Friday, April 19, 2013

NKOMA AWATIA WATANGANYIKA UKOMA KATIKA SIMU ASEMA ASIYESAJILI SIMU FAINI SH 500,000 AU JELA MIEZI SITA



Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanganyika (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.(swali ni nchi gani ulimwenguni inayo sherea kama hii au ndio udikteta wenu kuwanyama watu uhuru)
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano   mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Profesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh milioni 3 na kifungo cha miezi 12.
“Katika vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na Aprili 11 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanganyika na kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na uvunjifu wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika  jamii.
Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu  ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia 93 na asilimia 7 hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki 
UHURU WA WATU UKO WAPI..?? HUSNI MUBARAUK ALIKUWA HIVYO HIVYO FUNGA MITANDAO JAMII MARA ZIMA INTANETI MARA ZIMA SIMU ZOTE MARA KATA UMEME LEO YUKO WAPI MUBARAUK..??

No comments:

Post a Comment