Wednesday, April 17, 2013

PINDA ATAKA KUENDELEA KUWAPINDA WATANGANYIKA WENZAKE WAMSHTUKIA


UKIMUONA KWENYE PICHA HII UTATHANI ANAWAJALI KWELI KWELI WATANGANYIKA MASIKINI WALIO KATIKA HALI NGUMU KUMBE YEYE NDIE ANAE WAUWA KWA KUJIRUDIKIA MAMILIONI YAPESA KATIKA OFISI YAKE AKIDAI ATI NI ZA MAZISHI YA VIONGOZI WATAKAO KUFA DUUUUUUH PINDA UMECHEMSHA.
Baada ya kujulibikizia mamilioni ya pesa katika ofisi yake akidai ni kwajili ya maziko ya viongozi watakao kufa duuuuuh!!! Pinda anaonyesha kuendelea kuwapinda Watanganyika bila huruma kabisa. Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2013/2014, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Sh123 bilioni (123, 401,059,000) kwa ajili ya Mfuko wa Bunge na Sh4 trilioni nne, (4,226,123,954,802) kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi ikiwa ni matumizi ya kawaida na fedha za maendeleo za ndani na nje, ambapo kati yake ameomba kiasi cha Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi.

Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Dada Lucy Owenya ndiye aliyeibua hoja hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi hiyo iliyowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliposema inashangaza kutenga mabilioni kwa watu watakaokufa badala ya kuwekeza fedha hizo kwa maendeleo ya walio hai.
Anasema Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, Serikali inawajali viongozi watakaokufa na kupuuza kuutatua matatizo ya akina mama wajawazito wanaolala chini au wanne kitanda kimoja katika hospitali nyingi nchini humu alisema Dada Lucy Owenya.
Owenya akaitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kupunguza fedha hizo na kuzitumia  kujenga chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi pamoja na kuisaidia Hospitali Teule ya St Joseph kununua vitanda vya wodi ya wazazi.
“Ni aibu na fedheha kubwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya maandalizi ya kuzika viongozi, huku mambo muhimu na ambayo ni kipaumbele yakiachwa, hivi mmetenga kiasi hicho kwani mnajua nani atakufa na lini atakufa ndiyo mnajiandaa kumzika, ni aibu kutenga kiasi kikubwa hiki cha pesa kwa ajili ya watu watakaokufa na ambao kwa sasa wapo hai…Kwa nini pesa hii isitumike kwa maendeleo ya watu walio hai,” anahoji Dada Lucy Owenya.
Mbunge huyo akaongeza kusema Serikali imeshindwa kufikiri hasa namna ya kuwaondolea umaskini na taabu wanazopata wananchi wake lakini inathibutu kutenga kiasi kukubwa cha fedha kwa ajili ya kuwazika viongozi ambao bado wapo hai.
Mbunge mwingine aliyeonyesha kukerwa na bajeti hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu ni Kangi Lugola wa Jimbo la Mwibara (CCM) anayesema licha ya kuwa mbunge wa CCM haungi mkono bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kile aliochosema kitendo cha kutengea Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi watakaokufa ni ubadhirifu.
Lugola ameongeza kuwa hataunga mkono bajeti hiyo kwa sababu hajui atakufa lini.
“Mazishi gani ya viongozi kwa shilingi bilioni moja..?? Huu ni wizi mtupu ndani ya Serikali, kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo..?? Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” anasema.
Mbali na wabunge hao, wanasiasa wengine wamezungumzia bajeti hiyo ya Waziri Mkuu na kusema Serikali inapaswa kuwa makini na matumizi ya pesa za wananchi na kuzitumia kwa manufaa ya maendeleo yao na siyo ya kundi dogo la viongozi walio katika bunge hili hapa mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama  cha APPT-Maendeleo, Peter Kuga Mziray anasema ni makosa makubwa kutenga kiasi kikubwa hicho cha pesa kwa masilahi ya viongozi huku ukipuuza matatizo yanayowakabili wananchi walio wengi ambayo yangewezwa kumalizwa kwa kiasi kidogo tu cha fedha.
Mziray anasema kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya maziko ya viongozi ni kikubwa kiasi ambacho kingetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vingepatikana viwanda vingi ambavyo mbali na kutoa ajira kwa vijana wa Wakitanganyika, lakini vingeongeza soko la bidhaa zinazolimwa na wakulima maeneo mengi nchini.
“Ujenzi wa kiwanda chochote kiwe cha kusindika bidhaa za kilimo au mifugo hauzidi Sh300 milioni. Sasa kwa Sh1 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maziko ya viongozi ambao wapo hai tungepata viwanda si chini ya vitatu....hapa wananchi wangepata ajira na hata wakulima wangekuwa na uhakika wa soko la bidhaa wanazolima,” anasema Mziray.
Anaongeza kusema kuwa ingawa hapingani na utaratibu wa kuwa na fungu kwa ajili ya mazishi ya viongozi, lakini anadhani siyo sawa fungu hilo likawa kubwa namna hiyo hasa ukizingatia kuwa tabia ya Watanganyika kushiriki kwa hali na mali shughuli za misiba hususan ile ya viongozi.
“Hapa Tanganyika tuna utaratibu msiba ukitokea wananchi wenyewe wanajichangisha, sasa Serikali haina sababu ya kutenga kiasi hiki kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwazika viongozi, na badala yake itenge kiasi kidogo huku jukumu la msiba likiachwa kwa wanafamilia pamoja na marafiki kama ilivyo kwa wananchi wengine,” anasema.
Mziray akawataka wabunge kuwa kitu kimoja katika kuikosoa Serikali bila kujali itikadi za vyama vyao kwa kile alichosema wabunge kwa ujumla wao ndiyo wanaoweza kuinyoosha Serikali ikakumbuka vipaumbele vya taifa na siyo kuangalia kundi dogo la viongozi.
HANA HURUMA KWA WATANGANYIKA WENZAKE KWELI ATAKUWA NA HURUMA KWA WAZANZIBARI..?? YAGUJUUUUUUUUUUUUU TUACHIWEEE TUPUMUWEEEEE


No comments:

Post a Comment