Friday, April 19, 2013

MAMILLIONI YOTE MNAYO IBAA MUMESHINDWA KUNUNUWA MACHINE YA X-RAY KATIKA HOSPITALI YA CHAKE CHAKE..??



Ukienda hospital ya Chake Chake, ukiingia tu – utakutana na walinzia wanne kwenye geti (inaonyesha walikuwa askari hapo kabla, na sasa wastaafu je wamestafu lakini kula yao ndio hapo mlangoni sasa..??
Niwachane na hilo hospital hii kwa miaka sasa, haina machine ya X-Ray. Ukiumia, unaweza kukaa hapo mpaka utasahauliwa maana jawabu inakuwa ‘hatuna X-Ray machine’. Basi. Ukipata jamaaa yako atakuhangaikiaa weee, la kama huna kama mimi  weee utaka mpaka usema bora waukate basi kama ndio hakuna la kufanya kuliko maumivu haya mguu utaoza au mkono utavimba na kunuka. Hiyo ndio SMZ hiyo ndio mapinduzi daima, mapinduzi daiama,mapinduzi daima na sasa imeongezeka SMZ-GNU.
X-Ray ipo hospital ya Mkoani, ukimaliza huko uilete Chake-Chake. Unaweza pia baada ya kuhangaika kupata hiyo X-Ray Mkoani, Chake-Chake hakuna mtaalam wa kusoma picha  X-Ray. hilo ndio jawabu utakalo powa Ngoma hiyo.Kadhalika, Mkoani wanayo X-Ray machine, lakini hakuna msomaji umesikia wapi mambo kama haya ni hapa kwetu tu, uilete Chake-Chake. wapi utapata mambo mazuri kama haya only yapo hapa nchini kwetu Zanzibar tu.
Jamani hii ndio halisi inayoikabil hospital yetu au zetu zote ndio ziko hivyo ndani ya nchi yetu ya Zanzibar. nimesema mara nyingi watu wanajirundika vyeo tu na kutapia mlo wa mapesa ya posho ilhali kuna watu wanatesaka kila siku kwa sababu yakuwa na viongozi wasio juwa kazi zao wao waulize kuiba na kujirudikia mali tu. Mimi nasema haya kwa kuilaumu serikali hii yamajambazi watupu kuanzia raisi wake jambazi maana hakuchaguliwa kaekwa tu na mkoloni mweusi.mpaka mawaziri wake na wabunge wote majambazi. na sisi Wazanzibari pia tunajitakia wakati mwengine maana tunasoma kila siku kwenye magazeti kwenye mainteneti jinsi nchi ilivyo na viongozi wanavyo ibaa na kuibaa tena na tena. lakini tumekuwa kama madondocha siku za uchanguzi zikifika tunawachanguwa hao hao kisa nini umepewa t.shirt ya chalse au ya real madrid na panga au man utd  na wanawake nao mukisha pewa gora au upande wa kanga kwisha habari mpaka lini mambo haya..??
Hii ndio hali halisi inayotukabil na inayowakabil wananchi wetu. Nimekwenda pale mara kadhaa, nimeona walioanguka na mikarafuu, hawana matibabu, wanayayatika tu kitandani mbona watoto wao hatuwaoni katika hospitali hizi kwa nini..??  hatujiulizi kama hospitali hizi ni nzuri mbona watoto wa viongozi au wake zao hatuwaoni wakaja katika hospitali hizi..??  kutibiwa au kulala kitanda kimoja watu wa tatu au kulala kwenye sakafu hata siku moja halitoke basi sisi rai tutakuwa wajinga mpaka lini huu ni mwaka wa 2013 sio mwaka 1225 Wazanzibari kama hamja amka wala hamta amka tena nchi zote zina maiendeleo na zisizo na maendeleo zote washawatimuwa viongozi majambazi sisi bado tu kinyoko wetu wee kinyoko wetu wee hakujali kama anakujali kweli wangelitujengea hospitali za maana maskuli ya maana barabara za maana vyakula vya maana mbona mpaka leo bado tunakula mchele wa bembe na walisema bembe basi..??  lakini wao huo sio mpango wao wala nia yao ndio mukawaona kila kukicha magari mapya na safari zisokwisha maana wanawatengezea familia zao na watoto wao wakija wakivuliwa uongozi mambo yao ni poa sisi tumebaki pale pale.
