Hili ni hakika kabisa……ila sisi Wazanzibari hatujataka kuamka, akina Mwinyihaji, Machano na wenzao bado wamelala fofofofofofofo; Tanganyika kila siku ya Mungu wanazidi kuitafuna Zanzibar kwa kila hali. Sasa wamechomekea suala la ‘udini’ na hii ndio nyimbo yao na itakuwa hivyo miaka yote mpaka mwisho wa dunia. Sasa wameshapata nyimbo.

No comments:

Post a Comment