Saturday, April 6, 2013

MAASKOFU NCHINI TANGANYIKA WASABABISHA MSIKITI KUCHOMWA MOTO TUNDUMA MKOANI MBEYA


Agizo la Baraza la Maaskofu kuwataka waumini wao kuchinja na kuacha mara moja kula nyama inayochinjwa na Waislamu, limezua balaa mjini Tunduma mkoa mbeya nchini Tanganyika.
Msikiti mmoja umechomwa moto huku mwingine ukinusurika kimaajabu kama ilivyonusuriwa Al-Kaaba ilipovamiwa na Jeshi la Tembo.
Hayo yametokea kufuatia vurugu zilizotokea juzi kutokana hatua ya baadhi ya maaskofu kulazimisha Wakristo kuchinja katika machinjio ya mji hii ni kuonyesha wazi kuwa wakiristo siku zote ndio huanza bala.
Taarifa kutoka katika mji huo mdogo wa Tunduma zimeeleza kuwa, vurugu hizo zimeibuka baada ya Maaskofu kudaiwa kuhamasisha na kutekeleza maagizo ya Baraza lao la Maaskofu la Taifa (TEC), likiwataka Wakristo kuchinja.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa kabla ya kuibuka kwa vurugu hizo siku ya Jumatano wiki hii, palifanyika kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Kamanda wa Polisi mkoa (RPC) pamoja na viongozi wa Dini, Maaskofu na Masheikh.
Hata hivyo, Maaskofu hao imedaiwa kugomea rai ya Mkuu wa Mkoa, pale alipowataka kuwa na subira wakisubiri, wakati Serikali ikilitafutia ufumbuzi suala hilo kitaifa.
Katika vurugu hizo, baadhi ya mashuhuda wamemueleza muandishi wetu wa free zanzibar people from mkoloni mweusi wa siri kwa njia ya simu kuwa, Msikiti wa Ijumaa, Masjidi Jamaa, mjini hapo ulinusurika kuchomwa moto na Wakristo, waliokasirika kuzuiwa kuchinja huku Msikiti mpya ukiharibiwa vibaya na kuchomwa moto na Wakristo hao.
''Sijafanya tathumini kamili, kutokana na uharibifu huo, lakini kwa haraka haraka ninavyoona hapa inaweza kufika kiasi cha Tsh. 12 milioni''
Alisema Ustahi Nassoro Msham, akithibitisha uharibifu uliofanywa katika Msikiti huo.
Akisimulia, tukio hilo, kiongozi wa Masjid Jamaa, Ustadhi Twahir Mussa, alisema vurugu hizo zimetokana na Maaskofu kulazimisha kuchinja, na kukaidi maelezo ya Mkuu wa Mkoa Bw. Abbas Kandoro.

