Friday, April 26, 2013

SAMIA SULUHU ASEMA WATU WENGI HAWAUJUWI MUUNGANO VIJIJINI ZANZIBAR!!!


SAMIA SULUHU KUMBE NI MGOGO ASILI YAKE NDIO MAANA KAZI KUOMBA OMBA APATE KUMALIZA MJENGO WAKE ANAO UJENGA ANAJIDAI ATI ANATAKA ASAIDIWE ILI AWAFIKIYE WATU WA VIJIJINI AWAELIMISHE NINI MAANA YA MUUNGANO WEWE MAMA WATU WA ZANZIBAR WANAUJUWA MUUNGANO KULIKO WEWE MTAPIA MLO MWENYE NJAA USIYE SHIBA UNATAKA KUIYUWA ZANZIBAR KWA MADARAKA MUTAKUFA NYINYI KISHA TUTAWAOMBEA SAADA ZA KUWAZIKA MAANAMUMEZOWEA KUOMBA SIO ZANZIBAR MUTAIWACHA HAPA HAPA.
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu amesema miongoni mwa changamoto anazokabiliana nazo ni kukosa rasilimali za kumwezesha kuwafikia watu hasa wa vijijini na kuwaelewesha dhana nzima ya Muungano.
Waziri Sululu alitoa kauli hiyo mjini hapa alipotembelewa ofisini kwake na Balozi wa Uingereza nchini, Diana Melrose, ambaye alitaka kujua changamoto anazokutana nazo katika nafasi aliyonayo.
Waziri huyo alisema kuwa watu wa vijijini wengi hawaelewi Muungano, hivyo kumuomba balozi huyo kuzungumza na wafadhili wengine, ili wawapatie rasilimali za kufanikisha lengo hilo.
Aidha, Balozi Melrose alipenda kufahamu zaidi kuhusu maoni ya waziri juu ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar na pia changamoto zitokanazo na muungano huo.
Waziri Suluhu alisema kwa upande wake anaona ni bora kuendelea na Muungano kuliko kuuvunja na kushauri mabadiliko yafanyike ili kuuboresha.
Pia alisema yapo makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii hivyo hutumia nafasi waliyonayo kuwashawishi wananchi kuwa Muungano uvunjike sababu hauna maana.

Alitoa mfano wa baadhi ya makundi hayo ni wanasiasa na viongozi wa dini akisema sababu wao wanao ushawishi mkubwa katika jamii.
Akijibu swali la Balozi Melrose ambaye alitaka kujua kwamba inasemekana watu wa Zanzibar hawana furaha sababu ya Muungano hivyo ndiyo maana wanashauri uvunjwe, alikiri kuwapo kwa watu hao na kusema hali hiyo anafikiri inatokana na ubinafsi

No comments:

Post a Comment