Kila kukicha Ziara za viongozi kuja pemba ni nyingi mno, wanapishana ama njiani au airport – lakini hakuna action. Hakuna huduma, (delivery ya serikali ni zero); BLW wanapiga kelele zisizokuwa na dira wala maana, kiasi tu na wao waseme au waonyeshwe kwenye tv kuwa na wao wanasema mbona hayatekelezwi nikuwa wote lao moja kujionyesha basi wakisha wanagawana bahasha za pesa nchi iko vile vile inanuka kuanzia hospitali mpaka mitaani. Kwani machine ya X-Ray ni shilllingi ngapi jamani eeeee..??hebu natujiulize Wazanzibari machine ya X-RAY ni shillingi ngapi..?? Na je, XV Prado wanayopanda wao na kujirigia nayo ni shillingi ngapi..??  moja tu sio yote moja tu ni shillingi ngapi..?? Wazanzibari tukisha pata jibu tujiulize tena je ikiuzwa kwa mfano haiwezi kununua angalau used X-Ray machine..?? ikiwa inawezakana mbona basi hauzi na wao ni viongozi wetu watupendao ili inunuliwe mashine iwasaidiye watu lakini hilo haliko sisi na tufe siku za uchanguzi tuwatiliye tena kura wakiendelea kujitajirisha na sisi tunasuguwa lami tu mpaka lini..???
Dr.Shein, Rais aliye wekwa na mkoloni mweusi atumalize- yeye hii ndio fani yake si ni dokta yeye au ndio vyeti vyakujipandikizia tu..??,sina haja wala ya kusema chochote hapa. Hivi ameshindwa wapi..?? Juma Duni (CUF) ndiye waziri wa Afya alikuwa onyeshe mfano kuwa CCM walikuwa na wizara ya afya hawakufanya kitu sasa tunayo sisi CUF tunafanya hivi na hivi na kujenga hospitali mpya na ambazo zimecheka kusafishwa na kurekembishwa na kama ni dongo waziongeze lakini wapi waswahili wanasema mwana wa nyoka ni nyoka tu nini duni kafanya mambo yako vile vile kama yalivyokuwa na CCM je Babu umeshindwa wapi..?? tatizo liko wapi,au ndio mutatupa jibu la kusema kuwa maalim si raisi..?? hahahahahhaha bora ni cheke hahahahaha je, mnahitaji msaada gani..??
Ziara za Pemba kwa Dr.Shein, Maalim Seif, na Balozi Seif — kila siku, ina maana hamuioni hali hii. Tuseme ndio hakuna pesa katika serikali.kama hakuna pesa katika serekali punguzeni vinghora ili pesa zipelekwe hospitali.Balozi Seif juzi juzi tu katowa mapesa tele kumpa mpinda ati kwajili ya watu walioangukuwa na ghorofa unaziba kwa mwenzako wakati kwako kunavuja ndio haya.raisi watatu katika visiwa hivi viwili munashindwa kuvibadili maana yake nini..?? Basi kama hamuweze simujiuzulu tu munangangania nini au munapenda huo uluwa...?? japokuwa watu wanakufa na kuteseka...??
Nakumbuka sana hospital hii miaka ya 70s pale Chake Chake.Ilikuwa super hospitali hii sana kwa wakati ule. Ninaijua vizuri hospital hiyo na viunga vyake mpake kule kunaitwa ‘banda taka’. Nakumbuka kuna mikoko migi sana maeneo yale. Juzi nimezuru tena kuhudhuria shughuli ya harusi ya rafiki yangu mpenzi hapo, ndio nimeona hayo niliyoyaona ni aibu na kinyaaa kabisa hata kuku hafai kutibiwa kweli viongozi wa nchi hii ni viongozi au waganga njaa tuu...??

No comments:

Post a Comment