Alisema, kabla ya vurugu hizopalifanyika kikao kikubwa Mjini hapa kilicho shirikisha Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC), na maofisa wengine wa Mkoa kwa ujumla.
Alisema Ust.Twahir kwamba katika kikao hicho, kilichofanyika katika Hoteli ya Ukinga Hill, Mkuu wa Mkoa, Bw.Kandoro, alisisitiza kuheshimu maamuzi ya Serikali, kwamba suala la kuchinja libaki kama lilivyokuwa awali wakati likitafutiwa ufumbuzi wake.
''Maaskofu walimjibu Mkuu wa Mkoa kuwa wao wamepata maagizo kutoka kwa viongozi wao wa Baraza la Maaskofu Tanganyika (Tanzania) (TEC), na waliisoma barua ya maagizo hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Bw.Abbas Kandoro, na RPC.""
Imedaiwa kuwa baada ya hapo Wakristo hao walifanya nguvu kuchinja siku ya Jumatatu na Jumanne, bila kuruhusiwa baada ya kuhamasishwa na Maaskofu wao wa Taifa.hii ni uwazi kabisa kuwa Wakristo hawasikilizi serekali wao wanasikiliza viongozi wa wa Kanisa yani Maaskofu wao. Ustadh Twahir alisema walewaliogoma kuchinjiwa na Waislamu, walinukuu maagizo ya Maaskofu wao kuwa ni marufuku kula kilicho chinjwa na Waislamu, hivyo walidai hawawezi kwenda kinyume na viongozi wao.
Twahir alisema baada ya kugomewa kuchinja, walianza kufanya fujo mitaani na chaajabu alidai fujo hizo zilielekezwa katika Misikiti hapo mjini.
Alisema, kundi kubwa la Wakristo walivamia Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Masjid Jamaa, wakiwa na matairi ya magari na petroli, lakini zoezi la kuwasha moto lilishindikana kwa Kudra za Mwenyezi Mungu.
''Matairi yalikuwa yanatoa moshi tu bila kuwaka, mpaka walipofika askari na kuanza kuwakamata na kuwatawanya, na wengine wakakimbia ''. Alisema Ustadh Twahir.
Nassoro Msham, aliye msimamizi wa Msikiti uliovunjwa na kuchomwa moto, alisema Msikiti umebomolewa kuta, milango na madirisha sambamba na kuchomwa moto, majira ya saa saba mchana siku ya Jumatano.
Ust. Mussa, alisema Msikiti hua umejengwa kwa nguvu za Waislamu, katika harakati za kuongeza nyumba za Ibada kwa Waislamu, pamoja na mafundi wanaojenga barabara iendayo Sumbawanga.

Kwa upande wake alisema, sababu kubwa za vurugu hizo ni mvutano wa suala la kuchinja, ambapo alifika Mkuu wa Mkoa na kukutana na viongozi wote wa Dini, na katika kikao hicho, alishauri suala hilo wasubiri maamuzi ya ngazi za juu baada ya Waziri Mkuu kukutana na viongozi wa Dini.
Lakini alisema, Wakristo hawakukubaliana na maelezo hayo ya Mkuu wa Mkoa Mw. Abasi Kandoro, ambapo siku ya Jumatano wiki hii, walikusanya ng'ombe wao nakwenda machinjioni, lakini ilishindikana wao kuchinja kutokna na ulinzi kuwa mkali.
'' Waliposhindwa huko sasa walirudi huku mjini kwa jazba kubwa na hasira, walianza kufanya maandamano na fujo za kila aina, kwakweli hali ilikuwa ni mbaya kwa siku nzima hapa Tunduma '' Alisema Ustadh Mussa.
Ustadh Mussa alisema vurugu hizo zilizidi na Wakristo hao walianza kuelekea katika Misikiti ya Mjini na kuvamia Msikiti Mkubwa wa Ijumaa.
Alisema, baada ya kushindwa kuudhuru Msikiti huo, ambapo moto waliowasha ulikuwa ukigoma kuwaka kuchoma Msikiti, ndipo walielekea katika Msikiti uliopo mbali kidogo na eneo hilo la mjini, katika Msikiti mpya uliokuwa ukiendelea kujengwa, wakiwa na mashoka, mapanga na mawe pamojo na vyuma.
'' Huu Msikiti ulikuwa katika hatua za mwisho za ujenzi, ulikuwa ushapigwa bati, plasta, na kuwekwa milango na madirisha, tulikuwa katika hatua ya kuweka sakafu tumalizie, sasa wamechoma moto bati zimeungua na chini kumebomolewa '' Alisema Ustadh Masham.
Alisema, wakati tukio hilo likitokea, la kuchoma na kuvunja Msikiti huo, Waislamu walikuwa eneo la mjini wakilinda Misikiti hiyo, na hawakudhania kuwa Wakristo hao watafika huko kutokana na umbali wake.
Alipoulizwa kama kuna Waislamu waliokamatwa katika vurugu hizo, alisema katika tukio hilo Waislamu, hawakujibu mashambulizi, bali muda mwingi walikuwa Msikitini pasi na kutoka.

No comments:

Post a Comment